Author Archives: Dr. Makirita Amani

About Dr. Makirita Amani

Dr. Makirita Amani ni daktari wa binadamu, mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali. Dhumuni lake kubwa kwenye maisha ni KUWASAIDA WATU KUBORESHA MAISHA YAO NA KUFIKIA MAFANIKIO MAKUBWA KUPITIA KAZI ANAZOFANYA. Mawasiliano 0717396253 email makirita@kisimachamaarifa.co.tz

1624; Kazi, Huduma, Furaha…

By | June 12, 2019

Mafanikio siyo magumu kama wengi wanavyofikiri, mafanikio ni rahisi sana kama utachagua kuyaishi maisha yako. Mafanikio yanakuwa magumu kwa wengi kwa sababu wanajaribu kuwa watu ambao siyo, kwa kujilinganisha na watu wengine ambao hawawezi kuwa kama wao. Unapochagua kuwa wewe, unapochagua kuishi maisha yenye maana kwako, mafanikio ni kitu ambacho (more…)

1623; Uaminifu, Gharama Na Uharaka Wa Huduma…

By | June 11, 2019

Hivi ni vitu vitatu ambavyo vinachangia sana kwenye biashara kufanikiwa au kushindwa. Ukiweza kuvifanyia kazi vizuri vitu hivi vitatu kwenye biashara yako, utaweza kuikuza sana biashara yako na kufanikiwa. Kuna hali mbili inayohusisha vitu hivyo vitatu; Hali ya kwanza; uaminifu unakuwa juu, gharama za kuendesha biashara zinakuwa chini na huduma (more…)

#TAFAKARI YA LEO; USIFANYE MAMBO KUWA MABAYA ZAIDI…

By | June 11, 2019

“How much more harmful are the consequences of anger and grief than the circumstances that aroused them in us!” —MARCUS AURELIUS, MEDITATIONS, 11.18.8 Ni siku mpya, siku nzuri na ya kipekee sana kwetu. Ni fursa nyingine nzuri kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana. Kwa msingi (more…)

UKURASA WA 1622; Utafanikiwa Kwa Kuwa Wewe…

By | June 10, 2019

Kuna hadithi nyingi sana za mafanikio, kila aliyefanikiwa ana hadithi yake, na ukifuatilia hadithi nyingi, utakuta zinakinzana. Mmoja aliyefanikiwa atakuambia alifanya hivi, mwingine atakuambia alifanya kinyume chake. Sasa hapo unaweza kujikuta njia panda, usijue kitu gani sahihi kwako kufanya ili kufanikiwa. Wapo pia wengi ambao wamekuwa wanabadilika kila wanaposikia hadithi (more…)

#TAFAKARI YA LEO; HATA WEWE UNAWEZA PIA…

By | June 10, 2019

“If you find something very difficult to achieve yourself, don’t imagine it impossible—for anything possible and proper for another person can be achieved as easily by you.” —MARCUS AURELIUS, MEDITATIONS, 6.19 Tushukuru kwa nafasi hii nyingine ambayo tumeipata leo. Siyo wote ambao walipanga kuiona siku hii wameweza kuiona. Ila kwa (more…)

1620; Hii Kazi Unayojipa Siyo Yako, Unajitesa Bure…

By | June 8, 2019

Dunia ni kubwa na imejaa watu wa kila aina, Kuna watu wema na watu wabaya, kuna watu waaminifu na wasio waaminifu, kuna watu makini na walio wazembe. Hiyo ndiyo dunia, imekuwa hivyo kwa muda mrefu na itaendelea kuwa hivyo. Lakini wewe kwa sababu ambazo hatuzijui, umeamua kujipa jukumu la kuinyoosha (more…)