Author Archives: Dr. Makirita Amani

About Dr. Makirita Amani

Dr. Makirita Amani ni daktari wa binadamu, mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali. Dhumuni lake kubwa kwenye maisha ni KUWASAIDA WATU KUBORESHA MAISHA YAO NA KUFIKIA MAFANIKIO MAKUBWA KUPITIA KAZI ANAZOFANYA. Mawasiliano 0717396253 email makirita@kisimachamaarifa.co.tz

UKURASA WA 1333; Epuka Sumu Hii Pale Unapoweka Mipango Na Kuanza Kuifanyia Kazi…

By | August 25, 2018

Pamoja na kuwa na mipango mizuri ambayo mtu unaifanyia kazi, matokeo hayatakuja kama ulivyofikiri yanakuja. Kuna vitu vingi sana vitakwenda tofauti na unavyotegemea wewe. Pamoja na kujua kwamba vitu vitakwenda tofauti, pamoja na kujua kwamba kuna uwezekano ukawa umekosea na pia upo uwezekano wa kushindwa, kuna kosa moja kubwa sana (more…)

#TAFAKARI YA LEO; AMINI KWENYE UZURI WA NDOTO ZAKO…

By | August 25, 2018

The future belongs to those who believe in the beauty of their dreams. —Eleanor Roosevelt Hongera sana mwanamafanikio kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo. Ni nafasi bora na ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana. Kwa msingi wa NIDHAMU, UADILIFU NA (more…)

BIASHARA LEO; Mpe Mteja Sababu Za Kutosha Za Kununua Kwako, Na Sasa.

By | August 24, 2018

Unapochagua mteja wa biashara yako, na ukaona kabisa ana sifa zote za wateja wa biashara yako. Yaani ana uhitaji ambao biashara yako inaweza kumtimizia na pia anaweza kumudu gharama unayotoza. Kama mteja huyo hatanunua, basi kosa litakuwa lako na siyo la mteja. Mteja, hasa mpya, hatakuwa tayari kununua kwako mpaka (more…)

UKURASA WA 1332; Epuka Kugeuzwa Bidhaa Kwenye Dunia Ya Kelele…

By | August 24, 2018

Mtu mmoja aliwahi kusema maneno makali sana kuhusu mitandao ya kijamii. Alisema kwa mitandao ya kijamii ambayo watu wanatumia bure, wasichojua ni kwamba wao watumiaji ndiyo bidhaa ambayo mitandao hiyo inauza. Kwa sababu mitandao hiyo inaingiza fedha kwa njia kuu moja, ambayo ni matangazo. Na njia pekee wanayopata fedha kwenye (more…)

BIASHARA LEO; Siyo Idadi Ya Wateja, Bali Ubora Wa Huduma…

By | August 23, 2018

Kipimo cha wengi kwenye ukuaji wa biashara kimekuwa ni idadi ya wateja wanaokuja kwenye biashara hiyo. Hivyo mfanyabiashara anapoona wateja wanaokuja ni wengi, anaona biashara unakuwa na ina mafanikio makubwa. Na hili ndiyo linalopelekea wafanyabiashara wengi kushusha bei ya bidhaa au huduma zao, ili kuvutia wateja wengi zaidi. Kwa sababu (more…)

UKURASA WA 1331; Ni Watu Kama Wewe…

By | August 23, 2018

Tunapohitaji kushirikiana na wengine kwenye safari yetu ya mafanikio, huwa tunasahau kwamba wale ni watu kama sisi. Huwa tunasahau hilo na kuona labda ni watu wasioeleweka au wasioweza kutuelewa au kufanya kile tunachotaka. Tunasahau kwamba ni watu kama sisi, ambao wana mahitaji kama ambavyo tunayo sisi, ila tu yanatofautiana kwenye (more…)

#TAFAKARI YA LEO; WALIOSHINDWA WANATAKA NA WEWE USHINDWE…

By | August 23, 2018

Hongera sana mwanamafanikio kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo. Ni nafasi nyingine nzuri kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana. Kwa msingi wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa TATUA, AMUA NA ONGOZA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha (more…)

BIASHARA LEO; Jifunze Kupitia Biashara Kubwa Kuliko Yako…

By | August 22, 2018

Unapotaka kujifunza zaidi kuhusu biashara, unahitaji kuziangalia biashara ambazo ni kubwa kuliko biashara unayoendesha wewe. Hii ni kwa sababu biashara kubwa zina changamoto za tofauti na biashara ambazo siyo kubwa. Na makosa wanayofanya wafanyabiashara wengi wanaoanza na biashara ndogo, ni kuendelea kuziendesha vile vile hata baada ya biashara kuwa zimeshakua (more…)

UKURASA WA 1330; Uhusiano Wa Kushindwa Na Mafanikio Makubwa…

By | August 22, 2018

Watu wengi hufikiri maisha ni kufanikiwa au kushindwa, na hivyo hutumia kila namna kukwepa kushindwa, wakiamini kama hawashindwi basi wanafanikiwa. Na hakuna uongo mwingine duniani unaozidi huo. Siyo kweli kwamba kama hushindwi basi unafanikiwa. Kama hushindwi maana yake hujaribu mambo makubwa, mambo yaliyo nje ya uwezo wako. Na kama hujaribu (more…)