Author Archives: Dr. Makirita Amani

About Dr. Makirita Amani

Dr. Makirita Amani ni daktari wa binadamu, mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali. Dhumuni lake kubwa kwenye maisha ni KUWASAIDA WATU KUBORESHA MAISHA YAO NA KUFIKIA MAFANIKIO MAKUBWA KUPITIA KAZI ANAZOFANYA. Mawasiliano 0717396253 email makirita@kisimachamaarifa.co.tz

UKURASA WA 665; Mipango Siyo Matumizi…

By | October 26, 2016

Kupanga ni hatua moja, kufanyia kazi mipango yako ni hatua nyingine, ambayo ni ngumu na ina changamoto zake. Kila mmoja wetu amekuwa anapanga mambo mbalimbali kwenye maisha yake, tumepanga mengi kulingana na malengo yetu kwenye maisha. Lakini mpaka sasa tumeshajifunza kitu kikubwa, siyo kila tunachopanga kinatokea kama tulivyopanga. Mara nyingi (more…)

UKURASA WA 664; Usilazimishe Kila Mtu Kuwa Mteja Wako…

By | October 25, 2016

Kinachowachosha wafanyabiashara wengi, na kuona biashara wanayofanya haiwezi kufanikiwa, ni pale wanapofikiri ya kwamba kila mtu anapaswa kuwa mteja wa biashara wanayofanya. Ni kweli unaweza kuwa na biashara ambayo inaweza kumfaa kila mtu, lakini siyo kila mtu anaweza kuwa mteja wa biashara yako. Badala yake wapo watu ambao wanafaa sana (more…)

UKURASA WA 663; Tatizo La Wanaokupinga Na Kukukataa…

By | October 24, 2016

Katika jambo lolote ambalo unafanya kwenye maisha yako, watajitokeza watu ambao watakupinga. Watakuambia haiwezekani au unakosea na maneno mengine ya aina hiyo ya kukatisha tamaa. Pia utakataliwa mara nyingi kwenye kile unachofanya, utahitaji msaada wa wengine na wao watakataa. Au utahitaji kuwashawishi lakini hawatakubaliana na wewe. Hii ni hali ya (more…)

FALSAFA MPYA YA MAISHA; Maadui Wakubwa Wawili (02) Wa Furaha Kwenye Maisha Yetu.

By | October 23, 2016

Dhumuni kuu la falsafa kwenye maisha yetu ni kutuwezesha kuwa maisha bora, yenye furaha na mafanikio. Na kama ambavyo tumeshajifunza tena na tena na tena, furaha yetu haitokani na kitu kingine chochote ambacho kipo nje yetu. Furaha yetu inaanzia ndani yetu, furaha hailetwi na vitu au watu, bali tunaitengeneza sisi (more…)

UKURASA WA 662; Msingi Huu Wa Fedha Haujabadilika Na Hautakuja Kubadilika…

By | October 23, 2016

Karibu kila siku huwa napata taarifa kutoka kwa watu juu ya fursa nzuri ya kutengeneza kipato kikubwa bila ya kutumia nguvu kubwa. Watu hawa wanaoleta fursa hizi wanakuwa wameshawishika sana juu ya fursa hizo walizopewa. Lakini kawaida yangu ni kuchunguza kitu kwa undani kabla sijakubaliana nacho au kukifanya. Mara nyingi (more…)

UKURASA WA 661; Zana Muhimu Unazohitaji Kwa Mafanikio Yako.

By | October 22, 2016

Kama jinsi ambavyo unahitaji zana ili kufanya kazi yoyote unayotaka kufanya, ndivyo pia unavyohitaji zana ili kutengeneza mafanikio yako. Hakuna kitu kinachotokea chenyewe, kila kitu kinatengenezwa. Na panapotengenezwa kitu, zana ni muhimu. Zana za mafanikio zinaanza na wewe mwenyewe, zinaanzia kwenye akili yako na mfumo wa maisha yako. Zana zifuatazo (more…)

UKURASA WA 660; Pata Cheti Hiki Ambacho Hakiwezi Kupotea.

By | October 21, 2016

Siku za hivi karibuni kumekuwa na matangazo mengi ya vyeti kupotea. Kila chapisho la gazeti lina zaidi ya ukurasa mzima wenye matangazo ya kupotea kwa vyeti. Kikubwa cha kushangaza ni kwamba sehemu kubwa ya vyeti vinavyotangazwa kupotea, vimepotea miaka mingi iliyopita. Vipo vyeti vinatangazwa kupotea miaka 10 mpaka 20 iliyopita. (more…)

Utaratibu Wa Kupata Kitabu Cha BIASHARA NDANI YA AJIRA.

By | October 21, 2016

Habari rafiki yangu katika mafanikio? Nichukue nafasi hii kukupa habari njema ya kwamba kitabu BIASHARA NDANI YA AJIRA, jinsi ya kuanzisha na kukuza biashara yako ukiwa bado umeajiriwa sasa kinapatikana katika mfumo wa kuchapishwa. Mwanzo kitabu hiki kiliatikana katika mfumo wa nakala tete (softcopy) ila sasa unaweza kukipata kama kitabu (more…)

UKURASA WA 659; Vitu Viwili Unavyopaswa Kuvichukia Kwenye Maisha Yako.

By | October 20, 2016

Hupaswi kuwa na chuki kwenye maisha yako, kwa sababu chuki inaharibu mambo mengi kwenye maisha yako, hasa chuki hiyo inapokuwa juu ya wengine. Lakini kuna vitu ambavyo tunapaswa kuvichukia, ili visiweze kukudhuru. Na kwa sisi wana mafanikio, sisi ambao tumekataa kuwa kawaida na kuamua kuwa bora zaidi, sisi ambao tunataka (more…)

UKURASA WA 658; Sababu Halisi…

By | October 19, 2016

Ni vigumu sana kujua sababu halisi ya watu kufanya kile wanachokifanya, kwa sababu mara nyingi hawatakueleza sababu halisi, hasa kama itakuumiza. Kuna mtu anaweza kugombana na wewe, anaweza kukukasirikia na hata kukujibu vibaya. Anaweza kukupa sababu ya yeye kufanya hivyo, lakini mara nyingi hiyo siyo sababu halisi. Huwa kunakuwa na (more…)