Author Archives: Dr. Makirita Amani

About Dr. Makirita Amani

Dr. Makirita Amani ni daktari wa binadamu, mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali. Dhumuni lake kubwa kwenye maisha ni KUWASAIDA WATU KUBORESHA MAISHA YAO NA KUFIKIA MAFANIKIO MAKUBWA KUPITIA KAZI ANAZOFANYA. Mawasiliano 0717396253 email makirita@kisimachamaarifa.co.tz

UKURASA WA 1177; Tatizo La Kufanya Unachopenda…

By | March 22, 2018

Kufanya unachopenda ndiyo njia ya uhakika ya kupata mafanikio makubwa kwenye maisha. Siyo tu kifedha, bali hata ile hali ya kuridhika na unachofanya. Lakini sasa, wapo wanaofanya kile wanachopenda, lakini hawajapiga hatua kubwa kwenye maisha yao, wako pale pale ambapo wamekuwepo miaka yote. Kwa sababu hii basi, wengi wamekuwa wakiona (more…)

UKURASA WA 1176; Jikumbushe Maisha Yalikuwaje Kabla Ya Ulichozoea…

By | March 21, 2018

Mazoea ni sumu mbaya ambayo imekuwa inawasahaulisha watu kule walipotoka na kujikuta wanafanya makosa ambayo yanawarudisha kule walikotoka. Chukulia mfano wa mtu ambaye hana kazi, na maisha ni magumu, anaomba sana apate kazi, hata kama ni kazi yoyote na ataifanya kwa moyo kwa malipo yoyote. Kwa kuwa mawazo hujenga, basi (more…)

UKURASA WA 1175; Wakati Mwingine Siyo Makosa Yako…

By | March 20, 2018

Kuna wakati tunafanya kila tunachopaswa kufanya, tunajitahidi kuhakikisha kila kitu kinakwenda sawa, na tunategemea kupata matokeo bora kwa hatua tulizochukua. Lakini kinachotokea ni tunapata matokeo ya tofauti kabisa, matokeo yanakuwa mabaya kama vile hatujafanya kitu kabisa. Hapa ni rahisi kuanza kujilaumu na kuona kwamba tuna matatizo fulani. Tunaweza kuona tuna (more…)

UKURASA WA 1174; Usipange Kutokufanya Kitu Fulani, Ni Njia Ya Kushindwa….

By | March 19, 2018

Katika mipango yetu ya maisha, kuna vitu ambavyo tumekuwa tunafanya ambavyo vinaturudisha nyuma au vinatuzuia kufika kule ambapo tunataka kufika. Na hivyo katika kuhakikisha tunaondokana na mambo hayo, tunapanga kutokufanya vitu fulani. Lakini kinachotokea ni kwamba, tunajikuta bado tunafanya, na hivyo kuona kama tumeshindwa kuondokana na mambo hayo yanayoturudisha nyuma. (more…)

#TAFAKARI YA LEO; VITU HIVI VIWILI VISIKUSUMBUE…

By | March 19, 2018

“There are two things a person should never be angry at, what they can help, and what they cannot.” -Plato Hongera mwanamafanikio kwa nafasi hii nyingine nzuri sana ya leo, fursa ya kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana. Kwa msingi wetu wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA (more…)

UKURASA WA 1173; Jinsi Ya Kupata Muda Wa Kufanya Kila Kitu…

By | March 18, 2018

Hakuna kitu kinawapa watu msongo wa mawazo kwa sasa kama kupata muda wa kufanya kila kitu. Kila mtu ana mambo mengi ya kufanya kuliko muda alionao. Na hivyo kwa kuwa ya kufanya ni mengi kuliko muda, kinachofuata ni msongo. Kama hiyo haitoshi, bado mambo ya kufanya yanaongezeka, wakati muda haujawahi (more…)

UKURASA WA 1172; Vitu Viwili Unavyopaswa Kufa Navyo…

By | March 17, 2018

Kuna watu wengi wanaanzia chini kabisa, wanakuwa na hamasa kubwa, wanaweka juhudi kubwa, na juhudi hizo zinazaa matunda, wanaanza kufanikiwa. Lakini haichukui muda wanaanguka. Watu hawa wanakuwa wamefanya kosa moja kubwa, wanakuwa wameshiba, wanakuwa wamezoa kile ambacho wamekuwa nacho kiasi cha kusahau walipotoka na kilichowafikisha pale walipo. Watu pia, wanapoanzia (more…)