Category Archives: BIASHARA LEO

Mbinu za kibiashara unazoweza kutumia kukuza biashara yako na kufikia mafanikio makubwa.

BIASHARA LEO; Punguza Hatari Kwenye Biashara Yako…

By | September 9, 2018

Warren Buffett, mwekezaji mwenye mafanikio makubwa na mmoja wa watu matajiri sana duniani, anasema ana sheria kuu mbili za uwekezaji. Sheria ya kwanza ni usipoteze fedha na sheria ya pili ni usisahau sheria ya kwanza. Tunaweza pia kutumia sheria hii kwenye biashara zetu na ikatusaidia sana. Jiwekee sheria ya kutokupoteza (more…)

BIASHARA LEO; Kuuza Ni Kuwa Na Msimamo…

By | September 8, 2018

Moja ya vitu muhimu sana unavyopaswa kujua ni kwamba, kuuza ni kuwa na msimamo. Kama huna msimamo huwezi kufanikiwa kwenye mauzo. Utauza kwa kadiri utakavyokuwa na msimamo. Kwa sababu mara ya kwanza utakapowaambia watu kitu hawatachukua hatua, mara ya pili pia hawatachukua hatua, utakwenda mpaka mara ya sita, ndiyo wengi (more…)

BIASHARA LEO; Ijue Sheria Ya Kupungua Kwa Marejesho…

By | September 7, 2018

Kwenye uchumi kuna sheria inaitwa kupungua kwa marejesho, au kwa kiingereza law of diminishing return. Sheria hii inasema kwamba kuna wakati marejesho ya kitu fulani yanapungua licha ya juhudi zinazowekwa zinavyozidi kuwa kubwa. Yaani juhudi zinaongezwa, lakini matokeo yanazidi kuwa madogo. Wapo watu ambao wameanzisha biashara, zikawa zinafanya vizuri sana (more…)

BIASHARA LEO; Kazi Kubwa Iliyopo Kwenye Mwanzo Wa Biashara Yako…

By | September 6, 2018

Ni kutengeneza wateja wa biashara hiyo. Kutengeneza sifa ambayo wateja wako wanakuwa nayo kuhusu wewe. Huwezi kwenda kununua kitu kwenye biashara mara moja na ukatoka hapo ukawaambia watu ile ni sehemu nzuri. Utaenda na kupata huduma nzuri, utashawishika tena kurudi na utapata huduma nzuri, mara ya tatu ukipata tena huduma (more…)

BIASHARA LEO; Hadithi Zinauza Kuliko Kelele…

By | September 5, 2018

Kuna njia mbili za kuuza chochote unachouza. Njia hizo ni kelele na hadithi. Kwenye kelele, mtu anapaza sauti kwa njia mbalimbali ili kuwafikia wengi wajue kwamba yupo na anauza nini. Matangazo ya vyombo vya habari, matangazo kwenye mitandao ya kijamii ni moja ya aina za kelele za kutangaza na kujaribu (more…)

BIASHARA LEO; Matumizi Bora Ya Fedha Ya Matangazo Kwenye Biashara Yako…

By | September 4, 2018

Nimekutana na dhana hii ambayo nimeona ni nzuri sana kuijaribu kwenye biashara. Kama una biashara ambayo unahitaji kutangaza ili kuwafikia wengi, badala ya kutumia fedha kwenye matangazo, tumia fedha hiyo kwenye bidhaa au huduma ambazo unatoa kwa watu. Yaani ukishajua kiasi cha fedha unayopaswa kulipa kwenye matangazo ni kiasi gani, (more…)

BIASHARA LEO; Thamani Ya Ushauri Wa Bure Kwenye Biashara…

By | September 3, 2018

Ni bure, yaani hakuna. Kwa kifupi, hakuna thamani unayoipata kwenye ushauri wa bure, ambayo hukuwa unaijua tayari. Kwa sababu wengi wanaokupa ushauri wa bure kwenye biashara, wanaongelea vitu ambavyo tayari vimezoeleka, au wameona au kusikia kwa wengine. Hakuna mtu anayeweza kukupa ushauri wa bure kwenye biashara, ambao umetokana na utafiti (more…)

BIASHARA LEO; Kama Huwezi Kuuza Kitu Hiki, Ni Bora Usiwe Kwenye Biashara Kabisa…

By | September 2, 2018

Kuna watu wengi wanaingia kwenye biashara wakiwa wameshajiandaa kushindwa. Wanaingia kwenye biashara wakiwa hawana kitu cha tofauti wanachokwenda kuuza. Wanauza kile ambacho kila mtu anauza, na kwa namna ambayo kila mtu anauza. Sasa swali ni kama kile unachouza mteja anaweza kukipata sehemu nyingine yoyote, kuna umuhimu gani wa wewe kuwepo? (more…)

BIASHARA LEO; Weka Mafanikio Ya Wateja Wako Mbele Ya Faida Unayopata…

By | September 1, 2018

Somo moja ambalo kila mfanyabiashara anapaswa kulipata kila siku ni umuhimu wa kujali wateja wa biashara hiyo kwanza. Wengi wamekuwa wanaona hilo siyo sahihi, hasa kwa enzi hizi ambazo wateja siyo waaminifu. Enzi ambazo mteja anaweza kuamua kukuhama muda wowote na kwenda kununua kwa mfanyabiashara mwingine. Lakini hizi ndiyo enzi (more…)

BIASHARA LEO; Biashara Siyo Fedha, Ni Watu…

By | August 31, 2018

Watu wengi wanapofikiria kuhusu biashara, cha kwanza wanachofikiria ni fedha. Wanasema hawajaingia kwenye biashara kwa sababu hawana mtaji. Wanasema hawawezi kukuza biashara zao kwa sababu hawana fedha za kutosha. Wanasema biashara zao zinakufa kwa sababu hakuna fedha. Kufikiria biashara kwa upande wa fedha pekee ni kosa ambalo limewazuia wengi kuanzisha (more…)