Author Archives: Dr. Makirita Amani

About Dr. Makirita Amani

Dr. Makirita Amani ni daktari wa binadamu, mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali. Dhumuni lake kubwa kwenye maisha ni KUWASAIDA WATU KUBORESHA MAISHA YAO NA KUFIKIA MAFANIKIO MAKUBWA KUPITIA KAZI ANAZOFANYA. Mawasiliano 0717396253 email makirita@kisimachamaarifa.co.tz

UKURASA WA 1098; Kujionesha Na Kuonekana, Namna Unavyopoteza Nguvu Zako Mwenyewe.

By | January 2, 2018

Ni hitaji la ndani la kila binadamu kupenda kuthaminiwa, kuonekana ni wa muhimu kwa chochote kile ambacho anakifanya. Huu ni msukumo uliopo nyuma ya maamuzi ambayo wengi wanafanya, kuanzia mavazi wanayovaa, kazi na biashara wanazofanya, mali wanazomiliki na hata michango wanayotoa kwa wengine. Hakuna ubaya wowote kwenye hilo, ila pale (more…)

UKURASA WA 1097; Miaka Mitatu Ya Kurasa Na Nguvu Ya Kufanyia Kazi Wazo…

By | January 1, 2018

Siku kama ya leo, miaka mitatu iliyopita, nilipata wazo hili la kuandika makala fupi kila siku, na kuzipa jina la KURASA ZA MAISHA YA MAFANIKIO. Kabla ya makala hizi za kurasa, nilikuwa tayari nimejenga utaratibu wa kujiandikia kila siku, lakini zilikuwa makala ambazo ni kwa ajili ya mada maalumu. Labda (more…)

UKURASA WA 1096; Kufuata Ramani Na Kutengeneza Ramani…

By | December 31, 2017

Kwenye maisha, zipo ramani ambazo tayari zimeshatengenezwa, ramani za kila eneo la maisha yetu. Kila kitu cha kufanya ili mtu aweze kufika hatua fulani ya maisha yake. Ramani hizi tumekuwa tunafundishwa tangu tukiwa watoto na kuhakikisha tunazielewa ili mambo yetu yaende vizuri. Japokuwa ramani ni nzuri, hasa kwa mtu asiyejua (more…)

UKURASA WA 1095; Hatari Iliyopo Kwenye Mtazamo Wa Kusaka Fursa…

By | December 30, 2017

Kama kuna neno moja ambalo limetumika vibaya mpaka hata kupoteza kabisa maana yake, ni neno fursa. Kila siku watu wapo ‘bize’ kutafuta na kukimbizana na fursa. Na kwa namna fursa hizi zinavyoonekana na kuchukuliwa, zinavutia na kutamanisha mno. Mtu anavutiwa kufikiri kwamba kama asipoingia kwenye fursa fulani basi hawezi kufanikiwa. (more…)

#TAFAKARI YA LEO; MAANA YA MAISHA KWA MWEREVU NA MPUMBAVU….

By | December 29, 2017

To the wise, life is a problem; to the fool, a solution. – Marcus Aurelius Hongera sana mwanamafanikio kwa siku hii nzuri na ya kipekee. Ni nafasi bora kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana. Msingi wetu wa maisha ya mafanikio ni NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA (more…)

UKURASA WA 1094; Unachagua Kukuza Nini Kwenye Maisha Yako?

By | December 29, 2017

Kitu kimoja ambacho watu huwa hawaelewi haraka kwenye maisha ni kwamba, kila mtu anayatengeneza mazingira ya maisha yake, na kuna vitu ambavyo mtu anachagua kuvikuza kwa kujua au kutokujua. Ukweli ni kwamba kwenye dunia tunayoishi ni vigumu sana kuujua ukweli. Kila mtu anaiangalia dunia kupitia miwani yenye rangi fulani. Rangi (more…)

UKURASA WA 1093; Fursa Iliyopo Ndani Ya Tabia Ya Kuahirisha Mambo…

By | December 28, 2017

Moja ya tabia ambazo ni sumu kwa mafanikio ya wengi ni tabia ya kuahirisha mambo. Mtu unakuwa na hamasa kubwa ya kupiga hatua kwenye maisha yako, unaweka malengo na mipango na unajua kabisa nini unapaswa kufanya ili kufika pale unapotaka kufika. Lakini changamoto inakuja pale unapofika wakati wa kufanya. Hapa (more…)