UKURASA WA 1187; Kiwango Sahihi Cha Kuchukua Hatua…

By | April 1, 2018

Mafanikio yako kwenye maisha yanaendana na kiwango chako cha kuchukua hatua, kwenye kila eneo la maisha yako. Na inapokuja kuhusu kuchukua hatua, kuna viwango vitatu; Cha kwanza ni kutokuchukua hatua kabisa, yaani mtu yupo yupo tu, hafanyi chochote mpaka pale inapombidi kweli afanye. Kama ni kazi basi ana kila sababu (more…)

#TAFAKARI YA LEO; KUPATA MAFANIKIO YA KUDUMU, BADILIKA.

By | April 1, 2018

“Whosoever desires constant success must change his conduct with the times.” -Niccolo Machiavelli Hongera mwanamafanikio kwa siku hii nyingine nzuri sana kwetu, Ni nafasi bora na ya kipekee kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana. Msingi wetu wa mafanikio, NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo (more…)

UKURASA WA 1186; Vitu Vya Kawaida Kwa Watu Wa Kawaida…

By | March 31, 2018

Uchumi wa mapinduzi ya viwanda ulijengwa kwenye msingi wa viwanda kutengeneza vitu vya kawaida kwa watu wa kawaida. Ni rahisi kufanya hivyo, na ina faida zaidi. Lakini changamoto kubwa ni moja, ni vigumu kujitofautisha na wengine, ambao nao wanatengeneza vitu vya kawaida kwa watu wa kawaida. Uchumi wa mapinduzi ya (more…)

UKURASA WA 1185; Kuumizwa Ni Kuchagua….

By | March 30, 2018

Watu huwa wanalalamika kuumizwa na watu au vitu wanavyopitia kwenye maisha yao. Lakini katika kila hali ambayo watu wanalalamikia inawaumiza, wapo wengine ambao wanaendelea na maisha yao vizuri bila ya kulalamika kuumizwa. Iwe ni kwenye mahusiano, kazi na hata biashara, kuumizwa ni kuchagua. Pale unapochagua kuangalia kile kinachokutokea kama ni (more…)

UKURASA WA 1184; Kikwazo Kikubwa Cha Kupiga Hatua Na Kufanikiwa…

By | March 29, 2018

Huwa tunawalalamikia wale wanaotuzunguka, tukiona kama wao ndiyo kikwazo cha sisi kushindwa kufanikiwa kwenye yale tunayotaka. Labda ni watu wanaopaswa kutupa vitu fulani na hawatupi, au ni watu ambao wanatutegemea zaidi kuliko uwezo wetu. Wakati mwingine tunaona mazingira tuliyopo ni kikwazo cha sisi kupiga hatua, pale mazingira yanaoonekana kukosa yale (more…)

#TAFAKARI YA LEO; KILA TATIZO UNALOTATUA NI SHERIA…

By | March 29, 2018

“Each problem that I solved became a rule, which served afterwards to solve other problems.” -Rene Descartes Hongera mwanamafanikio kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo. Ni nafasi bora na ya kipekee kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana. Msingi wetu wa maisha ya mafanikio (more…)

UKURASA WA 1183; Kanuni Ya Ukuu, Iliyo Rahisi Kuelewa Na Kuishi…

By | March 28, 2018

Watu wanapenda ukuu kwenye maisha, kwenye kazi zao, kwenye taaluma zao, kwenye biashara zao na mengine wanayofanya. Lakini ni wachache ambao wamekuwa wakifikia ukuu kwenye yale wanayofanya. Na kadiri siku zinavyokwenda, kwa zama hizi tunazoishi, ndivyo wachache wanaweza kufikia ukuu. Hii ni kwa sababu, mambo ambayo watu wanafanya, yanapingana kabisa (more…)

UKURASA WA 1182; Fedha Hazina Hisia, Sisi Tunazipa Hisia…

By | March 27, 2018

Fedha ni fedha, ni kipande cha karatasi, au chuma, au tarakimu kwenye kompyuta ambayo imepewa thamani na wote tukakubaliana nayo. Nje ya hapo, fedha haina hisia yoyote ile. Lakini sasa, mtu akiokota, kupewa au kushinda zawadi ya fedha, ataitumia hovyo kuliko fedha ambayo ameitafuta kwa nguvu na jasho! Mtu akiwa (more…)