Author Archives: Dr. Makirita Amani

About Dr. Makirita Amani

Dr. Makirita Amani ni daktari wa binadamu, mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali. Dhumuni lake kubwa kwenye maisha ni KUWASAIDA WATU KUBORESHA MAISHA YAO NA KUFIKIA MAFANIKIO MAKUBWA KUPITIA KAZI ANAZOFANYA. Mawasiliano 0717396253 email makirita@kisimachamaarifa.co.tz

1484; Mabadiliko Yanatokea Kwa Matendo, Siyo Maneno Au Mipango…

By | January 23, 2019

Mabadiliko kwenye maisha yetu ni matokeo ya hatua tunazochukua na siyo maneno au mipango tuliyojiwekea. Hata kama mipango ni mikubwa kiasi gani, hata kama tunaweza kuielezea na kubishana kiasi gani, hakuna matokeo tutakayoyapata kama hakuna hatua tunayochukua. Nakukumbusha hili rafiki, ili kila mara ujue wapi pa kupeleka nguvu zako kama (more…)

1483; Kufanya Kazi Na Kutoroka Kufanya Kazi…

By | January 22, 2019

Unahitaji nguvu ile ile kufanya kazi kama unayotumia kutoroka kufanya kazi. Watu wengi wamekuwa wanatumia nguvu zao siyo kwenye kufanya kazi, bali kutoroka kufanya kazi. Wanapanga vizuri ni hatua zipi watakazochukua, lakini inapofika wakati wa kuchukua hatua, hawakosi kuwa na dharura. Na hata wanapoanza kufanya na wanakutana na ugumu, wanaacha (more…)

1482; Umuhimu Wa Kujiwekea Viwango Vyako Vya Utendaji…

By | January 21, 2019

Watu wengi huwa hawapendi kujiwekea viwango vyao vya utendaji, kwa sababu wanaona wakishindwa kuvifikia basi watakuwa wamefeli kwenye maisha yao. Ni kama ambavyo baadhi ya watu wamekuwa hawapendi kuweka malengo kwa sababu wasipoyafikia basi watajiikia vibaya. Faida ya kujiwekea viwango vyako vya utendaji kwenye maisha siyo kufikia viwango hivyo, bali (more…)

#TAFAKARI YA LEO; UTARATIBU WA KUTAFAKARI KILA ASUBUHI….

By | January 21, 2019

“Ask yourself the following first thing in the morning: What am I lacking in attaining freedom from passion? What for tranquility? What am I? A mere body, estate-holder, or reputation? None of these things. What, then? A rational being. What then is demanded of me? Meditate on your actions. How (more…)

1481; Wewe Fanya Kazi Yako, Na Waachie Watu Wachague Wenyewe…

By | January 20, 2019

Mwandishi mmoja amewahi kuandika kwamba zama hizi ambazo mtu unaweza kufanya kila kitu mwenyewe, zimekuwa zama ambazo ubora wa kazi umeshuka sana. Akitumia mfano wa sanaa na uandishi, anasema zamani msanii aliweka nguvu zako kwenye kutengeneza sanaa yake, na kazi ya masoko na kusambaza ilikuwa kazi za watu wengine, hasa (more…)

#TAFAKARI YA LEO; WASHA UPYA FIKRA ZAKO.

By | January 20, 2019

“Your principles can’t be extinguished unless you snuff out the thoughts that feed them, for it’s continually in your power to reignite new ones. . . . It’s possible to start living again! See things anew as you once did—that is how to restart life!” —MARCUS AURELIUS, MEDITATIONS, 7.2 Hongera (more…)

1480; Matendo Yako Yaendane Na Maneno Yako…

By | January 19, 2019

Tumekuwa hatupati tunachotaka na wakati huo huo tunakuwa haturidhiki na maisha tuliyonayo. Na hii siyo kwa sababu wengine wanapata wanachotaka au wana maisha bora sana kuliko sisi, bali kwa sababu tunajua tunajikwamisha wenyewe. Tumekuwa tunajikwamisha sisi wenyewe pale ambapo maneno yetu hayaendani na matendo yetu. Tunasema na kuweka mipango mikubwa, (more…)