Waliofika kileleni…

By | December 10, 2014

Watu waliofika kwenye kilele kikubwa sio kwa sababu watu hao waliruka na kujikuta kileleni, ila kwa sababu watu hao, wakati wenzao wamepumzika wao waliendelea kukomaa na kuendelea na safari. Endelea na safari yako wakati wengine wamelala… Endelea na safari yako wakati wengine wanastareheka… Endelea na safari yako wakati wengine wanabishana (more…)

Hasara Za Tabia Ya Kuahirisha Mambo.

By | December 9, 2014

Katika kujijengea tabia za mafanikio mwezi huu wa kumi na mbili tunajadili jinsi ya kuachana na tabia ya kuahirisha mambo. Tabia ya kuahirisha mambo ni tabia ambayo imeathiri watu wengi sana na kuwafanya washindwe kufikia malengo yao. Wiki iliyopita tuliona maana ya tabia ya kuahirisha mambo na kwa nini watu (more…)

Ana Miaka 53 Ila Bado Analishwa Uji…

By | December 9, 2014

Kwa kawaida mtu yeyote anayezaliwa huwa anapitia vipindi tofauti kwenye maisha yake. Kwanza kabisa anaanza kama mtoto ng’aa, ambapo anakuwa anategemea kunyonya maziwa ya mama tu. Anaendelea kukua na baadae anakuwa analishwa uji, huku akikazana kutambaa na hatimaye kutembea. Baada ya muda anaanza kula matonge ya ugali na kukimbia mwenyewe.. (more…)

Mambo ya kuzingatia kabla hujachukua mkopo wa biashara.

By | December 8, 2014

Wewe kama mjasiriamali kuna wakati ambapo utahitaji fedha zaidi ili uweze kukuza biashara yako. Fedha hizi unaweza kuzipata kupitia mikopo inayotolewa kwenye taasisi mbalimbali za kifedha. Wiki iliyopita hapa kwenye KONA YA MJASIRIAMALI tulijadili umuhimu wa taasisi za kifedha katika maendeleoa ya ujasiriamali. Katika makala ile tuliona vigezo muhimu unavyotakiwa (more…)

NENO LA LEO; Jambo Kubwa Na La Kushangaza.

By | December 8, 2014

We can easily forgive a child who is afraid of the dark; the real tragedy of life is when men are afraid of the light. –Plato Tunaweza kumsamehe mtoto mdogo anayeogopa giza; ila jambo kubwa na la kushangaza kwenye maisha ni pale mtu mzima anapoogopa mwanga. Ni kipi unachokiogopa kukifanya (more…)

Nyasi Za Upande Wa Pili Ni Za Kijani Zaidi…

By | December 8, 2014

Angalia zile nyasi za upande wa pili, ni za kijani zaidi ya nyasi zilizopo upande wako… Hii ni fikra ambayo huwa inamjia kila mtu katika sehemu aliyopo iwe ni maisha, kazi au biashara. Unaweza kuona wenzako wana maisha mazuri kuliko hayo uliyoko nayo kwa sababu tu unaona wanatembelea magari mazuri (more…)

Tulikuona Wakati Unakuja Mjini…

By | December 7, 2014

Tulikuona wakati unakuja mjini, usijione mjanja leo… Ulikuja umevaa yeboyebo na nguo umebeba kwenye mfuko wa rambo, leo unajiona unajua sana… Hayo ni maneno ya hovyo sana yanayotolewa na watu walioshindwa. Watu ambao wamepoteza muda wao kwa kufikiri wao ni wakongwe na anakuja mtu na kuwaacha wakishangaa. Ili kujifariji kwamba (more…)