Author Archives: Dr. Makirita Amani

About Dr. Makirita Amani

Dr. Makirita Amani ni daktari wa binadamu, mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali. Dhumuni lake kubwa kwenye maisha ni KUWASAIDA WATU KUBORESHA MAISHA YAO NA KUFIKIA MAFANIKIO MAKUBWA KUPITIA KAZI ANAZOFANYA. Mawasiliano 0717396253 email makirita@kisimachamaarifa.co.tz

UKURASA WA 1281; Kipi Kinaweza Kwenda Vibaya Zaidi?

By | July 4, 2018

Hili ni swali muhimu sana kujiuliza kwenye kila jambo unalofanya, swali ambalo litakuwezesha kujiandaa vizuri na pia kukuondolea hofu. Iko hivi rafiki, mambo mengi mabaya yanaweza kutokea kwenye chochote unachofanya. Ni uwezekano wa mambo haya mabaya kutokea ndiyo unawapa wengi hofu ya kujaribu vitu vipya. Kwa sababu wanafikiria kama mabaya (more…)

UKURASA WA 1280; Uwekezaji Mzuri Wa Muda Wako…

By | July 3, 2018

Wengi husema muda ni fedha, lakini hilo siyo sahihi, muda ni zaidi ya fedha. Na sababu pekee kwamba muda ni zaidi ya fedha, ukishapoteza muda huwezi kuupata tena. Poteza fedha na unaweza kutafuta nyingine, lakini ukipoteza muda, ndiyo umepotea moja kwa moja. Hivyo muda ni zaidi ya fedha, kama unahitaji (more…)

UKURASA WA 1279; Kama Huoni Vitu Hivi Viwili Basi Haupo Hai…

By | July 2, 2018

Maisha yetu ni mkusanyiko wa matukio mbalimbali yanayotokea kwenye kila siku ya maisha yetu. Japokuwa tunaweza kuwa na lengo moja kubwa tunalofanyia kazi, lakini hatutaamka siku moja na kujikuta lengo limetimia. Badala yake kila siku tunapiga hatua kuelekea kwenye lengo lile kubwa. Sasa watu wengi huwa wanasahau maisha ya kila (more…)

#TAFAKARI YA LEO; USISINGIZIE KILICHOTOKEA, BALI HATUA ULIZOCHUKUA…

By | July 2, 2018

“It’s not what happens to you, but how you react to it that matters.” – Epictetus AMKA mwanamafanikio, Amka kwenye siku hii mpya, siku bora na ya kipekee kabisa kwetu. Ni nafasi nyingine nzuri sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana. Msingi wetu wa maisha (more…)

UKURASA WA 1278; Ili Kesho Iwe Bora, Ifurahie Leo…

By | July 1, 2018

Kama kuna ndoto za alinacha, basi ni ile hali ya watu kuishi hovyo leo wakiamini kesho itakuwa bora sana. Ile hali ya watu kuichukulia poa leo, kutokana na changamoto mbalimbali wanazopitia, wakiamini kesho itakuwa nzuri zaidi. Sikiliza rafiki yangu, jinsi unavyoichukulia leo, ndivyo utakavyoichukulia kesho. Kwa sababu hata kama changamoto (more…)

#TAFAKARI YA LEO; USIFANYE MAMBO KUWA MAGUMU ZAIDI YA YALIVYO.

By | July 1, 2018

AMKA mwanamafanikio, Amka kutoka kwenye ndoto za siku moja mambo yatakuwa mazuri na nenda kaweke juhudi kuyafanya mambo kuwa mazuri kweli. Tayari siku mpya, siku bora na ya kipekee ipo kwenye mikono yetu. Ni maamuzi yetu sisi wenyewe tuitumieje siku hii, kama tuitumie kwa kuzalisha na kusonga mbele zaidi. Au (more…)

UKURASA WA 1276; Fanya Kabla Ya Muda Uliokadiria…

By | June 29, 2018

Kuna makadirio mawili ambayo sisi binadamu hatujawahi kupatia kwa asilimia mia moja kwenye kukadiria. Makadirio hayo ni ya muda na fedha. Muda wowote utakaokadiria kufanya kitu, utahitaji zaidi ya hapo. Na kiasi cha fedha unachokadiria kutumia, utatumia zaidi ya hapo. Leo nataka tuzungumzie makadirio ya muda, hasa pale unapotaka kufika (more…)