#UKURASA WA 1028; Kataa Kutumiwa Na Wengine, Anza Kujitumia Mwenyewe…

By | October 24, 2017

Sitaki kuwa hasi lakini ukweli lazima ukae wazi, ya kwamba kama unatumiwa na wengine, huwezi kufanikiwa. Unaweza tu kusahau kuhusu mafanikio kama umekabidhi maisha yako kwa wengine na kuwapa wao majukumu ya kufanya kile wanachotaka kufanya na muda wako, nguvu zako, utaalamu wako na hata uzoefu wako. Hatua ya kwanza (more…)

#UKURASA WA 1027; Matokeo Na Mchakato, Wakati Sahihi Kwa Kila Kimoja…

By | October 23, 2017

Dunia inapenda matokeo, ila haipendi mchakato. Watu wanafurahia na kuhamasika pale wanapoona mtu kapata matokeo fulani mazuri na makubwa. Lakini hawapendi kuona mchakato mzima uliozalisha matokeo yale, na hata wakiambiwa mchakato huo, wanaweza wasikubaliane nao. Tunapoishi maisha yetu, tunapanga michakato ambayo inatufikisha kwenye mafanikio. Watu wengi huzama kwenye mchakato, kwenye (more…)

Ukurasa Wa 1026; Kaa Kwenye Kile Unachofanya Hata Kinapokuwa Kigumu.

By | October 22, 2017

Kaa Kwenye Kile Unachofanya Hata Kinapokuwa Kigumu… Kila kitu unachopanga kufanya kwenye maisha yako, kuna wakati kinakuwa kigumu. Iwe ni kazi, biashara na hata maisha ya kawaida. Upo wakati utafikia ugumu na akili kuona haiwezi kwenda tena. Huu ndiyo wakati ambapo wengi huwa wanatoroka, wanaacha kufanya kile walichokuwa wanafanya na (more…)

#KURASA_KUMI ZA KITABU LEO; Mwamshe Socrate Aliyepo Ndani Yako.

By | October 21, 2017

KITABU; Socrates’ way : seven master keys to using your mind to the utmost / Ronald Gross. UKURASA; 171 – 180. Mpaka sasa umejifunza mambo mengi sana kuhusu mwanafalsafa Socrates. Katika mengi uliyojifunza, yapo ambayo yanakuwa yamekuvutia na ambayo unaona yanaendana na wewe. Mambo haya ndiyo yanaakisi Socrates ambaye yupo (more…)

UKURASA WA 1025; Chagua Eneo Moja Au Machache Na Zama Ndani….

By | October 21, 2017

Moja ya changamoto za zama tunazoishi sasa, ni wingi wa fursa, wingi wa vitu vya kufanya na wingi wa mambo yanayotuvutia, yanayotushawishi kwamba ni mazuri zaidi kwetu. Na hili limekuwa linatuzuia kufanikiwa kwa sababu watu wamekuwa wanatumia muda mwingi kujaribu mambo mapya na yanayoonekana ni mazuri, kuliko muda wanaotumia kwenye (more…)

#KURASA_KUMI ZA KITABU LEO; Tengeneza Sanaa Ya Maisha Yako.

By | October 20, 2017

KITABU; Socrates’ way : seven master keys to using your mind to the utmost / Ronald Gross. UKURASA; 161 – 170. Kama ilivyokuwa kwa Socrates, kila mmoja wetu ana kitu ndani yake, ambacho kinaweza kuinufaisha dunia. Kitu hichi kinatoka ndani yake na kwakukifanya mtu anapata furaha na kuridhika sana. Na (more…)