Author Archives: Dr. Makirita Amani

About Dr. Makirita Amani

Dr. Makirita Amani ni daktari wa binadamu, mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali. Dhumuni lake kubwa kwenye maisha ni KUWASAIDA WATU KUBORESHA MAISHA YAO NA KUFIKIA MAFANIKIO MAKUBWA KUPITIA KAZI ANAZOFANYA. Mawasiliano 0717396253 email makirita@kisimachamaarifa.co.tz

UKURASA WA 1265; Je Itasaidia?

By | June 18, 2018

Muda una ukomo na nguvu zetu zinakwisha haraka pale tunapozitumia. Hivi ni vitu viwili ambavyo vinatuzuia kufanya kila tunachotaka kufanya. Kwa sababu muda ukishapita na nguvu zikishaisha, hatuwezi kufanya tena, hata kama tunataka kiasi gani. Hivyo kama tunataka kupangilia vizuri maisha yetu, kama tunataka kupiga hatua, basi tunahitaji kutumia vizuri (more…)

#TAFAKARI YA LEO; UTAFANYA AU UTATOA SABABU…

By | June 18, 2018

Siku mpya, siku bora na siku ya kipekee, Ni nafasi nzuri kwetu wanamafanikio kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana. Msingi wetu wa maisha ya mafanikio ni NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA na mwongozo wetu ni TATUA, AMUA NA ONGOZA. Kwa kutumia msingi huu tunakwenda kufanya makubwa leo (more…)

UKURASA WA 1264; Simama Mbele Ya Kioo…

By | June 17, 2018

Unapokuwa na shaka na maisha yako, simama mbele ya kioo na utamwona mtu ambaye anapaswa kuyasimamia maisha yako. Unapokuwa na malalamiko au lawama, simama mbele ya kioo na utamwona mtu anayepaswa kubeba lawama na malalamiko hayo. Unapokuwa hujui nani atakusaidia kutoka hapo ulipo sasa, simama mbele ya kioo na utamwona (more…)

#TAFAKARI YA LEO; HUJAFANYA KITU…

By | June 17, 2018

Amka mwanamafanikio, Amka leo uende ukafanye kile ulichosema utafanya leo. Amka leo uende ukakamilishe kile ulichoanza lakini hukumaliza. Amka leo uende ukaanze kufanya kile ambacho umekuwa unasema utafanya. Amka sasa, na amka ukiwa na hamasa ya kwenda kufanyia kazi ndoto kubwa ya maisha yako. Ni siku mpya, siku nzuri na (more…)

UKURASA WA 1263; Usisimamie Vitu, Bali Dhibiti Vitu, Tawala.

By | June 16, 2018

Wanachofanya wengi, ni kusimamia vitu, kuvitumia kwa njia ambayo inafaa. Angalia watu wanachofanya kwenye biashara zao, wanachofanya kwenye muda wao, wanachofanya kwenye fedha zao na kwenye mambo mengine wanayofanya. Wanasimamia, wanafanya kile ambacho kinafaa kufanywa, kwa namba ambayo wamezoea kufanya. Lakini hivi sivyo watu wenye mafanikio makubwa wanavyofanya. Wenye mafanikio (more…)

#TAFAKARI YA LEO; KIPAJI PEKEE HAKITOSHI…

By | June 16, 2018

“Talent is insignificant. I know a lot of talented ruins. Beyond talent lie all the usual words: discipline, love, luck, but, most of all, endurance.” — James Baldwin Amka mwanamafanikio, Amka siyo tu kutoka kitandani, Bali Amka kutoka kwenye ndoto na nenda kaweke juhudi. Amka kutoka kwenye kuahirisha mambo na (more…)

UKURASA WA 1262; Siyo Ugumu Wa Vitu, Bali Ulaini Wako…

By | June 15, 2018

Kwenye safari ya mafanikio, utakutana na kila aina ya ugumu, vikwazo na changamoto. Utapanga vizuri na kujua kila hatua ya kuchukua, lakini utakutana na ugumu, ambao utakufanya uone hakuna namna nyingine. Kinachowatofautisha wale wanaofanikiwa na wale wanaoshindwa, siyo magumu wanayokutana nayo, bali wao wenyewe. Kwa kuwa kila mtu anakutana na (more…)

#TAFAKARI YA LEO; KUBALI KUONEKANA MJINGA NA MPUMBAVU…

By | June 15, 2018

“If you want to improve, be content to be thought foolish and stupid” – Epictetus Siku mpya, siku bora na siku ya kipekee sana kwetu. Hii ni nafasi nzuri kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana. Kwa msingi wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo (more…)

UKURASA WA 1261; Jinsi Ya Kuchagua Watu Wa Kujihusisha Nao…

By | June 14, 2018

Watu ni changamoto kubwa kwenye mafanikio yako, Utahitaji watu wa kukusaidia kama wafanyakazi, lakini wengi watakusumbua. Utahitaji watu wa kushirikiana nao kwenye yale unayofanya, Lakini wengi watakuangusha. Utahitaji watu wawe wateja wa kile unachofanya au kuuza, Lakini wengi hawatakuja kama unavyotaka waje. Utafika hatua na kupoteza imani na watu, na (more…)