Author Archives: Dr. Makirita Amani

About Dr. Makirita Amani

Dr. Makirita Amani ni daktari wa binadamu, mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali. Dhumuni lake kubwa kwenye maisha ni KUWASAIDA WATU KUBORESHA MAISHA YAO NA KUFIKIA MAFANIKIO MAKUBWA KUPITIA KAZI ANAZOFANYA. Mawasiliano 0717396253 email makirita@kisimachamaarifa.co.tz

UKURASA WA 691; Imani Inayowatenganisha Watu Na Utajiri…

By | November 21, 2016

Kuna imani ambazo zinakaribisha fedha na hivyo kuleta utajiri na pia kuna imani ambazo zinafukuza kabisa fedha. Ndani ya jamii zetu, imani kubwa zilizotawala ni zile za kufukuza fedha. Moja ya imani ambayo inafukuza fedha na kuwafanya wengi kubaki kwenye umasikini ni imani ya UHABA. Jamii na watu wanaokuzunguka wanakufanya (more…)

UKURASA WA 690; Kubishana Ni Kupoteza Muda Wako…

By | November 20, 2016

Kuna baadhi ya mambo huwa tunajikuta tunayafanya, lakini hatujui ni kwa jinsi gani yanatupotezea muda wetu. Na moja ya mambo hayo ni kubishana. Unajikuta unaona ni sahihi kabisa kwako kubishana, kwa sababu wewe ndiyo uko sahihi na yule mwingine amekosea au  hajui. Si ndiyo, wewe shabiki wa yangu upo sahihi (more…)

💥 #TAFAKARI YA LEO; MCHAKATO VS TUKIO…

By | November 19, 2016

Hongera rafiki yangu kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo, Ni nafasi ya kipekee kwetu kwenda kuweka juhudi kwenye kile tulichochagua kufanya. Tumia muda wako wa leo vizuri rafiki, kwa sababu ukishapita, huwezi kuupata tena. Asubuhi ya leo tutafakari kuhusu MCHAKATO na TUKIO. Vitu vingi ambavyo tunaviona kwa wengine (more…)

UKURASA WA 689; Hofu Mbili Zinazowazuia Wengi Kufanikiwa, Na Jinsi Ya Kuzishinda.

By | November 19, 2016

Hofu ndiyo sumu inayoua mafanikio zaidi ya kitu kingine chochote. Hofu imewazuia watu wengi kufanyia kazi ndoto za maisha yao. Hofu imewatisha watu kuendelea hata baada ya kuwa wameanza. Na hofu imekuwa inatumiwa na watu kuwarudisha wengine nyuma. Kama huamini hili hebu jiulize wewe mwenyewe, kama usingekuwa na hofu yoyote (more…)

💥 #TAFAKARI YA LEO; STOP DIGGING…

By | November 18, 2016

Hongera rafiki yangu kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo. Ni nafasi nyingine nzuri ya kwenda kuweka juhudi zaidi kwenye kile ambacho unafanya. Rafiki, tumia nafasi ya leo vizuri, huwezi kuipata tena kwenye maisha yako. Asubuhi ya leo tutafakari kuhush KUACHA KUCHIMBA… Ukishagundua tayari upo kwenye shimo, hatua ya (more…)

UKURASA WA 688; Unapata Kile Unachovumilia…

By | November 18, 2016

Wote tunajua ya kwamba, kwenye maisha tunapata kile ambacho tunakitaka. Kile ambacho tunakifikiria muda mrefu kwenye akili zetu, na kukitafuta kwa bidii ndiyo tunachopata kwenye maisha yetu. Tunapata kile ambacho kimetawala akili zetu muda mwingi kwa sababu akili zetu zina uwezo mkubwa wa kuumba na kutusogeza karibu na mazingira yenye (more…)

UKURASA WA 687; Mtu Huyu Ndiyo Mwenye Fedha Unazotafuta.

By | November 17, 2016

Kuna swali moja muhimu sana la kujiliza kama unataka kuongeza kipato chako. Ni swali muhimu na sahihi ambalo litakupa jibu sahihi la hatua unazoweza kuchukua wewe ili kupata ile fedha unayotaka kupata. Kwa mfano, kama unataka kujenga nyumba, au kununua gari, au kununua chochote ambacho ni muhimu kwako, utaanza kujiuliza (more…)

UKURASA WA 686; Kitakachokufanya Uendelee Kutumiwa Na Wengine…

By | November 16, 2016

Wote tunapenda uhuru kwenye maisha, na mafanikio ya kweli yanakuja pale mtu anapokuwa huru. Hata kama utakuwa na kila unachotaka, kama utanyimwa uhuru wa kuwa na yale maisha unayotaka, hutaweza kuyafurahia maisha yako na hii itakufanya usione maana ya mafanikio yako. Pamoja na hitaji hili kubwa la uhuru, bado watu (more…)