Tag Archives: KURASA 365 ZA MWAKA 2015

UKURASA WA 188; Matatizo Yote Ya Mahusiano Huanzia Hapa.

By | July 7, 2015

Kama kuna kazi ngumu hapa duniani basi ni kuishi. Ndio maisha ni mazuri na ndio maisha ni matamu ila ni kazi kubwa sana kuweza kuyaishi. Ni kazi kubwa kuyaishi kwa sababu huwezi kuishi maisha ya peke yako. Umezungukwa na watu wengi na watu hawa wana tabia tofauti tofauti. Watu wote (more…)

UKURASA WA 187; Usikubali jua lizame leo kabla hujafanya kitu hiki muhimu.

By | July 6, 2015

Siku ya leo kuna watu wengi sana watakaokuudhi. Kuna watu wengi watakukasirisha na wengine watakufanya ujisikie vibaya sana. Kwa hasira inayotokana na watu hawa unaweza kufanya maamuzi ambayo sio mazuri sana kwao na kwako pia. Ila kumbuka mara nyingi unapokuwa na hasira huwezi kufanya maamuzi ambayo ni sahihi. Na hata (more…)

UKURASA WA 186; Kama Utashindwa Kufanya Chochote Utakachojifunza, Basi Fanya Hiki Kimoja Tu, Na Maisha Yako Yatagusa Wengine.

By | July 5, 2015

Nimekuwa nakushirikisha mambo mengi sana ambayo unahitaji kuyafanya ili kuboresha maisha yako. Mambo haya yanahitaji wewe ubadilike, uanze kufanya tofauti na ulivyozoea kufanya na sio kitu rahisi sana. Kuacha kuangalia tv na kujisomea mambo yatakayokuweka mbele zaidiinahitaji kujitoa kweli. Kuacha kukaa na jamaa zako kila jioni mkipata moja moto na (more…)

UKURASA WA 185; Bila Kuwajua Watu Hawa Watatu Na Kumalizana Nao, Sahau Kuhusu Mafanikio.

By | July 4, 2015

Kuna watu watatu ambao kwa wewe kujua au kutokujua wamekuwa wanakuzuia kufikia mafanikio. Sio kwamba wao wanakuja na kukuzuia wewe kufikia mafanikio, ila kwa sababu yao wewe mwenyewe umeshindwa kufikia mafanikio kwenye maisha yako. Aina ya kwanza ya watu hawa ni watu ambao unataka kuwalinda. Kuna watu ambao wewe unataka (more…)

UKURASA WA 184; Ni Ruhusa Kwako Kubadili Mawazo.

By | July 3, 2015

Kwa mfano umeshakubaliana na mtu mtafanya kitu fulani halafu dakika za mwisho anakuambia nimebadili mawazo, sitafanya tena kama nilivyokuambia. Unajisikiaje? Unachukuliaje hali kama hiyo? Labda ni biashara na umeshakubaliana na mteja ila baadae anakuambia nimebadili mawazo. Au ni kwenye ajira na umeshakubaliana kitu fulani na mwajiri wako, umeshajiandaa kabisa na (more…)

UKURASA WA 183; Hakuna Anayekuchukia Wewe, Bali Wanahamisha Chuki Zao Kutoka Hapa.

By | July 2, 2015

Leo naomba tujadili kidogo kuhusu mtu kumchukia mwingine. Labda tuseme wewe kuna mtu anakuchukia, na amekuwa akikuonesha wazi wazi kwamba anakuchukia. Na hapa wewe huna tatizo lolote na mtu huyu. Unajaribu kuishi maisha yako bila hata ya kuingilia maslahi yao wala kuwavurugia chochote ambacho ni chao, lakini mtu anachagua tu (more…)

UKURASA WA 182; Urahisi Wa Kutengeneza Tabia Mbaya Na Ugumu Wa Kuishi Nazo.

By | July 1, 2015

Kuna jambo moja muhimu sana kwenye maisha ambalo unatakiwa kuwa unalijua. Na sio kulijua tu bali kulifanyia kazi kila siku maana kwa jambo hili moja ndio watu wanafanikiwa au wanashindwa. Jambo hilo ni kwmaba, tabia mbaya ni rahisi sana kutengeneza ila ni ngumu sana kuishi nazo. Na kwa upande wa (more…)

UKURASA WA 181; Kitu Cha Kufanya Pale Watu Wanapokuwa Hawakuamini Kama Unaweza.

By | June 30, 2015

Kama unataka kufanya jambo jipya, kama unataka kufanya jambo tofauti na wengine walivyozoea kufanya, naweza nikakuhakikishia jambo moja, WATU HAWATAKUAMINI. Watu hawatakuamini kwamba unaweza kufanya jambo hilo. Watu hawatakuamini kwamba kuna uwezekano wa jambo hilo kufanyika kwa tofauti. Na hapa ndipo watu wengi hukata tamaa na kuamua kuacha. Na hivyo (more…)

UKURASA WA 180; Pamoja Na Ushauri Mzuri Utakaopewa, Bado Kitu Hiki Utafanya Wewe Mwenyewe.

By | June 29, 2015

Unapokuwa unahitaji kufanya maamuzi ambayo huenda ni magumu kwenye kazi yako, biashara yako au hata maisha yako kwa ujumla, huwa unahitaji kupata ushauri. Unaweza kupewa ushauri mzuri sana kutoka kwa watu mbalimbali ambao unaweza kuwa unawaamini sana. Pamoja na ushauri huu muhimu bado wewe mwenyewe ndio utahitaji kufanya maamuzi ya (more…)

UKURASA WA 179; Unataka Kuwazidi Wengine? Umeshapotea.

By | June 28, 2015

Kwanza kabisa nikiri kwamba mimi huwa napinga sana dhana ya kushindana. Ndio kuna wakati ushindani unaonekana ni mzuri, lakini tatizo linakuja kwamba ukishakuwa na akili ya kushindana ndio unadumaa. Kama unakuwa na akili ya kushindana maana yake lengo lako kubwa ni kuwazidi wengine. Kuwa wa kwanza, kuwa bora zaidi ya (more…)