Tag Archives: CHANGAMOTO ZA BIASHARA

BIASHARA LEO; Usihofu Kama Watu Hawakuelewi.

By | June 6, 2015

Moja ya changamoto za kuwa mjasiriamali ni kwamba watu wengi hawatakuelewa. Kama unayafanyia kazi haya mambo ambayo unajifunza hapa kila siku, watu wengi hawawezi kukuelewa. Usiogope pale hali hii inapotokea, maana ndio umeanza kuuelewa ujasiriamali. Watu wengi hawawezi kukuelewa kwa sababu walitegemea ufanye biashara kama wanavyofanya wao. Ufungue biashara yako (more…)

BIASHARA LEO; Kabla Hujaanza Biashara Yoyote Mpya, Zingatia Jambo Hili Moja Muhimu Sana.

By | June 2, 2015

Biashara mpya zina kasi kubwa sana ya kushindwa. Hapa kwetu Tanzania hatuna tafiti za kutosha ila kwa nchi zilizoendelea na zilizofanya tafiti, biashara 8 kati ya 10 zinazoanzishwa hufa mwaka mmoja baada ya kuanzishwa. Hii ni hatari sana na kwa uzoefu tu hapa kwetu hali inaweza kuwa mbaya zaidi. Kuna (more…)

Changamoto ya kuendesha biashara wakati bado umeajiriwa.

By | May 18, 2015

Ni hali iliyowazi kwamba maisha yanakuwa magumu kadiri siku zinavyokwenda. Na gharama za maisha zinaongezeka huku vipato vya Ajira vikibaki pale pale au kuongezeka kidogo sana. Hali hii imewafanya waajiriwa wengi kujiingiza kwenye ujasiriamali. Hivyo licha ya kipato cha ajira wanapata kipato kingine cha ziada kupitia ujasiriamali wanaofanya. Waajiriwa wanakuwa (more…)

BIASHARA LEO; Faida Ya Kushindwa Kwenye Biashara.

By | April 8, 2015

Kama utajifunza biashara kabla ya kuingia kwenye biashara utajifunza vitu vingi sana. Utajua kila aina ya kanuni na kila aina ya mbinu ya kuanza na kukuza biashara yako. Lakini unapoingia kwenye biashara yenyewe mambo hayaendi kiulaini kama ulivyokuwa unajifunza. Kwenye biashara halisi sio kwmaba kila kitu kitakwenda kama ulivyokuwa umepanga (more…)

BIASHARA LEO; Kitu Hiki KImoja Kitakufanya Ushindwe Kwenye Biashara.

By | March 29, 2015

Moja ya kauli za kusikitisha sana ninayokutana nayo kwa watu ni kwmaba, najaribu kufanya hii biashara nione kama itanipa faida. Kwa kauli hii tu tayari umeshashindwa kwenye biashara unayotaka kufanya. Biashara haijaribiwi, ila inafanywa. Unaposema unajaribu biashara maana yake unaifanya kwa majaribio tu na kama majaribio yako yatakwenda vizuri utaendelea (more…)