Author Archives: Dr. Makirita Amani

About Dr. Makirita Amani

Dr. Makirita Amani ni daktari wa binadamu, mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali. Dhumuni lake kubwa kwenye maisha ni KUWASAIDA WATU KUBORESHA MAISHA YAO NA KUFIKIA MAFANIKIO MAKUBWA KUPITIA KAZI ANAZOFANYA. Mawasiliano 0717396253 email makirita@kisimachamaarifa.co.tz

#TAFAKARI YA LEO; KUWA MGUMU KWAKO MWENYEWE…

By | June 29, 2018

Siku mpya, Siku nzuri Na siku ya mafanikio. Hongera sana mwanamafanikio kwa siku hii nyingine ya kipekee sana kwetu. Ni nafasi nzuri kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana. Kwa msingi wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa TATUA, AMUA NA ONGOZA tunakwenda kufanya (more…)

UKURASA WA 1275; Aina Tatu Za Watu Katika Mahusiano Na Utoaji…

By | June 28, 2018

Kuna aina kuu tatu za watu katika mahusiano na utoaji. Na katika aina hizi, kuna moja ambayo watu wanafanikiwa sana wakati nyingine mbili watu wanaishia kuwa kawaida na hata kushindwa kabisa. Aina ya kwanza ni wachukuaji, hawa ni watu ambao wanataka kupata vitu kutoka kwa wengine. Wanapenda kunufaika wao zaidi (more…)

UKURASA WA 1274; Siyo Kosa La Yeyote, Hivyo Chukua Hatua…

By | June 27, 2018

Ni kawaida yetu sisi binadamu, pale mambo yanapokwenda vibaya, tunapopata matokeo tofauti na tuliyotegemea, huwa tunaanza kuangalia nani kasababisha, nani kapelekea mpaka tukapata matokeo hayo. Huwa hatuamini kwamba sisi wenyewe ndiyo tunaweza kuwa tunahusika, kwa sababu tunapenda kupeleka lawama kwa wengine. Leo nataka kukukumbusha hili muhimu sana mwanamafanikio, siyo kosa (more…)

UKURASA WA 1273; Pamoja Na Mipango Mikubwa Uliyonayo, Jikubali Kwanza…

By | June 26, 2018

Kila kitu kina faida na hasara, kila kitu. Faida ya kuwa na malengo na mipango mikubwa kwenye maisha yako ni kwamba kama hutakata tamaa, utafikia malengo na mipango hiyo na maisha yako yatakuwa bora sana. Lakini ipo hasara ya kuwa na malengo na mipango mikubwa, ambayo ni kushindwa. Utashindwa kwenye (more…)

UKURASA WA 1272; Ndiyo Unaweza Kupata Vyote, Na Unapaswa Kupata Vyote…

By | June 25, 2018

Tofauti kubwa ya wale waliofanikiwa sana na wale ambao hawajafanikiwa ni kwenye fikra zao kuhusu kupata vile vitu wanavyotaka. Waliofanikiwa sana wanajua wanaweza kupata vyote, vile wanavyovitaka wanaweza kuvipata na hawajiwekei ukomo. Na hata kama hawapati mwanzoni, hawajiumizi kwa sababu hawajapata, bali wanaangalia wanawezaje kupata vyote, na hapo wanapata njia (more…)

UKURASA WA 1271; Nzuri Si Nzuri Tena…

By | June 24, 2018

Rafiki, kwenye kila eneo la maisha yetu, tunaweza kuvipanga vitu kwenye makundi manne. Bora, nzuri, kawaida na hovyo. Tukitaka tunaweza kuongeza makundi mawili zaidi, bora sana na hovyo kabisa. Lakini napenda tubaki na makundi hayo manne, ili tuweze kupanga vizuri hatua za kuchukua. Hovyo ni kitu ambacho hakipaswi kufanywa kabisa, (more…)

#TAFAKARI YA LEO; USIIPOTEZE LEO…

By | June 24, 2018

“Expecting is the greatest impediment to living. In anticipation of tomorrow, it loses today” – Lucius Annaeus Seneca Hongera mwanamafanikio kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo. Ni nafasi bora na ya kipekee kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana. Kwa msingi wa NIDHAMU, UADILIFU (more…)