UKURASA WA 833; Kanuni Moja Ya Maajabu Ya Mafanikio Kwenye Biashara…

By | April 12, 2017

Haipo, watu wanapenda kusikia kanuni moja ya maajabu, yaani kitu kimoja tu ambacho ukikifanya biashara yako itafanikiwa sana. Ukitaka uwapate wengi zaidi sema siri, maana pia watu wanaamini zipo siri ambazo wao hawazijui ila wengine ndiyo wanazijua. Pia hakuna siri, siri ni kile usichokijua wewe, ambacho hakijafichwa popote, ila wewe (more…)

UKURASA WA 832; Tabia…

By | April 11, 2017

Huwa tunazijenga tabia, na baada ya hapo, tabia zinatujenga. Tabia ni sawa na uzi mwembamba ambao unaweza kuukata bila shida ukiwa mmoja. Lakini kila siku unajisokotea uzi huu taratibu, unapokuja kustuka umeshajisokota mwili mzima na huwezi tena kuukata. Hakutakuwa na kelele yoyote kwamba sasa unaanza kutengeneza tabia, bali utaanza kufanya (more…)

💥 #TAFAKARI YA LEO; SOLUTION VS DISTRACTION…

By | April 11, 2017

Hongera rafiki yangu kwa siku hii nzuri sana ya leo. Ni nafasi ya kipekee kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili tuweze kupata matokeo makubwa. Tunajua kabisa mafanikio yetu yanatokana na kazi, hivyo lazima tuweke kazi ya uhakika kila siku. Msingi wetu ni NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA ambapo tutaweza kufanya makubwa (more…)

UKURASA WA 831; Ukuta Usioonekana…

By | April 10, 2017

Zamani ulikuwepo ukuta halisi, ukuta unaoonekana ambao unawazuia watu kufanya kile ambacho walitaka kufanya. Palikuwepo na wafanyabiashara wachache sana, hivyo kuingia kwenye biashara yoyote ilikuwa ni vita, kwa sababu ungefanyiwa hujuma mpaka ukimbie mwenyewe. Palikuwepo na studio chache za kurekodi muziki hivyo mtu akikuambia wewe huwezi kuimba ndiyo imetoka, huna (more…)

KUISHI FALSAFA YA USTOA.

By | April 9, 2017

Kama ambavyo tumejifunza mpaka sasa, ustoa ni moja ya falsafa nzuri sana za maisha kwa sababu inatupa utulivu ndani ya nafsi zetu na kutuwezesha kuwa na maisha bora bila ya kujali tunapitia nini. Lakini kuishi falsafa hii ya ustoa kwa mgeni inaweza kuwa changamoto kubwa. Hii ni kwa sababu wengi (more…)

KUIFIKIRIA FALSAFA YA USTOA.

By | April 9, 2017

Kama ambavyo tumeona, ni muhimu sana mtu kuwa na falsafa ya maisha, kwa sababu bila ya falsafa, hakuna hatua kubwa mtu anaweza kupiga. Na kama ambavyo tumejifunza kwenye falsafa ya ustoa, dhumuni kuu la falsafa ya ustoa ni kuwa na utulivu kwenye maisha, kwa kuishi kulingana na asili. Zipo falsafa (more…)

USTOA WA KISASA – Anguko la ustoa wa zamani.

By | April 9, 2017

  Kama ambavyo tumeona, falsafa ya ustoa ilikuwa na nguvu kubwa wakati wa utawala wa Roma. Marcus Aurelius ndiye aliyekuwa mstoa wa mwisho mwenye nguvu. Marcus pia alikuwa mtawala wa Roma, lakini hakuipandikiza falsafa hii kwa waroma, aliishi yeye kama yeye. Baada ya Marcus, na kifo cha wastoa kama Epictetus (more…)

KUWA MSTOA – Anza Sasa Na Jiandae Kudhihakiwa.

By | April 9, 2017

Kuiishi falsafa ya ustoa siyo kitu rahisi, Kwanza kutokana na mazoea ambayo tayari tunayo, tunahitaji kubadili mengi tuliyokuwa nayo kwenye maisha na kubadili maisha yetu kwa ujumla. Na hakuna kitu kigumu kwa wengi kama wao wenyewe kuridhia kubadilika. Pia ugumu unakuja pale wengine wanapokuchukulia kwamba falsafa yako ni ya ajabu. (more…)