Category Archives: #TAFAKARI YA LEO

#TAFAKARI YA LEO; KUJUA PEKEE HAITOSHI…

By | January 15, 2021

Hautafanikiwa na kuwa na maisha bora kwa sababu unajua vitu vingi. Bali utafanikiwa kwa kuweka kwenye matendo yale unayojua, hata kwa kiwango kidogo tu. Kujifunza kitu mara moja hakutoshi, unapaswa kurudia mara kwa mara mpaka kitu hicho kiwe sehemu yako, kiwe asili kwako. Chagua misingi utakayoendesha nayo maisha yako, iishi (more…)

#TAFAKARI YA LEO; NATAKA WEWE USHINDE…

By | January 13, 2021

Tunategemeana sana kwenye maisha, hakuna anayeweza kushinda peke yake. Ushindi wa mwalimu ni wanafunzi wanaofaulu, ushindi wa daktari ni wagonjwa wanaopona na ushindi wa mpishi ni watu wanaoshiba na kufurahia chakula. Chochote unachofanya, angalia wale unaowalenga wananufaikaje, wajibu wako ni kuhakikisha wanashinda, maana wakishinda hao, ndiyo na wewe unashinda pia. (more…)

#TAFAKARI YA LEO; FANYA CHOCHOTE…

By | January 12, 2021

Kama upo njia panda na hujui kipi cha kufanya, anza kufanya chochote. Kwa kufanya chochote ni rahisi kufika kwenye kilicho sahihi kwako kufanya kuliko kuendelea kusubiri. Kwa kuanza na chochote unajifunza na kupata msukuko wa kuendelea kuliko kusubiri. Unaweza kusubiri utakavyo, lakini tambua muda haukusubiri na muda ukishapita haurudi tena. (more…)

#TAFAKARI YA LEO; USIPOST UJINGA, FANYA KAZI…

By | January 11, 2021

Mitandao ya kijamii imewageuza watu kuwa misukule wanaofanya kazi bila kulipwa. Inawahadaa watu kwa umaarufu feki unaopatikana kwa kupost vitu vya kijinga mtandaoni. Lakini umaarufu huo hauna manufaa kwa mtu zaidi ya kumharibia sifa yake. Umaarufu wenye manufaa ni ule unaotokana na kazi inayotoa thamani kwa wengine, ila huo unahitaji (more…)

#TAFAKARI YA LEO; KUWA CHANYA KUNALIPA…

By | January 10, 2021

Katika kila jambo au hali unayopitia, kuwa chanya kunalipa kuliko kuwa hasi. Kuwa chanya kunakuonesha fursa zaidi wakati kuwa hasi kunakuonesha matatizo zaidi. Kuwa chanya kunakupa matumaini wakati kuwa hasi kunakukatisha tamaa. Pamoja na manufaa haya ya kuwa chanya, bado wengi hukimbilia kuwa hasi. Hiyo ni kwa sababu kuwa hasi (more…)

#TAFAKARI YA LEO; FANYA MAAMUZI YA MAISHA YAKO…

By | January 9, 2021

Watu wengi ni wazito kufanya maamuzi ya maisha yao. Hiyo ni kwa sababu kufanya maamuzi ni kugumu kuliko kufuata mkumbo. Wengi huishia kuangalia wengine wanafanya nini na kufanya pia, bila kujiuliza kama ndiyo kitu sahihi kwao kufanya. Wewe usiwe hivyo, usiruhusu maisha yako yaendeshwe na wengine kwa namna watakavyo. Fanya (more…)

#TAFAKARI YA LEO; KUIFANYA DUNIA IWE UNAVYOTAKA…

By | January 8, 2021

Hicho ni kitu ambacho kipo nje ya uwezo wako kabisa. Lakini wengi wamekuwa wakihangaika nacho, wakitaka kuifanya dunia iende wanavyotaka wao na watu wawe vile wanavyotaka. Hilo linaposhindikana wanaumia na kukata tamaa. Mtu pekee unayeweza kumdhibiti na kumbadili hapa duniani ni wewe mwenyewe. Hivyo peleka nguvu zako kwenye kujibadili na (more…)

#TAFAKARI YA LEO; KABLA HUJAWEKA JUHUDI…

By | January 7, 2021

Kabla hujaweka juhudi kwenye chochote unachofanya, hakikisha kwanza hicho ndiyo kitu sahihi kwako kufanya. Kabla hujazidisha mbio, hakikisha uko kwenye uelekeo sahihi. Kwa sababu haijalishi ni juhudi au mbio kiasi gani unaweka, kama unachofanya siyo sahihi, unazidi kujipoteza. Siku zinaanza na kuisha na kila siku unakuwa ‘bize’ na kuchoka kweli (more…)

#TAFAKARI YA LEO; JIFUNZE KWA KILA MTU…

By | January 6, 2021

Kila mtu unayekutana naye, kuna kitu cha kujifunza kutoka kwake. Inaweza kuwa kitu cha kuanza kufanya au kuacha kufanya. Kuwa tayari kujifunza na utajifunza mengi mno. Unaweza kwenda mahali kupata huduma fulani na kisha ukapata huduma ambayo ni mbovu mno. Badala tu ya kulalamikia huduma mbovu uliyopata, jifunze kutokufanya hivyo (more…)