Author Archives: Dr. Makirita Amani

About Dr. Makirita Amani

Dr. Makirita Amani ni daktari wa binadamu, mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali. Dhumuni lake kubwa kwenye maisha ni KUWASAIDA WATU KUBORESHA MAISHA YAO NA KUFIKIA MAFANIKIO MAKUBWA KUPITIA KAZI ANAZOFANYA. Mawasiliano 0717396253 email makirita@kisimachamaarifa.co.tz

#KURASA_KUMI ZA KITABU LEO; Chunguza Vyanzo Vya Mawazo Na Imani Ulizonazo.

By | November 9, 2017

KITABU; How to Think Like Leonardo da Vinci / Michael J. Gelb UKURASA; 77 – 86 Kila mtu pale alipo, ana fikra ambazo zinatawala akili yake na pia zinatengeneza imani yake. Kile unachoamini sasa hakikutoka tu hewani, bali kiliingia kwa njia mbalimbali. Vipo vyanzo vikuu vitatu ya taarifa na maarifa (more…)

UKURASA WA 1044; Tengeneza Siku Ya Mafanikio Na Iishi Kila Siku…

By | November 9, 2017

Watu wengi wanapoyaangalia mafanikio, huwa wanaangalia vitu vikubwa sana. Huwa wanaangalia nyakati ambazo mtu ameweza kupiga hatua kubwa sana kutoka kwenye hatua ndogo. Lakini mafanikio huwa hayapo hivyo. Kwa mfano, hadithi nyingi za mafanikio huwa zinakupa kabla na sasa, au kama inavyotumika BEFORE na AFTER. Yaani mtu alikuwa hapa, na (more…)

#TAFAKARI YA LEO; NJIA YA KUWAJUA WATU VIZURI….

By | November 9, 2017

To understand the true quality of people, you must look into their minds, and examine their pursuits and aversions. – Marcus Aurelius Hongera mwanamafanikio kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo. Ni nafasi bora na ya kipekee kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana. Msingi (more…)

UKURASA WA 1043; Kufanya Kazi Kwa Nguvu, Akili, Kujitoa Na Kuamini Unachofanya.

By | November 8, 2017

Kuna watu wanasema usifanye kazi kwa nguvu, fanya kazi kwa akili. Hawa ni wavivu ambao wanafikiri kuna njia rahisi ya mafanikio. Hata daktari bingwa wa upasuaji wa ubongo na mishipa ya fahamu, mtu ambaye anakuwa amekaa darasani miaka mingi mpaka kufikia hatua hiyo, anatumia nguvu anapofanya upasuaji. Kwa sababu upasuaji (more…)

#TAFAKARI YA LEO; INACHUKUA MUDA KUJIFUNZA KUACHA…

By | November 8, 2017

The mind unlearns with difficulty what it has long learned. – Lucius Annaeus Seneca Habari za asubuhi ya leo mwanamafanikio? Hongera kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo. Ni nafasi bora na ya kipekee kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana. Msingi wetu wa maisha (more…)

#KURASA_KUMI ZA KITABU LEO; Jifunze kutokana na Uzoefu unaopitia.

By | November 7, 2017

KITABU; How to Think Like Leonardo da Vinci / Michael J. Gelb UKURASA 67 – 76. Moja ya misingi ambayo ilimwezesha Leonardo kufanya makubwa ni kuwa tayari kujifunza kupitia uzoefu anbao alikuwa anapitia. Leonardo aliishi kipindi ambacho watu walikuwa wanaamini hakuna elimu mpya, kila kitu kimeshajulikana. Hivyo hakuna aliyehoji wala (more…)

UKURASA WA 1042; Kufanya Na Kutaka Kufanya…

By | November 7, 2017

Kuna watu wanafanya biashara, na kuna watu wanataka kufanya biashara. Kuna watu ni wakulima, na kuna watu wanataka kuwa wakulima. Kuna watu ni waandishi, na kuna watu ambao wanataka kuwa waandishi. Sheria ya kwanza ya mwendo ya Mwanasayansi Isaack Newton inasema kwamba kila kitu kitaendelea kuwa pale kilipo, iwe ni (more…)

#KURASA_KUMI ZA KITABU LEO; Jinsi ya kufufua na kuchochea udadisi. KITABU; How to Think Like Leonardo da Vinci / Michael J. Gelb UKURASA; 57 – 66. Watoto wadogo huwa wanakuwa na maswali mengi sana. Huwa wanahoji na kudadisi kila kitu. Lakini kadiri wanavyokua, ndivyo udadisi wao unavyopungua. Maswali yanaisha na wanakubaliana na majibu wanayoyapata au kile wengine amekubali. Hali hii wanakuwa wamejifunza, kutokana na majibu waliyopokea wakati wa udadisi na maswali mengi. Huenda ni kukatishwa tamaa au kukemewa na kuambiwa waache usumbufu. Kila mtu anaweza kufufua na kuchochea udadisi ambao upo ndani yake. Na njia ya kufanya hivyo ni kuanza kuhoji maswali. Kuanza kuhoji kila kitu na kuchunguza kwa kina. Badala ya kukubaliana na majibu rahisi yanayotolewa na kukubaliwa na wengine, unahitaji kuhoji zaidi. Zoezi hili kinakuwa bora zaid kama ukiwa na kijitabu cha kuandika maswai uliyonayo. Hapa unaandika yale maswali unayojiuliza au kudadisi chochote unachokutana nacho. Leonardo da Vinci anasifika kwa kuwa na vijitabu vingi ambavyo alikuwa akiandika maswali yake. Kila alichohoji na kudadisi alikiandika, na hili lilimwezesha kupiga hatua zaidi. Njia bora zaidi ya kuhakikisha unahoji maswali muhimu ya udadisi ni zoezi la maswali 100. Hapa unajihoji na kuandika maswali 100 muhimu zaid kwako. Maswali haya hayahitaji kuwa na umaalumu wowote, bali ni kuihoji akili yako mpaka itoe maswali 100. Zoezi hili litakuwezesha wewe kujijua kwa undani na kujua kile hasa unachoamini na hata kujali pia. Mara zote kuwana kijitabu, na mara zote hoji na dadisi, utajifunza mengi sana. Rafiki na Kocha wako, Dr. Makirita Amani, www.amkamtanzania.com/kurasa

By | November 6, 2017

KITABU; How to Think Like Leonardo da Vinci / Michael J. Gelb UKURASA; 57 – 66. Watoto wadogo huwa wanakuwa na maswali mengi sana. Huwa wanahoji na kudadisi kila kitu. Lakini kadiri wanavyokua, ndivyo udadisi wao unavyopungua. Maswali yanaisha na wanakubaliana na majibu wanayoyapata au kile wengine amekubali. Hali hii (more…)