Author Archives: Dr. Makirita Amani

About Dr. Makirita Amani

Dr. Makirita Amani ni daktari wa binadamu, mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali. Dhumuni lake kubwa kwenye maisha ni KUWASAIDA WATU KUBORESHA MAISHA YAO NA KUFIKIA MAFANIKIO MAKUBWA KUPITIA KAZI ANAZOFANYA. Mawasiliano 0717396253 email makirita@kisimachamaarifa.co.tz

UKURASA WA 1112; Muunganiko Na Wengine, Utengano Na Wewe Mwenyewe…

By | January 16, 2018

Zama za taarifa, zama za teknolojia ambazo tumeungana kwa masaa 24. Sasa hizi, kwa masaa 24 ya siku unaweza kupata taarifa yoyote unayotaka, unaweza kuwasiliana na yeyote unayetaka. Muunganiko huu unaweza kuwa kitu kizuri, na unaweza kiwa kitu kibaya pia, kama hutaweza kuutumia vizuri. Kwa mfano, kadiri watu wanavyounganika na (more…)

UKURASA WA 1111; Tofauti Ya Washindi Na Wanaoshindwa Kwenye Ndoto…

By | January 15, 2018

Kila mtu huwa anakuwa na ndoto fulani. Tena ndoto ambazo ni kubwa na za ajabu na wengi huwa hawazisemi wazi wazi kwa sababu wanaogopa wengine watawacheka au kuwakatisha tamaa. Ungekuwa na uwezo wa kusoma ndoto za watu ndani ya akili zao, ungeona jinsi ambavyo dunia imejaa utajiri wa kutisha. Ungeona (more…)

UKURASA WA 1110; Sio Wewe Unataka Nini, Bali Dunia Inataka Nini…

By | January 14, 2018

Aliyekuwa raisi wa Marekani, John F. Kennedy aliwahi kunukuliwa akisema, usiulize nchi yako inakufanyia nini, bali jiulize wewe unaifanyia nini nchi yako. Ni kauli muhimu sana kwenye uwajibikaji na uzalendo, kwa sababu matendo ya kila mtu ndiyo yanaishia kuwa matendo ya taifa. Mimi nakuletea kauli kama hii, lakini kwa upande (more…)

UKURASA WA 1109; Kuchukua Hatua Ni Bora Kuliko Kuwa Sahihi…

By | January 13, 2018

Watu wanajifunza sana, watu wanakutana na vitu vipya, ambavyo vinaweza kubadili sana maisha yao, iwapo watachukua hatua. Lakini wanasubiri, wanasubiri kwa sababu hawajapata uhakika wa kile wanachokwenda kufanya. Hawajajua kama ni hatua sahihi kuchukua. Wanajiona hawajakamilika, hivyo wanasubiri. Kwa namna hii, wanajikuta hawachukui hatua yoyote, au wanapokuja kufikia hatua ya (more…)

UKURASA WA 1108; Maumivu Ni Sehemu Ya Mchezo…

By | January 12, 2018

Huwa tunapenda kufurahia michezo mbalimbali, ambapo wachezaji wanacheza na sisi tunaburudika. Lakini katika kila mchezo, watu wanaumia. Iwe ni mchezo wa ngumi, wachezaji wanapigana na wanaumia. Hata mchezo wa mpira wa miguu au mikono, wachezaji wamekuwa wanaumia uwanjani. Pamoja na maumivu hayo, wachezaji hawaachi kucheza. Watauguza majeraha na kurudi tena (more…)

UKURASA WA 1107; Kinachoendelea Kuchochea Hasira Zako Ni Hichi…

By | January 11, 2018

Kila mtu huwa anapata hasira, lakini kinachowatofautisha wale wanaoonekana wana hasira sana na ambao hawana hasira, ni namna gani wanaichukulia na kuishughulikia hasira wanayokuwa nayo. Watu kwa kujua au kutokujua, huwa wanatuudhi au kufanya mambo ambayo hatukutegemea wafanye. Hili huleta hasira kwa kila mtu, lakini wapo ambao hasira zao zinaishia (more…)

UKURASA WA 1106; Wale Unaowavumilia, Ndiyo Wanaokutengeneza…

By | January 10, 2018

Unapokutana na marafiki au jamaa zako, huwa mijadala yenu imetawaliwa na nini? Kwa wengi, mijadala wanayokuwa nayo wanapokutana imegawanyika kwenye makundi mawili, kutoroka na kujisumbua. Mijadala ya kutoroka ni ile ya kulalamika na kulaumu, hii ni mijadala inayotufanya tuone kwamba sisi hatuna tatizo bali wengine ndiyo wanatuletea matatizo. Kwa mijadala (more…)

UKURASA WA 1105; Acha Kukazana Kuibadili Dunia, Nenda Nyumbani Kaipende Familia Yako.

By | January 9, 2018

Karibu kila mtu huwa ana ndoto yake kubwa ya kuibadili dunia kwenye eneo fulani. Labda ni mwalimu ana ndoto ya kuibadili dunia kupitia maarifa anayotoa kwa wengine. Au ni daktari anataka kuibadili dunia kwa kuboresha maisha ya wengine. Au ni injinia anataka kuibadili dunia kwa kuja na ugunduzi wa kitofauti (more…)

UKURASA WA 1104; Ufanisi Kwenye Muda Ni Ubora Na Siyo Wingi…

By | January 8, 2018

Ipo dhana kwamba watu wenye ufanisi mkubwa, watu wanaozalisha kwa kiasi kikubwa ni watu ambao wapo ‘bize’ muda wote, watu ambao wanaweza kukamilisha mambo mengi zaidi, watu ambao wanaweza kufanya mambo mengi kwa wakati mmoja. Yote hayo ni uongo. Yote hayo yanawazuia wengi kufanya yale muhimu na kuyafanya vizuri na (more…)