Tag Archives: MBINU ZA MAFANIKIO

Kitu Kimoja Cha Kufanya Kila Siku Ili Ufikie Malengo Yako 2015…

By | February 1, 2015

Mpaka sasa umeshajifunza mbinu nyingi sana za kukuwezesha kufikia malengo uliyojiwekea kwa mwaka huu 2015. Kama una malengo na mipango tayari ni muhimu sana kutumia yale unayojifunza ili uweze kufikia malengo yako. Mpaka kufikia leo kuna watu ambao tayari wameshasahau malengo waliyokuwa wamejiwekea kwa mwaka huu 2015. Hii inatokana na (more…)

Ni Muda Unaenda Haraka Au Wewe Unaenda Taratibu?

By | February 1, 2015

Kufumba na kufumbua mwezi wa kwanza hatunao tena… Tuko mwezi wa pili na siku sio nyingi tutauanza mwezi wa tatu. Ni majuzi tu tulikuwa tunasherekea mwaka mpya, sasa hivi ni kama umechakaa. Muda unakwenda haraka eh? Hiki ndio kila mtu anachosema, kwamba muda unakwenda haraka sana. Lakini je ni kweli? (more…)

Huu Ni Mwaka Wa Kuacha Unafiki…

By | January 31, 2015

Umefika wakati wa kuacha unafiki.. Maana kuendelea na unafiki huu hakuwezi kukusaidia tena. Swali la msingi; wakati unazaliwa au unakua ni nani alikuambia maisha yatakuwa rahisi? Kwamba utapata kila kitu kwa urahisi? Kwamba kutakuwa na njia za mkato za wewe kupata unachotaka? Hakuna popote umewahi kuambiwa hivi. Lakini kwa unafiki (more…)

Je Upo Tayari Kupata Unachotaka? Siri Ni Hii Moja…

By | January 30, 2015

Unataka nini kwenye maisha yako? Maana kama hujui unachotaka tayari umeshakikosa. Je upo tayari kupata hiko unachotaka? Ni nini kinakuzuia mpaka sasa hujakipata? Haya ni maswali muhimu sana ya kujiuliza. Maana kuna kitu ambacho kimekufanya mpaka sasa hujapata unachotaka na kushindwa kujua kitu hiko kitaendelea kukuzuia. Jua kikwazo ni nini (more…)

Nafasi Ya Wewe Kuwa Bora Kila Siku… NA ZAWADI YA TSH 365,000/=

By | January 29, 2015

Kama mpaka sasa huna utaratibu wa kujifunza kila siku, tayari upo nyuma sana katika kufikia mafanikio kwenye jambo lolote unalofanya kwenye maisha yako. Kujifunza kila siku ni hitaji la chini sana la wewe kuweza kufikia mafanikio. Na tunaposema kujifunza kila siku ni kila siku kweli, jumatatu mpaka jumapili na kurudia (more…)

Unataka Kujifunza Kitu Chochote Unachoona Ni Kigumu? Fanya Hivi…

By | January 27, 2015

Njia bora kabisa ya kujifunza ni kufanya, kutenda. Utasoma vitabu vyote, utafundishwa na walimu waliobobea ila kama hutatendea kazi yale uliyojifunza ni kazi bure. Hakuna mtu aliyewahi kujifunza na akajua kuendesha baiskeli kwa kusoma vitabu tu. Hata baada ya maelekezo ulihitaji kuipanda baiskeli, kuanguka na hata kuumia ndio ukajua kuendesha (more…)

Mambo Matatu Muhimu Ya Kufanya Siku Ya Jumapili Ili Kuwa Na Wiki Yenye Mafanikio

By | January 25, 2015

Jumapili ni siku muhimu sana kama unataka kuwa na wiki yenye ufanisi mkubwa. Ni siku ambayo kama ukiitumia vizuri utakuwa na wiki yenye mafanikio na kama ukiitumia vibaya utakuwa na wiki mbaya na ya kupoteza muda. Kuna vitu vitatu unavyoweza kufanya siku ya jumapili ili kuwa na wiki yenye ufanisi (more…)

Kitu Muhimu Cha Kufanya Kabla Ya Kutumia Muda Au Fedha.

By | January 25, 2015

Muda una thamani kubwa sana kuliko fedha, hii ni kwa sababu ukipoteza fedha unaweza kupata nyingine ila ukipoteza muda huwezi kuupata tena. Ila muda na fedha vina tabia moja inayofanana, ukivitumia bila ya kuandika kwenye karatasi unavipoteza. Kitu muhimu cha kufanya kabla ya kutumia fedha au muda ni kupangilia matumizi (more…)