Author Archives: Dr. Makirita Amani

About Dr. Makirita Amani

Dr. Makirita Amani ni daktari wa binadamu, mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali. Dhumuni lake kubwa kwenye maisha ni KUWASAIDA WATU KUBORESHA MAISHA YAO NA KUFIKIA MAFANIKIO MAKUBWA KUPITIA KAZI ANAZOFANYA. Mawasiliano 0717396253 email makirita@kisimachamaarifa.co.tz

UKURASA WA 672; Zoezi La Kuitawala Fedha.

By | November 2, 2016

Watu wengi wamekuwa wakilalamika kwamba fedha inabadili watu, kwamba baadhi ya watu wamebadilika baada ya kupata fedha. Lakini ukweli ni kwamba, fedha haiwezi kumbadili mtu. Fedha inamboresha mtu kwenye kile ambacho tayari anacho. Kama mtu ana roho nzuri basi akiwa na fedha anakuwa na roho nzuri zaidi. Na kama mtu (more…)

UKURASA WA 671; Asilimia 1 Na Asilimia 99.

By | November 1, 2016

Kila tunachofanya kwenye maisha yetu, kina mchango kwenye mafanikio yetu. Inawezekana kuwa mchango chanya au mchango hasi. Inategemea ni nini umefanya na umefanya kwa kusudi gani. Pamoja na kila kitu kuwa na mchango wake, bado michango ya vitu unavyofanya haifanani. Kuna vitu ukifanya vina mchango mkubwa wakati vingine vina mchango (more…)

UKURASA WA 670; Tabia Mbili Kwa Kila Mjasiriamali Kuwa Nazo.

By | October 31, 2016

Kuna tabia mbili muhimu sana kila mjasiriamali anapaswa kujijengea. Hizi siyo tabia za kuzaliwa nazo, bali kila mtu anajijengea kadiri anavyokwenda na maisha yake. Kwa tabia hizi mbili, mtu ataweza kufanikiwa kupitia ujasiriamali. Tabia ya kwanza ni KUJUA WAKATI GANI WA KUCHUKUA HATARI. Maamuzi mengi kwenye ujasiriamali ni maamuzi ambayo (more…)

💥 #TAFAKARI YA LEO; JIDHIBITI MWENYEWE….

By | October 31, 2016

Habari za asubuhi ya leo rafiki yangu? Hongera kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo, ambapo tumepata nafasi nzuri ya kwenda kuweka juhudi zaidi kwenye kile tunachofanya. Hii ni nafasi ya kipekee rafiki yangu, tuitumie vizuri. Asubuhi ya leo tutafakati kuhusu KUJIDHIBITI WEWE MWENYEWE. Watu wengi wamekuwa wakikazana kutafuta (more…)

UKURASA WA 669; Toa Toa Toa… Omba.

By | October 30, 2016

Kanuni za maisha bora na ya mafanikio tunazojifunza sasa, siyo mpya, bali zimekuwepo tangu enzi na enzi. Tangu kuwepo kwa maisha ya binadamu, kanuni hizi zimekuwepo. Zimekuwa zinaleta majibu mazuri kwa wale wanaozitumia na kuleta majibu mabaya kwa wale ambao hawazizingatii. Watu wamekuwa wakipuuza na kutozingatia kanuni ndogo na muhimu (more…)

UKURASA WA 668; Vitu Vitatu Vinavyokutengeneza Wewe Kama Ulivyo.

By | October 29, 2016

Kila mtu ana upekee wake, hata mapacha wa kufanana waliozaliwa pamoja, bado wanakuwa na maisha tofauti wakishakuwa watu wazima. Hii ni kwa sababu kuna vitu ambavyo vinawajenga watu kuwa na maisha ambayo wanakuwa navyo, na vitu hivi vinatofautiana kwa watu. Uko hivyo ulivyo sasa, kwa sifa zote ambazo tayari unazo, (more…)

💥 #TAFAKARI YA LEO; ACHA SOKO LIAMUE….

By | October 29, 2016

Habari za asubuhi ya leo rafiki yangu? Hongera kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo. Ni nafasi ya kipekee kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa kwenye kile ambacho tumechagua kufanya. Tutumie muda wa leo vizuri rafiki. Asubuhi ya leo tutafakari kuhusu KUACHA SOKO LIAMUE. Kumekuwa na tabia ya watu kuponda (more…)

UKURASA WA 667; Umuhimu Wa Vitu Kwenye Maisha Yetu…

By | October 28, 2016

Kwenye maisha yetu kuna vitu ambavyo tumekuwa tunavipa umuhimu mkubwa sana. Tumekuwa tunaona bila ya vitu hivi maisha yetu hayawezekani kabisa. na tumekuwa tunang’ang’ania vitu hivi mpaka wakati mwingine kutuletea matatizo kwenye maisha yetu. Kwa kuona vitu fulani ni muhimu sana kwenye maisha yetu, tumekuwa ‘bize’ kupita kiasi, tukiamini kwamba (more…)

#TAFAKARI YA LEO; HAKUNA ANAYEKUJALI…

By | October 27, 2016

Hongera kwa siku hii nyingine nzuri sana kwako rafiki yangu. Ni nafasi bora na ya kipekee kwako kwenda kufanya makubwa. Tumia nafasi hii ya leo vizuri rafiki yangu. Asubuhi ya leo tutafakari kuhusu KUJALI KWA WENGINE. Mara nyingi tumekuwa tunashindwa kufanya mambo yetu kwa sababu tunaona wengine wanatufuatilia sana na (more…)

UKURASA WA 666; Hofu Inayotokana Na Kukosa Maarifa Sahihi…

By | October 27, 2016

Moja ya vitu vinavyopelekea watu kuwa na hofu na kushindwa kuchukua hatua, ni kukosa maarifa sahihi. Angalia watu wengi ambao wamekuwa wanapanga kuanza biashara lakini wanakuwa na hofu. Mara nyingi inatokana na wao kukosa maarifa sahihi ya kuanzisha biashara zao. Watafikiria namna biashara inavyohitaji kuendeshwa, na kuona hawawezi kila kitu. (more…)