Author Archives: Dr. Makirita Amani

About Dr. Makirita Amani

Dr. Makirita Amani ni daktari wa binadamu, mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali. Dhumuni lake kubwa kwenye maisha ni KUWASAIDA WATU KUBORESHA MAISHA YAO NA KUFIKIA MAFANIKIO MAKUBWA KUPITIA KAZI ANAZOFANYA. Mawasiliano 0717396253 email makirita@kisimachamaarifa.co.tz

UKURASA WA 1092; Badili Njia, Usibadili Maono…

By | December 27, 2017

Moja ya vitu muhimu kwenye kufikia mafanikio makubwa ni maono. Kama hujui unapokwenda, njia yoyote itakufikisha popote na kwa kuwa hujui unapokwenda, hutajua hata kama umefika. Hivyo lazima maono yawepo, na maono siyo kitu cha kubadili kila mara kama mtu unavyojisikia, badala yake ni kitu ambacho unachagua na kukifanyia kazi (more…)

UKURASA WA 1091; Kutamani, Kutaka Na Kujitoa…

By | December 26, 2017

Kila mtu anaweza kutamani, Unamwona mtu ana kitu fulani ambacho na wewe ungependa kuwa nacho, unakitamani, na kufikiria na wewe pia unaweza kuwa nacho. Hii ni hatua ya kwanza kabisa kwenye mafanikio na hata mipango yetu. Lazima kuwe na kitu cha kutufanya tuone tunataka zaidi ya tulichonacho sasa. Wapo watu (more…)

UKURASA WA 1090; Kabla Ya Kuzalisha, Maandalizi Yanahitajika…

By | December 25, 2017

Hakuna kitu ambacho huwa kinanishangaza kama uharaka wa watu kutaka mafanikio bila ya kuwa na subira. Watu hufikiri kwamba kwa sababu wameshajua nini wanataka, kwa sababu wameshaweka malengo, kwa sababu wameshakuwa chanya na wanaweka juhudi, basi wanapaswa kupata matokeo hapo hapo. Lakini hebu tuiangalie asili katika uzalishaji. Hakuna kiumbe ambacho (more…)

UKURASA WA 1089; Tamaa Ikishawaka, Jua Unapoteza…

By | December 24, 2017

Kama ipo njia ya uhakika ya kushindwa na kupoteza kwenye maamuzi yoyote ambayo mtu anafanya, ni kuendeshwa na tamaa. Yaani tamaa ikishawaka, basi lazima mtu apoteze, ni lazima. Anaweza asipoteze kwa wakati huo, akapata kile alichotamani, lakini hilo likamkosesha vitu vingi na vizuri vya baadaye. Tamaa inapokuwa juu, mtu anashindwa (more…)

UKURASA WA 1088; Unajificha Wapi?

By | December 23, 2017

Nataka kuanza biashara lakini bado sijajiandaa vya kutosha…. Nasubiri mpaka niwe tayari ndiyo nianze kufanya… Nataka kuandika lakini bado sijajifunza vya kutosha… Nataka kuboresha zaidi kazi zangu lakini kwa sasa bado sijakamilika… Zote hizo ni dalili za kujificha. Unataka kufanya kitu, lakini unajificha kwenye sababu fulani, ambazo zinaweza kuwa kweli (more…)

UKURASA WA 1087; Kigeugeu Cha Watu Inapokuja Kwenye Mafanikio Yako…

By | December 22, 2017

Inapokuja kwenye mafanikio yako, kuna wakati inakuwa vigumu kumwamini mtu yeyote kutokana na tabia ya kigeugeu ambayo watu wengi wanayo. Kwa hakika watu wanapenda kuhusishwa na vitu vinavyofanikiwa, na hawapendi kuwa sehemu ya vitu vinavyoshindwa. Mtu mmoja aliwahi kusema kwamba mafanikio yana wazazi wengi, ila kushindwa ni yatima. Ukifanikiwa kila (more…)

UKURASA WA 1086; Kazi Na Biashara Ambayo Itaendelea Kulipa Zaidi Na Zaidi…

By | December 21, 2017

Changamoto kubwa ya zama hizi ni kwamba karibu kila kazi ina watu wengi wanaoweza kuifanya kuliko wanaohitajika, hivyo malipo yanakuwa madogo kwa sababu ukikataa kufanya, wapo wengi ambao wapo tayari kufanya kwa malipo kidogo. Kwenye biashara pia, hali ni hiyo hiyo, karibu kila biashara inafanywa na kila mtu, na watu (more…)

UKURASA WA 1085; Kuwa Tofauti Kuwa Bora Zaidi, Na Siyo Kuwa Tu Tofauti…

By | December 20, 2017

Ukweli ni kwamba, moja ya njia rahisi za kukubali kushindwa, ni kufanya kile ambacho kila mtu anafanya, kwa namna ambavyo kila mtu anafanya. Hili halikutofautishi kwa namna yoyote ile, badala yake linakuletea msongo, kwa sababu unakuwa katikati ya kelele za wengi. Hivyo ni muhimu kuwa tofauti kama unataka kujitengenezea kitu (more…)