UKURASA WA 1064; Kama Unataka Kutengeneza Mabadiliko Ya Kudumu, Tengeneza Kwanza Utamaduni…

By | November 29, 2017

Tunapenda kupiga hatua kwenye maisha, tunapenda kufanikiwa, lakini kinachotukwamisha mara nyingi ni njia tunazotumia kupiga hatua na kufikia yale mafanikio tunayotaka. Kwa mfano, kuendelea kufanya kile ambacho mtu anafanya, kwa njia ambayo anafanya kutaendelea kuzalisha matokeo ambayo amekuwa anapata. Haihitaji shahada kujua kwamba kama utaendelea kufanya kazi unayofanya, kwa namna (more…)

UKURASA WA 1063; Siku Moja Si Kitu, Lakini Miaka Kumi Ina Kitu Kikubwa….

By | November 28, 2017

Mtu mmoja amewahi kusema kwamba tabia ni kama uzi mwembamba, ambao unajisokotea kidogo kidogo kila siku. Ni rahisi kukata uzi huo unapokuwa umejisokotea kidogo, lakini kadiri unavyozidi kusokota, ndivyo inavyokuwa vigumu kuukata. Katika kujenga tabia na hata kwenye hatua tunazopiga au kuacha kupiga, siku moja inaweza kuonekana kama siyo kitu. (more…)

UKURASA WA 1062; Jina Lako Limejengwa Juu Ya Nini?

By | November 27, 2017

Kuna jina ambalo ulipewa na wazazi au walezi wako, hili lilikuwa jukumu lao kwako ulipokuwa mdogo na hukuweza kujichagulia jina mwenyewe. Pia wapo ambao wamejipa au kubadili majina yao kwa sababu mbalimbali. Yote hayo ni majina ya kutumia kama utambulisho kwa wengine. Lakini pia kuna jina jingine muhimu, hili ni (more…)

UKURASA WA 1061; Ukiacha Kuangalia Ndoto Zako, Utaona Hichi Kitakachokutisha…

By | November 26, 2017

Nimewahi kusoma ujumbe mmoja wa kufundisha katika jumbe ambazo huwa zinasambazwa kwa njia ya simu. Katika ujumbe huu, muumini wa kanisa alikwenda kwa mchungaji na kumwambia hataki tena kuhudhuria ibada kwa sababu kila anapokuwa kwenye ibada anaona watu wakifanya mambo yasiyofaa. Wengi wanakuwa wanachezea simu zao, wengine wanapiga umbeya na (more…)