Tag Archives: KURASA 365 ZA MWAKA 2015

UKURASA WA 178; Lakini Nitapitwa…. (Sababu Ya Kijinga Inayokufanya Upoteze Muda)

By | June 27, 2015

Kama umejitoa ili kufikia mafanikio makubwa kwenye maisha yako, unahitaji kujifunza jinsi ya kutumia muda wako vizuri. Na kwa kuwa siku ina masaa 24 tu na hakuna anayeweza kuyazidisha, hakuna njia ya kuongeza muda ambao tunao. Kwa kuwa tunahitaji muda mwingi zaidi wa kufanya kile tunachofanya kwa ubora, basi tunahitaji (more…)

UKURASA WA 177; Ndio, Kwa Hiyo…

By | June 26, 2015

Ni vigumu sana kuweza kufanikiwa kwenye biashara, ndio kwa hiyo unahitaji kujipanga vizuri na kutokukata tamaa ili uweze kufikia mafanikio unayotarajia. Umri wangu ni mdogo/mkubwa sana kuweza kuanza kufanya jambo hili sasa. Ndio kwa hiyo unahitaji kuwa wa tofauti, licha ya umri wako kuwa usiotegemewa bado unaweza kuweka juhudi na (more…)

UKURASA WA 176; Hiki Ni Kipimo Kibovu Sana Cha Kupima Mafanikio Yako.

By | June 25, 2015

Kuna watu walikaa chini wakaamua kwamba kuwe na mtihani mmoja na wanafunzi wote waufanye, atakayepata maksi nyingi ndio amefaulu, atakayepata chache amefeli. Kuna watu pia wamekaa wakakubaliana kwamba ukiwa na magari ya kifahari, ukawa na nyumba ya kifahari na fedha isipokuwa tatizo kwako basi wewe umefanikiwa. Vyote hivi vinaweza kuwa (more…)

UKURASA WA 175; Ni Bora Kuweka Malengo Makubwa Na Kushindwa Kuliko Kuweka Malengo Madogo Na Kushinda.

By | June 24, 2015

Kwa jinsi tulivyolelewa na kukuzwa, kushindwa ni kitu cha aibu sana, ni kitu kinachostahili adhabu kubwa na kama utashindwa basi wewe ni mtu ambaye hufai. Si ndio tulivyofundishwa shuleni? Na ndio maana tulipewa adhabu kali pale ambapo tulishindwa kwenye kazi au mtihani. Kinyume na ilivyo kwenye elimu na hata kwenye (more…)

UKURASA WA 174; Je Unafanya Kile Unachopenda Au Unachotegemewa Kufanya?(Na Mbinu Za Kuweza Kufanya Kile Unachopenda Kufanya)

By | June 23, 2015

Ni jambo la kushangaza kwenye maisha kwamba baadhi yetu tunaishi maisha ambao hata hatuyajui. Tunatumia muda wetu mwingi kuishi maisha ambayo hata hatukupanga kuyaishi. Tunajikuta tunaishi maisha tofauti kabisa kwa sababu tunalazimika kuishi maisha ambao kila mtu anaishi. Tumeshazungumza sana kuhusu kuishi maisha ya wengine, leo ngoja tuzungumze kufanya kazi (more…)

UKURASA WA 173; Maamuzi Uliyofanya Awali Na Maamuzi Mapya.

By | June 22, 2015

Mambo unayofanya sasa yanatokana na maamuzi uliyofanya awali. Na maamuzi haya uliyofanya awali yalitokana na uelewa uliokuwa nao kwa kipindi hiko unafanya maamuzi hayo. Sasa swali linakuja kwako je sasa hivi bado una uelewa kama uliokuwa nao kipindi unafanya maamuzi? Kama jibu ni ndio basi endelea na kile unachofanya. Kama (more…)

UKURASA WA 172; Tatizo La Kuweka Kinyongo…

By | June 21, 2015

Ni kwamba unakosa nafasi ya kufuatilia mambo mengine muhimu kwako. Unaweza kujiaminisha kwamba kinyongo ulichomwekea mtu unastahili kabisa. Alininyanyasa sana nilipokuwa mdogo… Alinitesa sana katika mapenzi/ndoa…. Alinisababishia hasara kubwa kwenye biashara yangu… Alisababisha kifo cha mtu muhimu sana kwangu…. Na sababu nyingine nyingi unazojipa kwamba kuweka kinyongo kwa mtu ni (more…)

UKURASA WA 171; Unapokata Tamaa Maana Yake Umekubali Hivi.

By | June 20, 2015

Kukata tamaa maana yake umeamua kuondoka kwenye safari inayokupeleka kwenye mafanikio. Kukata tamaa maana yake umeamua kwamba nguvu zote ulizoweka, mambo yote uliyojitoa mpaka sasa hayana maana na umeamua kuyapoteza. Kukata tamaa maana yake ni kusema ulikuwa hujui kile ulichopanga kufanya na hata sasa hujui ni kitu gani unataka kufanya (more…)

UKURASA WA 170; Kinachoendelea Kukuzuia Kufikia Mafanikio Ni Hiki.

By | June 19, 2015

Kuna watu ambao wanakuwa wameanzia chini sana kwenye maisha. Wanatokea kwenye familia masikini, wanaweka juhudi nyingi sana na hatimaye wanafikia mafanikio waliyokuwa wanayatazamia. Ila baada ya kufikia mafanikio haya wanashindwa kwenda tena mbele na wanabaki palepale. Kwa kubaki palepale kwa muda mrefu wanajikuta wameachwa nyuma. Kuwa wengine wanaingia kwenye kazi (more…)

UKURASA WA 169; Utaendelea Kuidhulumu Dunia Mpaka Lini?

By | June 18, 2015

Kila mmoja wetu ana kitu kikubwa sana ambacho kipo ndani yake, ambacho akikitoa anaweza kuleta mabadiliko makubwa sana kwa watu wengine. Lakini tatizo kubwa ni kwamba wengi wetu hatutoi vitu hivi. Na tumekuwa tunaidhulumu dunia kwa kiasi kikubwa sana. Kazi ambayo nimekuwa naifanya, ya uandishi na kufundisha, imekuwa inawasaidia watu (more…)