Category Archives: #TAFAKARI YA LEO

#TAFAKARI YA LEO; JINSI YA KWENDA NA WENYE IMANI NA ITIKADI KALI…

By | May 29, 2021

Kwenye maisha yako utakutana na watu wenye imani na itikadi kali juu ya kitu ambacho unajua kabisa siyo sahihi. Ushahidi uko wazi kabisa kwamba wanachoamini watu hao siyo sahihi, lakini bado wanakiamini na kukisimamia. Unaweza kuona ni wajibu wako kuhakikisha unawashawishi waachane na imani hizo, lakini utakuwa umefanya makosa sana (more…)

#TAFAKARI YA LEO; MAHALI PA KUPATA USHAURI MZURI…

By | May 28, 2021

Umekuwa unahangaika sana kutafuta ushauri kwa watu wasiojua chochote kuhusu wewe na unachofanya, wakati yupo anayekujua vizuri na kuweza kukushauri vyema kabisa.Sauti iliyo ndani yako ni mshauri mzuri kwako, sauti hiyo inakujua wewe tangu unazaliwa, inakumbuka kila ambacho umewahi kupitia na inajua nini kizuri kwako.Sauti hiyo imekuwa inajaribu kuwasiliana na (more…)

#TAFAKARI YA LEO; UNALISHA NINI AKILI YAKO….

By | May 27, 2021

Hebu fikiria umekaa mwezi mzima bila kula chakula kabisa, mwili wako utakuwa katika hali gani? Vipi ukikaa mwezi mzima bila kuoga kabisa? Hutafikisha hata mwezi, mwili utakuwa umeharibika kabisa. Sasa pata picha ni kwa kiasi gani unaharibu akili yako kwa kutokuilisha chakula sahihi. Matokeo ya mwili yanaonekana haraka kwa sababu (more…)

#TAFAKARI YA LEO; USISUBIRI HAMASA…

By | May 25, 2021

Usisubiri mpaka upate hamasa ndiyo uanze kufanya kile unachotaka kufanya. Badala yake anza kukifanya na utatengeneza hamasa ya kuendelea kukifanya zaidi. Ukisubiri mpaka upate hamasa ndiyo uanze utajichelewesha. Ukianza kabla hata hujawa na hamasa unajenga hamasa ya kuendelea kufanya. Kama ilivyo kanuni ya sayansi, kilichosimama huendelea kusimama wakati kilicho kwenye (more…)

#TAFAKARI YA LEO; IPE AKILI MAZOEZI…

By | May 22, 2021

Moja ya nadharia ya mageuzi (evolution) ni kwamba kiungo cha mwili kinachotumiwa sana kinakuwa imara na kile kisichotumiwa kinakuwa dhoofu. Ndiyo maana kama unatumia sana mkono wa kulia, unakuwa na nguvu kuliko wa kushoto. Kadhalika ndivyo ilivyo kwenye akili, ukiitumia sana inakuwa imara, usipoitumia inakuwa dhoofu. Akili dhoofu haiwezi kufanya (more…)

#TAFAKARI YA LEO; KUKUTANA NA BAHATI…

By | May 21, 2021

Kila anayefikia mafanikio makubwa kwenye maisha, huwa kuna bahati anakutana nazo kwenye safari yake ya mafanikio. Lakini bahati hizi haziendi kwa aliyelala, bali zinaenda kwa aliye kwenye mapambano. Kwa kuwa hujui lini bahati itakufikia, wajibu wako mkubwa ni kuhakikisha uko hai na uko kwenye mapambano ili bahati inapokuja ikukute. Ukikata (more…)

#TAFAKARI YA LEO; NI VIWANGO ULIVYOJIWEKEA…

By | May 20, 2021

Kile ambacho wengine wanakupa kwenye maisha yako, ni kulingana na viwango ulivyojiwekea wewe mwenyewe. Ukijiwekea viwango vya juu na kuvisimamia, watakupa kadiri ya viwango hivyo. Hakuna anayekudharau au kukutukana kama huvumilii vitu hivyo. Kupata kile unachotaka, jiwekee viwango vyako kisha kataa kabisa kupokea au kuvumilia chochote chini ya viwango hivyo. (more…)