Author Archives: Dr. Makirita Amani

About Dr. Makirita Amani

Dr. Makirita Amani ni daktari wa binadamu, mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali. Dhumuni lake kubwa kwenye maisha ni KUWASAIDA WATU KUBORESHA MAISHA YAO NA KUFIKIA MAFANIKIO MAKUBWA KUPITIA KAZI ANAZOFANYA. Mawasiliano 0717396253 email makirita@kisimachamaarifa.co.tz

UKURASA WA 1236; Kelele Za Dunia…

By | May 20, 2018

Tunaishi kipindi cha kipekee, kipindi bora kabisa kuwahi kutokea duniani. Kipindi ambacho, mtu anaweza kujifunza chochote, bila ya kuwa na kitu au mtu wa kumzuia. Maarifa na taarifa ni nyingi na zinapatikana kwa urahisi, kwa yeyote anayezitaka. Lakini pamoja na wingi huu wa taarifa na urahisi wa kupatikana kwake, ni (more…)

UKURASA WA 1235; Fursa Ambayo Haitajirudia Tena….

By | May 19, 2018

Zipo kauli za kitapeli, kauli ambazo zinatumika kuwahadaa watu, wachukue hatua haraka bila hata ya kufikiri kwa kina. Moja ya kauli hizo ni hii ya fursa ambayo haitajirudia tena. Watu wakishasikia kauli hiyo wanakimbilia kuchukua hatua, bila hata ya kuchunguza kwa kina. Kinachotokea baadaye inakuwa hasara kubwa kwao, wanajikuta wameingia (more…)

UKURASA WA 1234; Kwa Nini Mafanikio Yanaendelea Kuwa Siri…

By | May 18, 2018

Ukiona kitabu kimeandikwa siri kumi za mafanikio, utavutiwa kukinunua na kukisoma. Lakini ndani ya kitabu hicho, hutakutana na vitu vipya ambavyo huvijui. Zile unaambiwa ni siri, utakuta ni mambo yale yale ambayo unayafahamu. Kuwa na maono makubwa, kujitoa kufanya kazi, kuwa na nidhamu, kujifunza na kushirikiana na wengine ni mambo (more…)

UKURASA WA 1233; Njia Mbaya Ya Kuondokana Na Maumivu…

By | May 17, 2018

Maumivu ni sehemu ya maisha, na kama falsafa nyingi zinavyotufundisha, maumivu tunatembea na kukutana nayo kila siku. Kinachotufanya tukue na kufanikiwa ni maumivu tunayokutana nayo. Watu wamekuwa wakitumia njia mbalimbali kutaka kuondokana na maumivu wanayokutana nayo. Lakini njia rahisi ambayo watu wamekuwa wanakazana nayo, imekuwa inazidisha maumivu badala ya kuyaondoa. (more…)

UKURASA WA 1232; Picha Ni Muhimu Zaidi…

By | May 16, 2018

Ukitaka kueleweka vizuri, ukitaka kushawishi watu wachukue hatua, ukitaka ujumbe wako ufike vizuri, picha ni muhimu zaidi kuliko maneno. Unaweza kutoa maelezo yenye kuonesha data na kile ambacho ni kweli, lakini watu hawapendi kusikia tu maelezo na kusikia ukweli. Watu wanataka kitu kitakachowahamasisha, kitakachowafanya wajione ni sehemu ya kile wanachosikiliza. (more…)

UKURASA WA 1231; Zawadi Na Mchakato Wa Kuelekea Kwenye Zawadi…

By | May 15, 2018

Habari za watu waliofanikiwa, walioanzia chini na kuweza kupanda mpaka juu sana ni habari nzuri, zinazovutia na zinazosisimua. Ni habari rahisi kufuatilia na kuelewa, alianzia hapa sifuri na sasa ni shujaa. Ni habari zenye matumaini, kwamba huyu ambaye alianzia chini, bila ya chochote kwenye mazingira ambayo sisi pia tupo, ameweza (more…)