BIASHARA LEO; Hakuna Kitakachotokea Mpaka Umuuzie Mteja Kitu…

By | August 14, 2018

Uhai wa bishara yoyote unatoana na kitu kimoja, mauzo. Mauzo ndiyo njia pekee ya kuleta fedha kwenye biashara yako. Hivyo kwenye biashara yako, hakuna kitakachoweza kutokea mpaka pale mteja anapotoa fedha kununua unachouza. Hivyo nguvu zako zote unapaswa kuziweka kwenye kuhakikisha mteja anaelewa na kuwa tayari kununua. Lakini pamoja na (more…)

UKURASA WA 1322; Ukiuliza Kwa Nini Hutapata Jibu…

By | August 14, 2018

Kuna wakati watu wanafanya vitu ambavyo unashindwa kabisa kuvielewa. Unashindwa kuelewa kwa nini wamefanya kama ambavyo wamefanya, maana hukutegemea wafanye hivyo. Sasa njia mbaya kabisa ya kujua kwa nini ni kuwauliza kwa nini wamefanya walichofanya. Kwa sababu hakuna hata mmoja atakayekupa jibu sahihi kwa nini amefanya kile alichofanya, ambacho siyo (more…)

#TAFAKARI YA LEO; SIYO MUDA UNAOFANYA, BALI KIASI UNACHOFANYA…

By | August 14, 2018

Hongera sana mwanamafanikio kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo. Ni nafasi bora na ya kipekee kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana. Kwa msingi wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa TATUA, AMUA NA ONGOZA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku (more…)

BIASHARA LEO; Usivunje Mioyo Ya Wateja Wako…

By | August 13, 2018

Tabia ya binadamu ni moja, tunapenda kuamini vitu na kisha kuvizoea. Kadiri vitu vinakwenda kama tulivyozoea viende, maisha yetu ni mazuri. Lakini vitu vinapokwenda tofauti na tulivyozoea, wakati tumeshaweka matumaini yetu kwenye vitu hivyo, hapo ndipo mgogoro unapoanzia. Hivi ndivyo unavyopaswa kwenda na wateja wako kwenye biashara yako. Wafanye wateja (more…)

UKURASA WA 1321; Chukua Dakika Chache Kufanya Zoezi Hili La Kukuamsha…

By | August 13, 2018

Mwanafalsafa Socrates alinukuliwa kusema maisha ambayo hayapimwi wala kuhojiwa hayana maana ya kuishi. Haijalishi tuna misingi mizuri kiasi gani tunayoishi kwenye maisha yetu, mara kwa mara tutajikuta tunaanguka. Tunajikuta tunafanya vitu vinavyoenda kinyume na misingi yetu. Siyo rahisi kuona vitu hivyo kama mtu utakuwa unafanya kwa mazoea. Kama mtu utakuwa (more…)

BIASHARA LEO; Ushindani Utaondoa Faida Yote Na Kukuacha Huna Kitu…

By | August 12, 2018

Upo usemi maarufu kuhusu biashara kwamba biashara ni ushindani. Sasa kama utaubeba usemi huo na kuingia kwenye biashara kwa kuamini kwamba unaweza kushindana, unaweza ukashinda, lakini utabaki na ushindi usio na maana. Ushindi pekee unaohitaji kwenye biashara ni faida. Na faida ni pale gharama zako zote mpaka mteja anapata anachotaka, (more…)

UKURASA WA 1320; Njia Pekee Ya Wewe Kupata Ukuu Kwenye Maisha Yako…

By | August 12, 2018

Karibu kila dini na falsafa ina mafundisho yanayotukumbusha kwamba tulikuja duniani tukiwa watupu na tutaondoka tukiwa watupu. Chochote tunachotafuta na hata tukijiambia tunamiliki hapa duniani, hatutaondoka nacho. Watu wanapata mali na wanazipoteza, watu wanakuwa na fedha nyingi na zinapotea. Na kwenye falsafa ya ustoa hatusemi umepoteza, bali umerudisha. Kwa sababu (more…)

#TAFAKARI YA LEO; KUIBADILI DUNIA NA KUJIBADILI MWENYEWE…

By | August 12, 2018

“Everyone thinks of changing the world, but no one thinks of changing himself.” — Leo Tolstoy Siku mpya, Siku bora na ya kipekee sana kwetu. Ni nafasi nyingine nzuri sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana. Kwa msingi wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na (more…)

BIASHARA LEO; Kitu Kimoja Kinachoweza Kuteketeza Biashara Yako Kabisa…

By | August 11, 2018

Watu wamekuwa wanatoa sababu mbalimbali kwa nini biashara zao zimeshindwa. Na unapowasikiliza, utawasikia wakisema mambo ya nje tu. Kwamba uchumi mgumu, kwamba watu hawana fedha, kwamba ushindani umekuwa mkali na mengine kama hayo. Hutawasikia wakisema mambo ya ndani, ambayo ndiyo sababu kuu ya kufa kwa biashara. Mambo kama uzembe, uvivu, (more…)