Author Archives: Dr. Makirita Amani

About Dr. Makirita Amani

Dr. Makirita Amani ni daktari wa binadamu, mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali. Dhumuni lake kubwa kwenye maisha ni KUWASAIDA WATU KUBORESHA MAISHA YAO NA KUFIKIA MAFANIKIO MAKUBWA KUPITIA KAZI ANAZOFANYA. Mawasiliano 0717396253 email makirita@kisimachamaarifa.co.tz

1579; Fanya Kwa Ukamilifu Au Usifanye Kabisa…

By | April 28, 2019

Matatizo makubwa kwenye dunia yanasababishwa na watu kufanya vitu nusu nusu, watu kuingia kufanya kitu huku mguu mmoja upo ndani na mguu mwingine upo nje. Watu hawafanikiwi kwenye biashara kwa sababu hawajaingia kwa ukamilifu na wazima wazima, wapo mguu mmoja nje mguu mwingine ndani. Hawajajitoa kweli kufanikiwa kwenye biashara hiyo, (more…)

#TAFAKARI YA LEO; MAHITAJI YAKO NDIYO YANAKUFANYA KUWA MTUMWA…

By | April 28, 2019

“Tantalus: The highest power is— Thyestes: No power, if you desire nothing.” —SENECA, THYESTES, 440 Hongera sana mwanamafanikio kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo. Ni nafasi ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana. Kwa msingi wetu wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA (more…)

1578; Nani Aliyeweka Hizo Sheria…

By | April 27, 2019

Kila sheria unayofuata kwenye maisha yako inapunguza uhuru wako. Hivyo kama unafuata kila sheria unayowekewa na wengine, huwezi kuwa huru na maisha yako. Jamii zina sheria nyingi sana, sheria ambazo hazina hata mantiki yeyote. Swali muhimu kujiuliza kabla hujafuata sheria yoyote unayowekewa ni watu gani walioweka hizo sheria? Je sheria (more…)

1577; Ukipunguza Utabiri Utajipunguzia Matatizo…

By | April 26, 2019

Ubongo wetu unapenda sana uhakika, wa mambo tuliyonayo sasa na hata yatakayotokea baadaye. Na hapa ndipo huwa tunapenda kutabiri mambo yatakayotokea baadaye. Kwa utabiri huu, tunajipa uhakika sasa, lakini tunajiweka kwenye nafasi ya kuumia zaidi baadaye. Kwa sababu wote tunajua ya kwamba hakuna utabiri wowote wenye uhakika wa asilimia 100. (more…)

1576; Unachouza Wewe Ni Furaha, Sahau Vingine Vyote…

By | April 25, 2019

Hitaji kuu la kila mtu ni furaha, hili ni hitaji la ndani kabisa la kila binadamu. Kila tunachofanya tunasukumwa na vitu viwili, kupata kile tunachotaka, ambacho ni furaha au kuepuka tusichotaka ambacho ni maumivu. Hakuna mtu mwenye akili timamu, anayefanya jambo la kumuumiza yeye mwenyewe kwa makusudi. Hata pale watu (more…)

1575; Sababu Tatu Sahihi Za Kutokuwa Tajiri…

By | April 24, 2019

Inapokuja kwenye utajiri, wengi huwa na sababu nyingi kwa nini hawajaweza kuufikia utajiri. Wengi husema wamejaribu sana lakini siyo bahati yao. Wengine hutoa lawama kwa wazazi kwa kutowapa misingi sahihi au elimu bora. Wengine hulaumu uongozi na hata mazingira au hali ya hewa kuwarudisha nyuma. Na wapo ambao husingizia majukumu (more…)