UKURASA WA 152; Kila Mtu Anawinda Kitu Hiki Muhimu Ulichonacho, Kuwa Makini.

By | June 1, 2015

Tunaishi dunia ambayo kila mtu kuna kitu anatafuta. Na kipimo kimoja ambacho kinapima kile ambacho kila mtu anataka ni fedha. Kama unataka kuwa na maisha yenye hadhi nzuri basi yatapimwa kwa kiwango cha fedha unachotengeneza au ulichonacho. Hivyo kwa kila wakati kila mmoja wetu anapambana kupata fedha. Tunafanya kazi na (more…)

UKURASA WA 151; Je Unazalisha Au Wewe Ni Mtumiaji Tu?

By | May 31, 2015

Katika dunia tunayoishi, kuna makundi mawili ya watu. Kuna kundi la watu ambao ni wazalishaji, hawa ni watu ambao wanatuletea vitu vyote tunavyotumia. Simu, tv, vyakula vizuri, vitabu, makala tunazosoma, nguo tunazovaa, magari na vingine vingi. Kundi la pili ni la watumiaji. Hawa ni watu ambao wanatumia vitu hivi vinavyotolewa (more…)

BIASHARA LEO; Hiki Ndio Kikomo Cha Biashara Yako Kukua.

By | May 30, 2015

Biashara yako ina ukomo wake wa kukua, yaani biashara inaweza kukua mpaka itakapofikia ukomo huo utakaoujua leo. Bila ya kujua ukomo hii ni vigumu sana kwa biashara yako kuweza kukua zaidi. Wafanyabiashara wengi ambao biashara zao zimedumaa hawajui kwamba tayari zimefikia ukomo. Hivyo hukazana kufanya mambo mengi ambayo bado hayasaidii (more…)

UKURASA WA 150; Sababu Moja Inayokufanya Unakwama.

By | May 30, 2015

Moja ya vitu vizuri nilivyojifunza kwenye maisha ni kwamba, watu huwa wanayafanya maisha yao kuwa magumu wao wenyewe. Yaani kama unaona maisha yako ni magumu, basi wewe mwenyewe umechangia sehemu kubwa sana ya ugumu huo. Unaweza kukataa na kusingizia kila kitu unachoweza, serikali ambayo haitoi ajira, uchumi ambao ni mgumu, (more…)

Ukurasa Wa 149; Hawa Ndio Watu Unaotakiwa Kuwafikiria Zaidi.

By | May 29, 2015

Utakapoamua kuboresha maisha yako, utakapoamua kufanya tofauti na ulivyokuwa unafanya na utakapoanza kupata majibu ya tofauti na uliyokuwa unapata mwanzo, kuna watu watakuchukia. Nataka nikuambie hilo wazi. Kuna watu watakuchukia wazi wazi na kukuambia huwezi au unapoteza muda wako, na hata ukiweza watakuambia subiri. Na kuna wengine watakuchukia kwa ndani (more…)

BIASHARA LEO; Hatua Za Kuajiri Wafanyakazi Bora Kwenye Biashara Yako.

By | May 28, 2015

Mafanikio ya biashara yako yatategemea wafanyakazi utakaokuwa nao kwenye biashara yako. Kwanza kama unafikiria kw anini uajiri, kama bado ni mfanyabiashara mdogo na unafanya kila kitu peke yako, ni muhimu sana kuandaa mpango wa kuajiri ili wakati wa kuajiri utakapofika usipate tabu. Jua majukumu unayohitaji kuyatoa kwa wengine ili biashara (more…)