UKURASA WA 1247; Uhuru, Utu Na Utajiri…

By | May 31, 2018

Hivi ni vitu vitatu ambavyo kila mtu anavipigania, vitu vitatu ambavyo vinayafanya maisha ya yeyote kuwa bora sana. Kila mtu anapenda kuwa huru, kufanya maamuzi yake, kuendesha maisha yake, kufanya kile ambacho ni muhimu kwake. Lakini uhuru hauji bure, uhuru unahitaji kufanyiwa kazi na pia unakuja na majukumu. Wakati mwingine (more…)

#TAFAKARI YA LEO; USITEGEMEE CHOCHOTE, ILA WEKA JUHUDI…

By | May 31, 2018

“Expect nothing, and you will enjoy everything!” Hongera mwanamafanikio kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo. Ni nafasi bora na ya kipekee kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana. Kwa msingi wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa TATUA, AMUA NA ONGOZA tunakwenda (more…)

UKURASA WA 1246; Ukuaji Wowote Unahitaji Muda…

By | May 30, 2018

Kwa asili, ukuaji wowote unahitaji muda, tena muda wa kutosha na haraka haijawahi kusaidia. Tukianza na sisi wenyewe binadamu, mimba inatungwa, inakaa tumboni kwa miezi tisa, baada ya hapo anazaliwa mtoto, ambaye hawezi kujilisha wala hata kusema anataka kujisaidia, inamchukua miaka mitano kuweza kupata ufahamu wa kawaida wa kufanya mambo (more…)

UKURASA WA 1245; Hamasa Ya Kazi Inapoishia…

By | May 29, 2018

Siku ya kwanza ya kitu chochote, ni siku ambayo watu huwa wanakuwa na hamasa kubwa sana. Si unaikumbuka siku ya kwanza kwenda shule, huenda hukulala, ulisubiri kwa hamu kuamka na kwenda shule. Kadhalika siku ya kwanza kusafiri kwenda mahali ambapo hujawahi kwenda. Kumbuka pia siku yako ya kwanza ya biashara, (more…)

UKURASA WA 1244; Jinsi Ya Kuongea…

By | May 28, 2018

Nilishakushirikisha jinsi ya kusikiliza, leo nakwenda kukushirikisha jinsi ya kuongea. Unaweza kushangaa kwamba kuongea nako inapaswa kujifunza? Si unatoa tu maneno uliyonayo? Ni sababu hiyo ndiyo inapelekea wengi kuingia kwenye matatizo, kuongea kwa sababu tu wanaweza kuongea. Sasa tujifunze jinsi ya kuongea. Ongea kwa sababu una kitu MUHIMU cha kuongea, (more…)

UKURASA WA 1243; Ujumbe Uliopo Ndani Ya Kushindwa…

By | May 27, 2018

Huwezi kufanikiwa kwenye maisha bila ya kupitia kushindwa. Na tunaweza kusema kinachowatofautisha wanaofanikiwa na wasiofanikiwa ni kushindwa. Kila anayejaribu kufanya chochote kwenye maisha, lazima akutane na kushindwa. Kinachowatofautisha wanaofanikiwa na wasiofanikiwa ni kinachotokea baada ya kushindwa. Wasiofanikiwa, huacha baada ya kushindwa, huchukulia kushindwa kama kikwazo kikuu cha kufikia ndoto zao, (more…)

UKURASA WA 1242; Kama Watu Wanapata Wanachotegemea Kupata, Hufanyi Makubwa…

By | May 26, 2018

Mafanikio yako ni matokeo ya thamani unayoongeza kwa wengine. Kadiri unavyoongeza thamani kubwa ndivyo unavyojitengenezea mafanikio makubwa zaidi. Sasa changamoto ni moja, mara nyingi watu huwa hawajui wanataka nini mpaka pale wanapokipata. Kwa mfano kabla hatujawa na simu janja (smartphone) watu hawakuwahi kusema kwamba wanahitaji aina hizi za simu. Lakini (more…)

UKURASA WA 1241; Njia Kuu Ya Kuiokoa Biashara Iliyopo Kwenye Changamoto Na Inayokaribia Kufa.

By | May 25, 2018

Kila biashara huwa inapitia changamoto mbalimbali. Baadhi ya changamoto zinaifanya biashara kuwa imara zaidi kwa sababu mfanyabiashara anajifunza na kuweza kupiga hatua zaidi. Lakini baadhi ya changamoto huwa zinakuwa kikwazo kikubwa kwenye biashara na kuiweka biashara kwenye hatari ya kufa kabisa. Hizi ndiyo changamoto ambazo wafanyabiashara wengi huwa wanaziogopa kwa (more…)