Author Archives: Dr. Makirita Amani

About Dr. Makirita Amani

Dr. Makirita Amani ni daktari wa binadamu, mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali. Dhumuni lake kubwa kwenye maisha ni KUWASAIDA WATU KUBORESHA MAISHA YAO NA KUFIKIA MAFANIKIO MAKUBWA KUPITIA KAZI ANAZOFANYA. Mawasiliano 0717396253 email makirita@kisimachamaarifa.co.tz

UKURASA WA 1155; Dawa Nzuri Kwa Wale Wanaokukatisha Tamaa…

By | February 28, 2018

Ukitaka usisumbuane na watu, wewe fanya mambo ya kawaida kabisa. Usipange kufanya makubwa na wala usijisumbue kupiga hatua kubwa. Hapo utakuwa na marafiki wengi, lakini wote ni wale ambao hakuna hatua kubwa wanayopiga kwenye maisha yao. Lakini pale utakapoanza kupanga kupiga hatua kubwa, pale utakapoanza kufanya makubwa, jua utaamsha kila (more…)

#TAFAKARI YA LEO; ULICHONACHO SASA, NDIYO UNACHOHITAJI KWA SASA…

By | February 28, 2018

Whatever the universal nature assigns to any man at any time is for the good of that man at that time. – Marcus Aurelius Hongera mwanamafanikio kwa siku hii mpya kwetu. Ni nafasi nzuri na ya kipekee kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana. Msingi wetu (more…)

UKURASA WA 1154; Tengeneza Vitu…

By | February 27, 2018

Kuna mtu mmoja amewahi kunukuliwa akisema duniani kuna makundi matatu ya watu, wale ambao wanafanya vitu vitokee, wale ambao wanashangaa vitu vinavyotokea na wale ambao hawajui nini kinachotokea. Unahitaji kuwa kwenye kundi la kwanza kama unataka kuwa na mafanikio kwenye maisha yako, kuwa kwenye kundi la wanaofanya vitu vitokee, kuwa (more…)

#TAFAKARI YA LEO; KILA BAYA NI MATOKEO YA USHIRIKIANO…

By | February 27, 2018

Every sin is the result of a collaboration. – Lucius Annaeus Seneca. Hongera mwanamafanikio kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo. Ni nafasi bora na ya kipekee kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana. Msingi wetu wa maisha ya mafanikio ni NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA (more…)

DARASA LA JUMAPILI; JINSI YA KUFIKIRI KWA KINA NA KUFANYA MAAMUZI SAHIHI.

By | February 26, 2018

DARASA LA JUMAPILI. MADA; JINSI YA KUFIKIRI KWA KINA NA KUFANYA MAAMUZI SAHIHI. Habari wanamafanikio? Jumapili hii kwenye muda wetu wa darasa, kuanzia saa 12 jioni mpaka saa 2 usiku, tutakuwa na darasa la JINSI YA KUFIKIRI KWA KINA NA KUFANYA MAAMUZI SAHIHI. Hili ni darasa muhimu kwa zama tunazoishi (more…)

DARASA LA JUMAPILI; UWEKEZAJI KWENYE SOKO LA HISA

By | February 26, 2018

DARASA LA JUMAPILI. MADA; UWEKEZAJI KWENYE SOKO LA HISA. Karibuni wanamafanikio kwenye darasa letu la jumapili ya leo ambapo tunakwenda kujifunza na kujadili kwa kina kuhusu uwekezaji kwenye soko la hisa. Hii ni moja ya njia muhimu za uwekezaji ambayo wengi wamekuwa wanashindwa kuitumia kutokana na kukosa maarifa sahihi ya (more…)

BIASHARA LEO; Vitu Ambavyo Havilipi Moja Kwa Moja Kwenye Biashara Yako.

By | February 26, 2018

Kuna tabia moja ya waajiriwa ambayo nimekuwa naona inawarudisha nyuma sana kwenye kupiga hatua kwenye kazi hiyo. Tabia hiyo ni kufanya yale ambayo wanalipwa tu. Kama mtu halipwi moja kwa moja kwa kufanya kitu, basi hakifanyi. Na utawasikia kabisa wakijiambia kwani nalipwa? Tabia hii nimekuwa naiona pia kwa wafanyabiashara ambao (more…)

UKURASA WA 1153; Una Mpango Wa Kucheza Kwa Muda Mrefu Kiasi Gani?

By | February 26, 2018

Kama maisha ni mchezo, basi kuna jambo muhimu sana unalopaswa kulijua kabla ya kuingia kwenye mchezo huu. Na jambo hilo ni una mpango wa kucheza kwa muda mrefu kiasi gani? Hili ni muhimu kwa sababu, usipokuwa makini kwenye muda, utajikuta unafupisha mchezo wako mwenyewe. Kwa mfano kwenye mchezo wa riadha, (more…)

UKURASA WA 1152; Ongea Na Watu….

By | February 25, 2018

Wahenga walisema kama unataka kupata ya watu, basi ongea na watu. Hii ni kauli yenye nguvu sana kwenye maisha ya mafanikio, kwa sababu huwezi kufanikiwa wewe mwenyewe. Chochote unachotaka kwenye maisha yako, kinatoka kwa wengine. Na ili uweze kukipata, unahitaji kuongea na watu. Dunia nzima inazunguka kwenye kitu kimoja, kuongea (more…)