Category Archives: FEDHA NA UWEKEZAJI

Soma makala kuhusu fedha na uwekezaji ili kupata maarifa sahihi ya kifedha na jinsi ya kuwekeza kwa mafanikio.

UWEKEZAJI LEO; Tofauti Ya Uwekezaji Kwenye Hisa Na Hatifungani.

By | September 20, 2017

Kwenye makala iliyopita ya UWEKEZAJI LEO, tuliona kwamba amana kuu mbili zinazopatikana kwenye soko la hisa la Dar ni hisa na hatifungani. Watu wengi wamekuwa wakisikia hisa mara kwa mara, lakini siyo hatifungani. Na hii ni kwa sababu zipo kampuni nyingi zinazouza hisa zake kuliko zinazouza hatifungani. Katika makala haya (more…)

UWEKEZAJI LEO; Aina Mbili Za Amana Zinazopatikana Kwenye Soko La Hisa La Dar Es Salaam.

By | September 19, 2017

Watu wengi wanaposikia soko la hisa, basi hufikiri kinachouzwa na kununuliwa ni hisa pekee. Lakini huu siyo ukweli. Kwenye soko la hisa kuna bidhaa mbalimbali za kifedha ambazo zinapatikana. Bidhaa hizi za kifedha kwa pamoja zinajulikana kama amana. Na hizi ndizo hupatikana kwenye masoko ya hisa na njia nyingine za (more…)

UWEKEZAJI LEO; Lijue Soko La Hisa La Dar Es Salaam (DSE).

By | September 18, 2017

Kama umekuwa unasikia kuhusu uwekezaji kwa hapa Tanzania, basi utakuwa umesikia kuhusu soko la hisa la dar es salaam kwa kiingereza Dar es salaam Stock Exchange (DSE). Huenda umekuwa unasikia na kuona hilo kwenye taarifa mbalimbali za habari. Swali ni je unaposikia soko la hisa ni mawazo gani yanakujia kwenye (more…)

Watu Waliofanikiwa Wanasema Uongo, Ndiyo Maana Wengi Wanaojifunza Kutoka Kwao, Hawafanikiwi.

By | June 9, 2017

Leo nakuletea makala hii ambayo nitahitaji uwe mtulivu sana, na uisome kwa kina ili tuweze kuelewana. Ni makala yenye hoja kinzani, hivyo ukienda nayo haraka, unaweza usinielewe, au ukaona inakwenda kinyume na kile ambacho nimekuwa nakushirikisha kila siku. Ninachotaka kukuambia ni kwamba, watu wengi waliofanikiwa ni waongo, na hii inapelekea (more…)

Hivi Ndivyo Unavyoweza Kujenga Biashara Kubwa Ya Wateja Wanaolipa Fedha Taslimu Na Siyo Mikopo.

By | June 5, 2017

Changamoto kubwa ya biashara nyingi kwenye mzunguko wa fedha ni madeni. Biashara unaanza vizuri, inakuwa na bidhaa na huduma zote, wateja wanaanza kukopa, wakiahidi kulipa wanapopata fedha zao. Lakini wateja wengi wanakuwa siyo waaminifu, wanapopata fedha hawalipi madeni, na mbaya zaidi wanahama biashara yako na kwenda sehemu nyingine. Hili limekuwa (more…)

Maajabu Ya RIBA MKUSANYIKO (COMPOUND INTEREST) Katika Kujijengea Utajiri.

By | May 18, 2017

Mwanasayansi Albert Einstein amewahi kunukuliwa akisema kwamba; riba mkusanyiko ni ajabu la nane la dunia, anayeielewa ananufaika, asiyeielewa analipa gharama. Kauli hii pekee inatosheleza kukushawishi kwa nini ni muhimu sana kujua na kutumia nguvu ya RIBA MKUSANYIKO au kama inavyofahamika kwa kiingereza COMPOUND INTEREST. Leo tutakwenda kujifunza kwa kina kuhusu (more…)

Tabia Moja Itakayokuwezesha Kudhibiti Matumizi Ya Fedha Zako.

By | May 16, 2017

Umewahi kununua kitu, halafu baadaye ukajikuta unajutia kununua kitu kile? Wakati unanunua ulijishawishi kabisa ya kwamba unakihitaji na umepata kwa unafuu, lakini baada ya kukinunua wala hujawahi kukitumia! Au umekitumia mara chache mno? Hali hii ipo sana kwenye vitu vidogo vidogo kama mavazi, pia tabia hii inawaathiri zaidi wanawake. Swali (more…)

Kubana Matumizi Siyo Mbinu Ya Kutajirika, Mbinu Hasa Ni Hii.

By | May 9, 2017

Linapokuja swala la fedha, kuna vitu vikuu viwili; Cha kwanza ni mapato, kile ambacho unapata kutoka kwenye kazi au biashara ambayo unaifanya. Kitu cha pili ni matumizi, namna ambavyo unatumia kile kipato chako. Changamoto kubwa sana kwenye fedha huwa inaanza pale matumizi yanapozidi mapato, hapo ndipo wengi hujikuta wanaingia kwenye (more…)

Angusha Na Tawala Watu Hawa Wawili Ili Uweze Kuwa Na Mafanikio Makubwa.

By | May 4, 2017

Kuna watu wawili ambao wamesimama kati yako hapo ulipo wewe na pale ambapo unataka kufika, yaani mafanikio yako kimaisha. Hii ina maana kwamba, ukiweza kuwavuka watu hao wawili, hakuna cha kukuzuia wewe kufika pale unapotaka kufika. Lakini kama ilivyo, shida kubwa ya kutatua tatizo siyo tatizo lenyewe, bali kulijua tatizo. (more…)

Jinsi Ya Kuchagua Uwekezaji Unaokufaa Wewe Kulingana Na Mahitaji Yako.

By | May 3, 2017

Kila mtu ambaye yupo makini na fedha, anataka kufikia uhuru wa kifedha na utajiri, basi uwekezaji ni kitu cha lazima kufanya. Siyo kitu cha kujaribu na wala siyo kitu cha kuangalia kama unaweza, bali ni kitu ambacho unapaswa kujifunza, kukijua kiundani na kuwekeza. Hii ni kwa sababu kadiri umri wetu (more…)