UKURASA WA 858; Kuona Unachotaka Kuona…

By | May 7, 2017

Ukiacha kudanganywa na wengine, au kuwadanganya wengine, sisi binadamu tupo vizuri sana kwenye kujidanganya wenyewe. Kwa makusudi kabisa, tunaamua kuacha kuuangalia ukweli na kuangalia kile ambacho tunataka sisi, kile ambacho tunataka kuona.

IMG-20170218-WA0003

Changamoto kubwa kwenye hili ni kwamba unaweza hata usijue kama unajidanganya. Wewe unaona mambo yanakwenda vizuri tu, kumbe unachofanya ni kuangalia kile unachotaka kuona, na kujiaminisha mambo yapo vizuri.

Akili zetu nazo huwa hazituachi nyuma kwenye hili, pale unapojitokeza ushahidi ambao unakwenda kinyume na kile tunachotaka kuona, ambao unapinga kile tunachoamini, tunaupuuza au tunatafuta njia kuupinga ushahidi huo. Kwa njia hii tunaendelea kuona kile tunachotaka kuona, na kujiaminisha mambo yapo vizuri sana.

SOMA; Unachotaka Kuficha Ndicho Wanachotaka Kuona…

Ili kuondokana na hali hii, kuhakikisha tunauona ukweli kama ulivyo na siyo tunachotaka kuona, ni lazima tuwe tayari kupokea kila kinachokuja mbele yetu. Badala ya kupinga na kusema hiyo siyo kweli, tupokee na kuchunguza, tujipe muda wa kuchunguza na kujifunza zaidi. Lazima tuwe tayari kusikiliza yale yanayokwenda kinyume na kile tunachoamini. Lazima tuache kujiona sisi ndiyo tupo sahihi na wengine wote wanakosea. Na muhimu zaidi jua kila mtu anaweza kuwa sahihi na kila mtu anaweza kuwa anakosea, ikiwemo na wewe mwenyewe pia.

Unapoiweka akili yako kuuona ukweli kama ulivyo, utaacha kujifurahisha na kuona mambo kama yalivyo. Lakini kama utaendelea kutaka kuona unachotaka, utaendelea kujidanganya.

Kila la Kheri Rafiki Yangu.

Rafiki na Kocha wako,

Makirita Amani,

Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea www.kisimachamaarifa.co.tz/vitabu

Kupata blog ya kitaalamu unayoweza kuitumia kutengeneza kipato tembelea www.mtaalamu.net/patablog

Category: KURASA ZA MAISHA

About Dr. Makirita Amani

Dr. Makirita Amani ni daktari wa binadamu, mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali. Dhumuni lake kubwa kwenye maisha ni KUWASAIDA WATU KUBORESHA MAISHA YAO NA KUFIKIA MAFANIKIO MAKUBWA KUPITIA KAZI ANAZOFANYA. Mawasiliano 0717396253 email makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.