#TAFAKARI YA LEO; KITU HUNG’ARISHWA KWA KUSUGULIWA….

By | January 6, 2018

A gem cannot be polished without friction, nor a man perfected without trials. – Lucius Annaeus Seneca Hongera mwanamafanikio kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo. Leo tumepata nafasi nyingine nzuri kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana. Msingi wetu wa maisha ya mafanikio ni (more…)

UKURASA WA 1101; Uhuru, Uvumilivu Na Nguvu Ni Zao La Kitu Hichi Kimoja…

By | January 5, 2018

Watu wamekuwa wakisema fedha au utajiri siyo mzuri, kwa sababu wakiwaangalia baadhi ya watu wenye fedha na utajiri, wamekuwa watumwa kwa fedha na utajiri wao. Mtu anakuwa na fedha na mali nyingi, lakini bado haridhiki, anaona kuna kitu anakosa, anazidi kutaka zaidi na zaidi. Hiyo hali ya kutaka zaidi na (more…)

UKURASA WA 1100; Mtu Pekee Wa Kumwonea Aibu Ni Huyu…

By | January 4, 2018

Moja ya vitu vinavyowasukuma wengi kudanganya au kutafuta njia zisizo sahihi za kufanya mambo, ni kuwaonea wengine aibu. Kuona kama wengine wakijua ukweli ulivyo, basi watawadharau na kuona hawafai. Hivyo watu wanadanganya, au kuigiza mambo ili wengine wasiwachukulie kwa namna ya tofauti. Kwa kudanganya huko au kuigiza, watu kwa nje (more…)

#TAFAKARI YA LEO; SIYO UGUMU WA VITU, NI UGUMU WETU WENYEWE…

By | January 3, 2018

It’s not because things are difficult that we dare not venture. It’s because we dare not venture that they are difficult. – Lucius Annaeus Seneca Habari za asubuhi ya leo mwanamafanikio? Hongera kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo. Ni nafasi bora na ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka (more…)

UKURASA WA 1099; Tofauti Ya Wabobezi Na Wachanga Kwenye Fani Mbalimbali…

By | January 3, 2018

Katika kila aina ya fani, kuna makundi mawili ya watu. Kuna watu ambao wamebobea kwenye fani hiyo, hawa ni wale ambao wameshajijengea majina kwenye kile wanachofanya. Hawa ni watu ambao watu wanawatafuta wanapokuwa na shida na wanatoa thamani kubwa. Pia kuna ambao ni wachanga, hawa ni watu ambao wanaingia kwenye (more…)

UKURASA WA 1098; Kujionesha Na Kuonekana, Namna Unavyopoteza Nguvu Zako Mwenyewe.

By | January 2, 2018

Ni hitaji la ndani la kila binadamu kupenda kuthaminiwa, kuonekana ni wa muhimu kwa chochote kile ambacho anakifanya. Huu ni msukumo uliopo nyuma ya maamuzi ambayo wengi wanafanya, kuanzia mavazi wanayovaa, kazi na biashara wanazofanya, mali wanazomiliki na hata michango wanayotoa kwa wengine. Hakuna ubaya wowote kwenye hilo, ila pale (more…)

UKURASA WA 1097; Miaka Mitatu Ya Kurasa Na Nguvu Ya Kufanyia Kazi Wazo…

By | January 1, 2018

Siku kama ya leo, miaka mitatu iliyopita, nilipata wazo hili la kuandika makala fupi kila siku, na kuzipa jina la KURASA ZA MAISHA YA MAFANIKIO. Kabla ya makala hizi za kurasa, nilikuwa tayari nimejenga utaratibu wa kujiandikia kila siku, lakini zilikuwa makala ambazo ni kwa ajili ya mada maalumu. Labda (more…)