UKURASA WA 1194; Maisha Ni Kuliona Kusudi…

By | April 8, 2018

Kusudi la maisha, ni kile kitu ambacho mtu umeletwa kufanya hapa duniani. Ni kile pekee ambacho kinatofautisha maisha yako na ya wengine. Kila mtu ana kusudi lake, na hakuna makusudi yanayofanana kwa kila kitu. Maono ni pale akili inachoona kisichokuwepo na kuwa na imani kwamba kitakuwepo. Maono ni kitu ambacho (more…)

UKURASA WA 1193; Kufanya Kitu Kimoja, Kufanya Mara Moja…

By | April 7, 2018

Dunia imekuwa inawahadaa wengi kwamba kipo kitu kimoja ambacho wakikijua na kukifanya basi maisha yao yatakuwa bora, mafanikio kwao itakuwa uhakika. Watu wamekuwa wakidanganyika kwamba kuna kitu wakikifanya mara moja tu basi maisha yao yanabadilika kabisa. Kwa imani hiyo, watu wamekuwa wanatumia muda mwingi kutafuta kitu hicho ambacho kama wakifanya (more…)

UKURASA WA 1192; Ukweli Upo Hapo Ulipo, Usiende Mbali Kuutafuta, Fungua Macho Kuuona…

By | April 6, 2018

Moja ya mahangaiko ambayo sisi binadamu tumekuwa tunafanya, ni kwenda mbali kutafuta kitu ambacho tayari kipo pale tulipo. Halafu pamoja na kwenda mbali hatupati tunachotafuta, mwishowe tunaona maisha ni magumu na kukata tamaa. Angalia mifano mingi na utajionea mwenyewe. Mtu anaondoka kwenye kazi moja na kwenda kwenye kazi nyingine akiamini (more…)

#TAFAKARI YA LEO; MAFANIKIO KIDOGO NI SUMU YA MAFANIKIO MAKUBWA.

By | April 5, 2018

We become wiser by adversity; prosperity destroys our appreciation of the right. – Lucius Annaeus Seneca Hongera mwanamafanikio kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo. Ni nafasi bora na ya kipekee kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa kwa msingi wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA na mwongozo wa TATUA, AMUA NA (more…)

UKURASA WA 1191; Mambo Mabaya Hutokea Hata Kwa Watu Wazuri…

By | April 5, 2018

Sehemu ambapo akili zetu sisi binadamu zinashindwa kuelewa, ni pale tunapofanya kila tunachopaswa kufanya, lakini tunapata matokeo tofauti na tuliyotegemea kupata. Tunaamini kama tunaweka juhudi fulani, basi tunapaswa kupata matokeo yanayoendana na juhudi hizo. Na pale matokeo tunayopata yanapokuwa tofauti, tunaona kama tumedhulumiwa au tumedanganywa. Lakini ukweli ni kwamba, mambo (more…)

UKURASA WA 1190; Uwezo Wa Aina Mbili Wa Kukuvusha Nyakati Ngumu Kiuchumi…

By | April 4, 2018

Kadiri siku zinavyokwenda, ndivyo uchumi unavyozidi kuwa mgumu duniani kote. Hii ni kwa sababu maendeleo ya sayansi na teknolojia yanakuja na vifaa ambavyo vinarahisisha sana kazi na hivyo watu wachache zaidi kuhitajika kwenye kazi yoyote ile. Kwa mfano kompyuta moja inaweza kuchukua kazi za watu watano, ikaendeshwa na mtu mmoja (more…)

UKURASA WA 1189; Kazi Kubwa Unayopaswa Kufanya Ambayo Unaikwepa…

By | April 3, 2018

Mabadiliko yoyote kwenye maisha siyo rahisi, hata kama mabadiliko hayo hayagharimu fedha. Yanakuwa mabadiliko magumu kwa sababu kwa sehemu kubwa, yanatutaka tubadili kabisa ile imani ambayo tumeshajijengea kwenye maisha yetu. Ipo hivi rafiki, kuna vitu vingi ambavyo unaamini ndiyo ukweli na ndivyo maisha yanavyopaswa kuwa, lakini siyo imani sahihi. Sasa (more…)

#TAFAKARI YA LEO; UJINGA NI KUTEGEMEA MABAYA YATOKEE…

By | April 3, 2018

Nothing is so wretched or foolish as to anticipate misfortunes. What madness is it to be expecting evil before it comes. – Lucius Annaeus Seneca Hongera mwanamafanikio kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo. Ni nafasi bora na ya kipekee kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo (more…)

UKURASA WA 1188; Hebu Tuone Nini Kitatokea…

By | April 2, 2018

Katika safari ya mafanikio, sehemu kubwa ya hatua utakazochukua ni zile ambazo huna uhakika nazo kwa asilimia mia moja. Unajua kabisa kuna kitu unapaswa kufanya, lakini huna uhakika matokeo yatakuwaje. Hapo ndipo wale wanaoishia kuwa kawaida wanakwama, wakati wale wanaofanikiwa wanafanya licha ya kutokuwa na uhakika. Kinachowasukuma ni kauli kwamba (more…)