Author Archives: Dr. Makirita Amani

About Dr. Makirita Amani

Dr. Makirita Amani ni daktari wa binadamu, mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali. Dhumuni lake kubwa kwenye maisha ni KUWASAIDA WATU KUBORESHA MAISHA YAO NA KUFIKIA MAFANIKIO MAKUBWA KUPITIA KAZI ANAZOFANYA. Mawasiliano 0717396253 email makirita@kisimachamaarifa.co.tz

BIASHARA LEO; Sehemu Tatu Pekee Za Kuweka Nguvu Zako Kibiashara…

By | August 28, 2018

Kuna vitu vingi sana ambavyo wafanyabiashara wengi huwa wanafanya. Lakini sehemu kubwa ya vitu hivyo ni kupoteza muda na nguvu pia. Unaweza kuwaona watu wapo ‘bize’ sana, wanakazana kufanya kila kitu, lakini ukifanya tathmini ya yale wanayofanya, unagundua kwamba hayakuwa na umuhimu mkubwa. Kitu chochote unachofanya kwenye biashara yako, lazima (more…)

UKURASA WA 1336; Hata Wanyama Wanakushinda Kwenye Hili…

By | August 28, 2018

Kama umewahi kuwaangalia wanyama jinsi wanavyoishi, basi utakuwa umeiona siri kubwa ya namna asili inavyopeleka mambo yake. Chukua mfano wa simba ambaye amemwona swala anapita, kisha akaanza kumkimbiza swala yule, swala akatimua mbio sana, simba akakazana. Lakini pamoja na jitihada zote, swala anafanikiwa kumponyoka simba. Je unafikiri simba anafanya nini (more…)

BIASHARA LEO; Kumbuka Kuna Mtu Anaweza Kuwa Rahisi Zaidi Yako…

By | August 27, 2018

Wafanyabiashara wavivu na wasiotaka kuweka kazi, huwa wanatumia njia moja kwenye kushindana. Njia hiyo ni kushusha bei na kuuza kwa bei rahisi zaidi ya wengine. Ni njia ambayo kwa haraka inaweza kuongeza wateja na faida, lakini baadaye inakuwa mzingo mkubwa kwa mfanyabiashara. Hii ni kwa sababu, kila mtu anaweza kupunguza (more…)

UKURASA WA 1335; Unajulikana Kwa Kipi?

By | August 27, 2018

Kila mara jina lako linapotajwa kwa watu, ukiwa haupo, kila mtu kuna picha ambayo anaijenga kwenye akili yake kuhusu wewe. Sasa wengi wamekuwa wakijaribu kujenga picha fulani kwa nje, ambayo imekuwa haifanikiwi. Kwa zama hizi za mitandao ya kijamii, kila mtu anaweza kuwa muigizaji wa maisha, akitengeneza picha ya nje (more…)

BIASHARA LEO; Ugonjwa Wa Fursa Mpya Utaua Ndoto Zako Kibiashara…

By | August 26, 2018

Pata picha ya mkulima huyu, Ameambiwa akilima karanga zitamlipa sana, analima shamba na kupanda karanga, wakati karanga zinaanza kuchipua, anaambiwa kuna fursa mpya, kama atalima mahindi, basi atafanikiwa sana, anang’oa karanga na kupanda mahindi. Mahindi yanakua na kabla hayajafikia kuvunwa, anaambiwa fursa kubwa sasa hivi ni maharagwe, anang’oa mahindi hayo (more…)

UKURASA WA 1334; Hili Jukumu Lako Usitegemee Walifanye Wengine…

By | August 26, 2018

Huwa tunapenda sana kukubalika na kila mtu. Tunapenda watu watukubali kwa vile tulivyo na kwa kile tunachofanya. Lakini mara nyingi hilo limekuwa halitokei, siyo watu wote wamekuwa wanatukubali kwa vile tulivyo. Hasa wale ambao tunataka sana watukubali, ndiyo kabisa hawana muda na sisi. Kutegemea wengine wakukubali ndiyo uweze kufanya kitu, (more…)

#TAFAKARI YA LEO; KAMA UNASHANGAZWA, HUJAJIANDAA…

By | August 26, 2018

Hongera sana mwanamafanikio kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo. Ni nafasi bora na ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana. Kwa msingi wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa TATUA, AMUA NA ONGOZA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila (more…)

BIASHARA LEO; Hatua Mbili Za Kishujaa Za Kuchukua Kwenye Biashara Yako.

By | August 25, 2018

Biashara haina tofauti sana na vita, kwa sababu kufanikiwa kwenye biashara kunakutaka uwe shujaa kama walivyo mashujaa wa vita. Biashara nyingi zinazoanzishwa huwa zinakufa kwa sababu wanaoanza biashara hizo wanakuwa hawajajiandaa kisaikolojia kupambana na changamoto mbalimbali za biashara. Wengi hufikiri biashara ni wazo na mtaji, vingine vitakwenda. Lakini biashara ni (more…)