Author Archives: Dr. Makirita Amani

About Dr. Makirita Amani

Dr. Makirita Amani ni daktari wa binadamu, mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali. Dhumuni lake kubwa kwenye maisha ni KUWASAIDA WATU KUBORESHA MAISHA YAO NA KUFIKIA MAFANIKIO MAKUBWA KUPITIA KAZI ANAZOFANYA. Mawasiliano 0717396253 email makirita@kisimachamaarifa.co.tz

UKURASA WA 1059; Njia Mbili Za Kuwahamasisha Watu Na Moja Yenye Nguvu Zaidi…

By | November 24, 2017

Tunahitaji kuwahamasisha watu kwenye maeneo mbalimbali ya maisha yetu. Kwa kuwa kila tunachohitaji kwenye maisha yetu kinatoka kwa wengine, kadiri tunavyokuwa na ushawishi mkubwa kwa wengine, ndivyo inavyokuwa rahisi kwetu kupata chochote tunachotaka. Sisi binadamu tunaongozwa na hisia kuu mbili; Moja ni tamaa ya kupata zaidi, kila mtu anapenda kupata (more…)

UKURASA WA 1057; Mkataba Hautakulinda, Uchaguzi Wa Watu Ndiyo Utakulinda…

By | November 22, 2017

Katika ushirikiano wetu na watu wengine, iwe ni kwenye kazi au biashara, tumekuwa tunapenda kuwa na mikataba ili kulinda haki na maslahi yetu. Lengo la mikataba limekuwa ni kulazimisha kila upande kutimiza wajibu wake, na kuepuka kufanya maamuzi yasiyo sahihi kwa mwingine. Watu wamekuwa wakikazana sana kupata mkataba, wakiamini mkataba (more…)

#KURASA_KUMI ZA KITABU LEO; Marcus Aurelius, Mtawala Wa Roma Na Mstoa.

By | November 21, 2017

KITABU; Meditations / Marcus Aurelius. UKURASA; 1 – 10. Marcus Aurelius, aliyekuwa mtawala wa Roma kati ya mwaka 161 mpaka kifo chake mwaka 180 anaandikwa kama mmoja wa watawala watano bora kabisa wa Utawala Wa Roma. Marcus alizaliwa katika familia ya kawaida na baada ya wazazi wake wake kufariki aliasiliwa (more…)

UKURASA WA 1056; Ni Bora Ufanye Kitu Kingine…

By | November 21, 2017

Kitu kimoja ambacho tunakihitaji sana lakini tunacho kwa ukomo hapa duniani ni muda. Kuna wakati tunahitaji tupate angalau muda wa ziada, ili kuweza kukamilisha mambo yetu lakini haupatikani. Lakini kuna wakati unakuta mtu alikuwa anapoteza muda, kwa kuwa hakuwa amejua kipi muhimu kufanya na muda wake. Leo nataka tukumbushane kitu (more…)