#TAFAKARI YA LEO; HAKI YA KUZALIWA NA HAKI YA KUPATA…

By | August 18, 2018

Siku mpya, siku bora na ya kipekee sana kwetu. Ni nafasi nzuri sana kwa kila mmoja wetu kwenda kupiga hatua zaidi kwenye maisha yake, Leo, kwenda kuwa bora zaidi ya ulivyokuwa jana. Kwa msingi wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa TATUA, AMUA NA ONGOZA tunakwenda kufanya makubwa (more…)

BIASHARA LEO; Usimsahau Mteja Huyu Wa Kwanza Na Muhimu Kwa Biashara Yako…

By | August 17, 2018

Mteja wa kwanza na muhimu sana kwa biashara yako, ni mtu yeyote ambaye anafanya kazi kwenye biashara yako. Wasaidizi wako kwenye biashara, yeyote yule anayejihusisha na biashara hiyo, ni mteja wa kwanza na wa muhimu sana kwenye biashara yako. Kwa sababu hawa ni wateja ambao wanaweza kuwakaribisha wateja wakanunua zaidi (more…)

UKURASA WA 1325; Acha Kujikatisha Tamaa Wewe Mwenyewe…

By | August 17, 2018

Kuna baadhi ya vitu inabidi uone huruma kujifanyia kwenye maisha yako, kwa sababu kila mtu anakazana kukufanyia. Moja ya vitu hivyo ni kukata tamaa. Watu wengi waliokuzunguka wanajaribu kukukatisha tamaa. Sasa kama na wewe mwenyewe utajikatisha tamaa, nafasi yako ya kufanikiwa itakuwa sifuri kabisa. Unahitaji kuwa mtu pekee ambaye atasimama (more…)

BIASHARA LEO; Washauri Wako Kwenye Biashara…

By | August 16, 2018

Ni jambo la kushangaza lakini watu ambao hawajawahi kufanya biashara yoyote kwenye maisha yao wanaweza kugeuka kuwa washauri kwenye biashara yako. Wengi huamini kwa sababu wanaona biashara nyingi, basi wana mengi ya kushauri kwa biashara yoyote ile. Ni kweli kwamba kila mtu anaweza kuwa na ushauri mzuri kwenye aina yoyote (more…)

UKURASA WA 1324; Hatari Huwa Kubwa Zaidi Mwishoni…

By | August 16, 2018

Ukiona giza limekuwa nene sana jua pamekaribia kupambazuka, hii ni kauli ya waswahili inayoashiria kwamba pale mambo yanapoonekana ni magumu zaidi, ndiyo karibu na ushindi. Na huu ndiyo uhalisia wa maisha, pale mtu anapofikia mwishoni kabisa mwa jambo lolote, yaani anakaribia kupata matokeo makubwa sana, ndiyo mambo huwa yanaonekana ni (more…)

#TAFAKARI YA LEO; KUWA BORA LEO ZAIDI YA JANA…

By | August 16, 2018

Hongera sana mwanamafanikio kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo. Ni nafasi bora na ya kipekee kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana. Kwa msingi wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa TATUA, AMUA NA ONGOZA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku (more…)

BIASHARA LEO; Njia Pekee Ya Biashara Ndogo Kuishinda Biashara Kubwa…

By | August 15, 2018

Watu wengi wanapokuwa na biashara ndogo zinazoshindana na biashara kubwa huwa wanajiona kama wapo upande wa kushindwa. Huwa wanaona biashara kubwa kwa sababu ina rasilimali nyingi basi itawashinda kwa urahisi sana. Lakini ipo njia ya biashara ndogo kuishinda biashara kubwa, ambayo wala haihitaji gharama za ziada. Njia hiyo ni kutengeneza (more…)

UKURASA WA 1323; Achana Na Mbinu Na Njia Za Mkato, Fanya Kitu Sahihi Na Kifanye Kwa Usahihi…

By | August 15, 2018

Siku hizi kuna mbinu na njia za mkato kwenye kila kitu. Utasikia kuna mbinu na njia ya mkato ya kupunguza uzito, kwamba unakunywa tu kidonge na uzito unapungua. Wengine watakuambia kuna programu ya simu janja ambayo itakusaidia kufanya vitu fulani. Na kwenye fedha na mafanikio, ndiyo kabisa kila siku kuna (more…)

#TAFAKARI YA LEO; KAMA KILA MTU ANAWEZA KUFANYA, USIFANYE…

By | August 15, 2018

Siku mpya na nzuri sana kwetu. Siku ya kipekee ambapo tumepata nafasi nzuri ya kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana. Kwa msingi wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa TATUA, AMUA NA ONGOZA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu. Asubuhi (more…)