UKURASA WA 1005; Usishushe Viwango Vyako…

By | October 1, 2017

Tunapoanza kufanya kitu chochote, iwe ni kazi, biashara na hata maisha ya kawaida, huwa kuna viwango ambavyo tunajiwekea. Huwa tuna picha ya namna tutakavyokuwa tunafanya, huwa tuna malengo na mipango mikubwa ya kile tunachofanya. Lakini tunapoanza kufanya, tunakutana na dunia, tunakutana na wale ambao wanafanya kile tunachofanya. Na tunagundua, wengi (more…)

#KURASA_KUMI ZA KITABU LEO; Falsafa Ya Maisha mazuri na yenye furaha.

By | September 30, 2017

KITABU; Philosophy for life and other dangerous situations : ancient philosophy for modern problems / Jules Evans Kurasa; 197 – 206.. Kumekuwa na jitihada mbalimbali za kuchagua falsafa moja ambayo inaweza kuleta maisha mazuri na ya furaha kwa kila mtu. Lakini kila falsafa imekuwa inawafaa watu fulani na wengine kuikataa, (more…)

UKURASA WA 1004; Unapojishikiza Kwenye Vitu, Unapoteza Uhuru Wako…

By | September 30, 2017

Maisha yetu wanadamu kuna wakati yanakuwa ya ajabu sana. Mtu unakazana kutafuta na kupata vitu, halafu ukishavipata vinakuwa matatizo kwako. Umewahi kukutana na mtu ambaye maisha yake yalikuwa mazuri kabla hajapata fedha au utajiri, lakini baada ya kupata vitu hivyo maisha yanakuwa magumu? Wengi wamekuwa wakisema kabisa kwamba ni bora (more…)

#KURASA_KUMI ZA KITABU LEO; Kila mtu anahitaji mashujaa wake…

By | September 29, 2017

KITABU; PHILOSOPHY FOR LIFE AND OTHER DANGEROUS SITUATIONS : ANCIENT PHILOSOPHY FOR MODERN PROBLEMS / JULES EVANS UKURASA; 187 – 196… Sisi binadamu ni viumbe wa kijamii, huwa tunapenda kukubalika ndani ya jamii tunayoishi. Na ili kuweza kukubalika, huwa tunaishi maisha ya kuiga. Mambo mengi ambayo tunafanya, ni kwa sababu (more…)

BIASHARA LEO; Ushauri Bora Kabisa Wa Biashara Yako Upo Kwenye Tabia Za Wateja Wako…

By | September 29, 2017

Unapokuwa na wateja ambao wanalalamikia mambo mengi kwenye biashara yako, ni vyema ukajihakikishia kwamba ni wateja sahihi kabla hujachukua hatua. Kwa sababu wapo watu ambao wamepewa ushauri wa namna ya kuboresha biashara zao na watu ambao siyo wateja wa biashara hizi. Yaani mtu anakuja na kukuambia ungefanya hivi ungepeta wateja (more…)

UKURASA WA 1003; Njia Bora Ya Kuwakasirisha Wanaokukasirisha…

By | September 29, 2017

Changamoto kubwa za maisha yetu zinaanzia kwa wale wanaotuzunguka. Msongo wa mawazo, hasira, chuki, wivu na hisia nyingine za aina hiyo, zinatoka kwa wale wanaotuzunguka. Kadhalika pia hisia nzuri za furaha, matumaini, upendo tunazipata kutoka kwa wengine. Wapo watu ambao wanafanya mambo fulani kwa makusudi, ili wewe ukasirikie. Wengine wanafanya (more…)

#KURASA_KUMI; Matatizo ya dunia yataisha iwapo itatawaliwa na wanafalsafa.

By | September 28, 2017

KITABU; Philosophy for life and other dangerous situations : ancient philosophy for modern problems / Jules Evans UKurasa; 177 – 186.. Mwanafalsafa Plato, kupotia kitabu chake cha The Republic, aliandika kwamba dunia itatulia na kuwa sehemu salama, iwapo wanafalsafa wataitawala dunia. Aliamini changamoto ambazo dunia inipitia, zinaweza kutatuliwa na wanafalsafa (more…)