Author Archives: Dr. Makirita Amani

About Dr. Makirita Amani

Dr. Makirita Amani ni daktari wa binadamu, mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali. Dhumuni lake kubwa kwenye maisha ni KUWASAIDA WATU KUBORESHA MAISHA YAO NA KUFIKIA MAFANIKIO MAKUBWA KUPITIA KAZI ANAZOFANYA. Mawasiliano 0717396253 email makirita@kisimachamaarifa.co.tz

1534; Kazi Yako Inapaswa Kukutambulisha, Na Siyo Wewe Kuitambulisha Kazi Yako…

By | March 14, 2019

Katika zama tunazoishi sasa, mambo yanaenda kasi sana kiasi kwamba watu wamesahau kabisa nini kinahitajika kwenye kazi zao. Tunaishi kwenye zama za taarifa, ambapo watu hawawezi kutofautisha kati ya taarifa, maarifa na kelele. Kila mtu anapiga kelele akiamini kelele zaidi zitamfanya ajulikane na wengi. Na hapo ndipo unapoangalia mitandao ya (more…)

#TAFAKARI YA LEO; ADUI YAKO MKUBWA NI KUJIDANGANYA MWENYEWE…

By | March 14, 2019

“Zeno would also say that nothing is more hostile to a firm grasp on knowledge than self-deception.” —DIOGENES LAERTIUS, LIVES OF THE EMINENT PHILOSOPHERS, 7.23 Hongera mwanamafanikio kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo. Ni nafasi bora na ya kipekee kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo (more…)

1533; Hakuna Mkopo Usio Na Riba, Na Mkopo Wa Muda Una Riba Kubwa Sana…

By | March 13, 2019

Rafiki, ipo kauli maarufu kwamba hakuna kitu cha bure, kwamba unapoambiwa unapata kitu bure, kuna namna unagharamia kile unachopata bure. Inaweza kuwa kwenye ubora, kwamba unapata kitu bure, lakini hakitakuwa bora kama unavyotaka na huwezi kuhoji kwa sababu umepata bure. Au unaweza kulipa gharama kwenye utu wako, pale unapopata kitu (more…)

#TAFAKARI YA LEO; KUNA SIKU UTAELEWA…

By | March 13, 2019

“Whenever you find yourself blaming providence, turn it around in your mind and you will see that what has happened is in keeping with reason.” —EPICTETUS, DISCOURSES, 3.17.1 Ni siku nyingine mpya, siku nzuri na ya kipekee sana kwetu. Tumepata nafasi nyingine bora sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili (more…)

1532; Usitafute Usalama, Tafuta Uwezo…

By | March 12, 2019

Watu wengi wamekuwa wanafikiria lengo kubwa la maisha ni kutafuta usalama. Ndiyo maana wengi wanashindwa kuondoka kwenye ajira, kwa sababu wanaamini ni salama zaidi kwa upande wa kipato kuwa kwenye ajira kuliko kuwa nje ya ajira. Mambo mengi watu wanafanya kwa lengo la kuwa salama zaidi kwenye maisha yao. Lakini (more…)

1531; Wakati Wa Kusema Ndiyo Kwenye Kila Kitu…

By | March 11, 2019

Mara kwa mara nimekuwa nakushirikisha nguvu ya neno HAPANA. Umuhimu wa kutumia neno hili ili kuweza kupiga hatua kwenye maisha yako. Hili ni neno ambalo litakupa uhuru mkubwa sana kwenye maisha yako. Unapokuwa na uhaba wa muda, neno hapana ni rafiki sana kwako. Unapaswa kusema hapana kwenye vitu visivyo muhimu (more…)

#TAFAKARI YA LEO; ISHI BILA KIZUIZI…

By | March 11, 2019

“The unrestricted person, who has in hand what they will in all events, is free. But anyone who can be restricted, coerced, or pushed into something against what they will is a slave.” —EPICTETUS, DISCOURSES, 4.1.128b–129a Hongera sana mwanamafanikio kwa siku hii nyingine nzuri sana leo. Tumepata nafasi ya kipekee (more…)

1530; Mambo Mengi, Muda Mchache…

By | March 10, 2019

Hii ni kauli ambayo nimekuwa naona inatumiwa na watu wengi sana, wengi wanaitumia kama utani na wengine kama sababu. Lakini siyo wengi wanaoipa kauli hiyo uzito ambao inastahili. Kama utaipa kauli hiyo uzito unaostahili, itaweza kukusaidia sana kwenye maisha yako. Kama kweli unakiri mambo ni mengi na muda ni mchache, (more…)