UKURASA WA 1329; Kama Tayari Unajua Kila Kitu, Jua Hakuna Unachojua…

By | August 21, 2018

Kipimo kizuri cha watu ambao hawafanikiwi, watu ambao hawawezi kupiga hatua zaidi kwenye maisha yao ni ujuzi wa mambo. Watu ambao hawajafanikiwa tayari wanajua kila kitu. Waoneshe kitabu na waambie hiki ni kitabu kizuri kwako kusoma. Watakuambia labda hawana muda au hakuna jipya wanaweza kujifunza kwenye kitabu hicho. Watakuambia waziwazi (more…)

#TAFAKARI YA LEO; WAKATI MWINGINE MZURI NI SASA…

By | August 21, 2018

Hongera sana mwanamafanikio kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo. Ni nafasi bora na ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana. Kwa msingi wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa TATUA, AMUA NA ONGOZA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila (more…)

BIASHARA LEO; Moja Kwa Ajili Ya Wote…

By | August 20, 2018

Kila mfanyabiashara huwa anapenda kuwa na wateja wengi awezavyo, kwa sababu ni kupitia wateja ndiyo biashara inatengeneza faida. Hivyo ndoto ya kila mfanyabiashara ni kuwa na wateja wengi zaidi, na wengi wanapoanzisha biashara, huwa wanalenga kumuuzia kila mtu. Hivyo hutawakuta wakiweka mipango ya kuwafikia wateja wa aina fulani, wao watakuwa (more…)

UKURASA WA 1328; Usikimbie Kufanya Maamuzi…

By | August 20, 2018

Moja ya changamoto kubwa kwenye kufikia mafanikio ni kuogopa kufanya maamuzi. Watu wengi hukwepa kufanya maamuzi kwa sababu wanaogopa kukosea, au wanaona labda wakifanya maamuzi sasa watakosa vizuri zaidi vinavyokuja baadaye. Wengine hukwepa kufanya maamuzi kwa kujiona bado hawajawa tayari, hivyo kuendelea kuiandaa mpaka pale watakapojiona wamekuwa tayari. Ukweli ni (more…)

BIASHARA LEO; Usitawanye Nguvu Zako Kwa Yasiyo Muhimu…

By | August 19, 2018

Kuna watu wamekuwa wanaanzisha biashara, mwanzoni inaonekana kuwa na mafanikio makubwa, lakini haichukui muda inashindwa au hata kufa kabisa. Kinachotokea ni kwamba mtu anakuwa ameiona fursa, na anakuja na wazo la biashara ambalo linatoa suluhisho kwenye changamoto au uhitaji fulani. Basi wazo hilo linakuwa la kipekee na mafanikio yanaanza kuonekana. (more…)

UKURASA WA 1327; Lengo Ni Kupanda Ngazi Ya Juu Zaidi…

By | August 19, 2018

Wale wanaosema kwamba mafanikio au fedha hazileti furaha, kuna kitu wanakuwa hawajakielewa tangu mwanzo wa safari. Furaha kwenye maisha siyo mwisho wa safari, bali ni safari yenyewe. Usifikiri kwamba kama unaanzia chini, huna kitu basi ukishapata unachotaka utakuwa na furaha sana. Kwa sababu kwenye kupata hakuna mwisho, na hakupaswi kuwa (more…)

#TAFAKARI YA LEO; NIONESHE UNANUNUA NINI KWANZA NA NITAKUAMBIA UTAFIKA WAPI NA MAISHA YAKO….

By | August 19, 2018

“When I get a little money I buy books; and if any is left I buy food and clothes.” – Erasmus, 16th century scholar. Hii ndiyo siku bora kabisa ambayo wote tulikuwa tunaisubiria. Ni siku ya kipekee kupata kuwepo hapa duniani, kwa sababu ndiyo siku tunayoweza kuchukua hatua na kuyafanya (more…)

BIASHARA LEO; Kisichoonekana Hakifikiriwi, Kisichofikiriwa Hakionekani…

By | August 18, 2018

Kwa kiingereza wanasema out of sight out of mind. Kama hukioni kitu, huwezi kukifikiria. Na pia kinyume chake itakuwa sahihi, kama hufikirii kitu, huwezi kukiona. Sasa utajiuliza kauli hii ina matumizi gani kwenye biashara yako. Na ukweli ni kwamba, kauli hii ina kila kitu kuhusu wateja wa biashara yako. Kuna (more…)

UKURASA WA 1326; Maisha Yako Yote Ni Mabadiliko, Kuwa Tayari…

By | August 18, 2018

Watu huwa wanasema kuna siku kubwa tatu kwenye maisha ya mtu, siku ya kuzaliwa, siku ya kuoa au kuolewa na siku ya kufa. Kwa uelewa wa kawaida, hizi ndiyo siku kubwa zinazobadili kabisa maisha ya mtu yeyote yule. Lakini kwa upande wa maisha ya mafanikio, kila siku ambayo mtu anaishi, (more…)