UKURASA WA 1240; Tumaini, Hofu Na Ndoto…

By | May 24, 2018

Hivi ni vitu vitatu vyenye nguvu kubwa ya kufanya maisha yako yawe ya mafanikio au ya kushindwa. Tumaini ni nguvu inayokusukuma kupiga hatua zaidi, hata kama huoni kile unachokwenda kupata na wala huna uhakika nacho. Tumaini linakufanya uamini usichokiona na uwe na uhakika wa kukipata, hata kama hujawahi kukipata huko (more…)

#TAFAKARI YA LEO; ULIZALIWA HURU, KWA NINI UNAJIFUNGA?

By | May 24, 2018

“Man was born free, and he is everywhere in chains.” -Jean-Jacques Rousseau Mwanamafanikio, hii ni siku mpya, siku nzuri na ya kipekee kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana. Ni nafasi ya kipekee kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana. Kwa msingi (more…)

UKURASA WA 1239; Fanya Kwa Kujali Zaidi…

By | May 23, 2018

Siku ya kwanza kwa mtu kufanya chochote kile, huwa anaifanya kwa kujali sana, anaweka juhudi kubwa katika kufanya na hiyo inamletea matokeo bora sana. Lakini sasa yanakuja mazoea, baada ya muda mtu anazoea kile anachofanya, anazoea matokeo ambayo amekuwa anapata na anaanza kupata matokeo ambayo siyo makubwa tena. Kwa matokeo (more…)

UKURASA WA 1238; Wote Ni Wale Wale…

By | May 22, 2018

Kosa kubwa ambalo watu wengi wamekuwa wanafanya, ambalo linawazuia kufanikiwa kwenye chochote wanachofanya, ni kujumuisha mambo au watu. Kwa sababu mtu mmoja amesumbua au amekuangusha basi unachukulia watu wote waliopo kundi moja na mtu huyo hawafai. Kwa sababu umejaribu kitu kimoja ukashindwa, basi unachukulia vitu vingine vyote navyo vitashindikana tu. (more…)

UKURASA WA 1237; Hatari Ya Unachojua Na Usichojua…

By | May 21, 2018

Tumekuwa tunafikiri kwamba kinachotuzuia kufanikiwa na vile vitu ambavyo hatuvijui, hivyo kama tutajua vitu hivyo, kikwazo cha mafanikio kitaondoka. Ni kweli tusichojua ni kikwazo kwetu kufanikiwa, lakini pia tunachojua kinaweza kuwa kikwazo kikubwa zaidi. Na kwa wengi, kinachowazuia kufanikiwa siyo wasichojua, bali kile ambacho tayari wanajua. Unakuta kile ambacho mtu (more…)

UKURASA WA 1236; Kelele Za Dunia…

By | May 20, 2018

Tunaishi kipindi cha kipekee, kipindi bora kabisa kuwahi kutokea duniani. Kipindi ambacho, mtu anaweza kujifunza chochote, bila ya kuwa na kitu au mtu wa kumzuia. Maarifa na taarifa ni nyingi na zinapatikana kwa urahisi, kwa yeyote anayezitaka. Lakini pamoja na wingi huu wa taarifa na urahisi wa kupatikana kwake, ni (more…)