UWEKEZAJI LEO; Tofauti Ya Uwekezaji Kwenye Hisa Na Hatifungani.

By | September 20, 2017

Kwenye makala iliyopita ya UWEKEZAJI LEO, tuliona kwamba amana kuu mbili zinazopatikana kwenye soko la hisa la Dar ni hisa na hatifungani. Watu wengi wamekuwa wakisikia hisa mara kwa mara, lakini siyo hatifungani. Na hii ni kwa sababu zipo kampuni nyingi zinazouza hisa zake kuliko zinazouza hatifungani. Katika makala haya (more…)

BIASHARA LEO; Bidhaa Bora Haihitaji Punguzo La Bei…

By | September 20, 2017

Moja ya mjadala mkubwa kwenye biashara, hasa biashara ndogo ni iwapo mtu unaweza kuvutia wateja zaidi kwa kuweka punguzo la bei, au kuuza bei rahisi kuliko wengine. Na mara nyingi majibu ni ndiyo ndani ya muda mfupi, utavutia wateja ndani ya muda mfupi, lakini iwapo na wengine nao watapunguza bei, (more…)

#KURASA_KUMI; Tatizo La Dhana Ya Maisha Ya Furaha.

By | September 20, 2017

KITABU; Philosophy for life and other dangerous situations : ancient philosophy for modern problems / Jules Evans UKurasa 94 – 103. Falsafa ya Epicurean inaweka msisitizo wa kuishi maisha ya raha muda wote na kuepuka aina yoyote ya maumivu. Kitu ambacho kwa haraka kinaweza kuonekana ni kizuri, kwa sababu nani (more…)

UKURASA WA 994; Siyo Mwanzo Na Wala Siyo Mwisho…

By | September 20, 2017

Maisha yetu ni mwendelezo wa mambo ambayo hayana mwanzo wala mwisho. Maisha yetu yana mwanzo pale tunapozaliwa na yana mwisho pale tunapokufa. Lakini hapo katikati, mambo tunayokutana nayo kwenye maisha yetu, hayana mwanzo wala mwisho. Nakushirikisha hili rafiki kwa sababu watu tumekuwa tukijidanganya kwamba kama tukiweza tu kutoka pale tulipo (more…)

UWEKEZAJI LEO; Aina Mbili Za Amana Zinazopatikana Kwenye Soko La Hisa La Dar Es Salaam.

By | September 19, 2017

Watu wengi wanaposikia soko la hisa, basi hufikiri kinachouzwa na kununuliwa ni hisa pekee. Lakini huu siyo ukweli. Kwenye soko la hisa kuna bidhaa mbalimbali za kifedha ambazo zinapatikana. Bidhaa hizi za kifedha kwa pamoja zinajulikana kama amana. Na hizi ndizo hupatikana kwenye masoko ya hisa na njia nyingine za (more…)

BIASHARA LEO; Mteja Mmoja Asikufanye Ubadili Biashara Yako Yote…

By | September 19, 2017

Wakati unapoanza biashara yoyote, huwa unakuwa na mawazo yako juu ya biashara hiyo. Huwa unakuwa na mipango mikubwa juu ya biashara yako na wateja unaowalenga pia. Lakini unapoingia kwenye biashara hasa, mambo huwa tofauti na ulivyotegemea. Wakati mwingine kitu ulichofikiri wateja wanakitaka kweli kinakuwa siyo kitu chenyewe. Hili linakufanya ubadili (more…)

#KURASA_KUMI; Furaha Ni Kuishi Sasa.

By | September 19, 2017

KITABU; Philosophy for life and other dangerous situations : ancient philosophy for modern problems / Jules Evans UKurasa 84 – 93.. Epicurus ni mwanafalsafa aliyeamini kwenye furaha kwenye kuishi kwenye wakati ujao. Epicurus aliamini kwamba lengo letu hapa duniani ni kuwa na maisha ya furaha na kuepuka maumivu. Alianzisha falsafa (more…)

UKURASA WA 993; Jambo Moja Kwa Wakati…

By | September 19, 2017

Unaweza kupiga hatua moja kwa wakati, na ukaendelea hivyo mpaka ukafika mbali mno. Hata kama umechelewa kiasi gani, ukikazana kupiga hatua mbili kwa wakati mmoja, hutaenda mbele, badala yake utaanguka. Wahenga pia walishatuambia anayekimbiza sungura wawili, hawezi kumkamata hata mmoja. Kwa sababu wote wanakupa tamaa na mwisho kila mmoja atakimbilia (more…)