1553; Cha Kujiunguza Na Moto Huu Mkubwa Uliopo Ndani Yako…

By | April 2, 2019

Kila mmoja wetu ana kitu cha tofauti ambacho kipo ndani yake, ambacho hakuna mtu mwingine hapa duniani ambaye anacho. Kila mmoja wetu ana moto mkubwa unaowaka ndani yake, ambao akiuachilia, utatoa nuru kubwa sana kwa dunia. Lakini watu wengi wanatumia nguvu kubwa kuzima moto huo au kuuzuia usionekane, kwa sababu (more…)

#TAFAKARI YA LEO; KUWA MAKINI NA UNACHORUHUSU KIINGIE KWENYE AKILI YAKO…

By | April 2, 2019

“Drama, combat, terror, numbness, and subservience—every day these things wipe out your sacred principles, whenever your mind entertains them uncritically or lets them slip in.” —MARCUS AURELIUS, MEDITATIONS, 10.9 Hongera mwanamafanikio kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo. Ni nafasi nzuri sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza (more…)

1552; Kuwa Mbinafsi Wa Vitu Hivi Viwili Kama Unataka Kufanikiwa Zaidi…

By | April 1, 2019

Changamoto ya maisha ni hii, unapokuwa hujafanikiwa, hakuna anayehangaika na wewe, utakutana na changamoto chache sana, maisha yatakuwa yanaenda tu kawaida, hakuna migogoro mingi na wengine. Lakini unapoanza kufanikiwa, watu wanaanza kukufuatilia zaidi, na lawama nyingi zitakuja kwako kutokana na maisha ambayo mafanikio yako yatakulazimu uyaishi. Kwa mfano kadiri unavyofanikiwa (more…)

1551; Yapo Mambo Mengi Sana Ya Kufanya Hapo Ulipo…

By | March 31, 2019

Kama umewahi kukwama kwenye jambo lolote na kujiambia huna cha kufanya, umekuwa unajidanganya. Kuna mambo mengi sana ya kufanya popote unapokuwa, lakini kwanza lazima uanze kuangalia kipi cha kufanya na utaviona vingi. Kama huoni kitu cha kufanya, maana yake umekataa kuangalia ni kipi cha kufanya kwa pale ulipo. Lakini ukianza (more…)

#TAFAKARI YA LEO; WEWE NI ZAO LA MAFUNZO YAKO…

By | March 31, 2019

“Chasing what can’t be done is madness. But the base person is unable to do anything else.” —MARCUS AURELIUS, MEDITATIONS, 5.17 Hongera mwanamafanikio kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo, Ni nafasi nzuri sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana. Kwa msingi wetu wa (more…)

1550; Jinsi Unavyoweza Kutoka Kwenye Shimo…

By | March 30, 2019

Kila mmoja wetu kuna wakati ambapo anajikuta kwenye shimo fulani katika maisha yake. Shimo hilo ni pale unapokuwa umekwama, ulichotegemea hakiwezekani tena na hujui ni nini utafanya ili kutoka pale ulipokwama sasa. Kila mtu anapitia hali hii, lakini wanaofanikiwa wanaishinda na kuondoka kwenye shimo wanalokuwa wameingia. Kwa upande wa pili, (more…)

1549; Sauti Hasi Iliyopo Ndani Yetu…

By | March 29, 2019

Kila mtu ana sauti hasi ambayo ipo ndani yake. Hii ni sauti ambayo kila mara inamkumbusha madhaifu yake, makosa yake, na jinsi ambavyo hawezi kufanya makubwa kama alivyopanga. Weka mipango yoyote mikubwa na kuna kisauti ndani yako kitaanza kukusumbua, kitakuambia huwezi, kitakuonesha wengine ambao walijaribu wakashindwa. Kuna wakati kisauti hiki (more…)