Category Archives: #TAFAKARI YA LEO

#TAFAKARI YA LEO; KIKWAZO NI MATUMIZI MABAYA YA RASILIMALI…

By | May 4, 2021

Kutokufanikiwa kwako hakutokani na kukosa rasilimali, bali kunatokana na matumizi mabaya ya rasilimali ambazo tayari unazo. Mfano rasilimali kubwa kabisa ni muda na nguvu zako. Kila siku una masaa yale yale 24, kama hufanikiwi siyo kwa sababu umepunjwa muda, ila kwa sababu unautumia vibaya, kwa mambo yasiyo na tija. Kadhalika (more…)

#TAFAKARI YA LEO; KUMILIKI KAZI…

By | May 3, 2021

Kazi ndiye rafiki wa kweli, rafiki atakayekufikisha kwenye mafanikio makubwa lakini pia asiyekuwa na wivu wala kukatisha tamaa. Lakini kazi zote hazifanani, kuna kuifanya kazi husika, kuyasimamia wanaofanya kazi na kumiliki kazi inayofanyika. Japo zote ni kazi, ila kiwango cha malipo kinatofautiana sana. Wewe kazana uwe mmiliki wa kazi inayofanyika (more…)

#TAFAKARI YA LEO; NI MAAMUZI YAKO…

By | May 1, 2021

Pale maisha yako yalipo sasa ni matokeo ya maamuzi ambayo umefanya siku za nyuma. Hata kutokufanya maamuzi ni sehemu ya maamuzi, kwa sababu unakuwa umeruhusu wengine ndiyo wakufanyie maamuzi. Na ukifanya maamuzi halafu usichukue hatua nayo pia ni maamuzi umefanya kutokuchukua hatua na yamekufikisha ulipo sasa. Njia pekee ya kuyabadili (more…)

#TAFAKARI YA LEO; KAMA HAWAKUELEWI NI SAWA…

By | April 30, 2021

Kama watu wanakulalamikia kwamba hueleweki, hawayaelewi maisha yako hilo lisikusumbue sana. Maana hakuna yeyote anayeiona dunia kwa namna unavyoiona wewe. Imani, mtazamo, fikra na uzoefu ulionao ni wa kipekee, ukiishi kwa kuzingatia hayo, utakuwa tofauti kabisa na wengine. Na kuwa tofauti haimaanishi unakosea, bali inamaanisha unafanya kilicho sahihi kwako. Watu (more…)

#TAFAKARI YA LEO; KUWA MAKINI NA UNACHOFANYA…

By | April 28, 2021

Unaweza kuwa bize kweli kweli, kila siku unachoka sana, lakini unayofanya yakawa ni kikwazo kwa unachotaka. Hili ndiyo linazuia wengi wasifanikiwe, wanahangaika na mambo ambayo siyo tu hayawasaidii, bali pia yanawazuia wasipate wanachotaka. Kila unachofanya, jiulize kwanza kama kitakufikisha unakotaka na kuwa na ushahidi kutoka kwa wale ambao wameshafika unakotaka (more…)

#TAFAKARI YA LEO; KUPATA UNACHOTAKA…

By | April 27, 2021

Kupata chochote kile unachotaka, kunahitaji ushujaa wa hali ya juu sana, maamuzi ya kwamba lazima utakipata na ung’ang’anizi mpaka ukipate. Kama chochote kinaweza kukuzuia, hutapata unachotaka, lazima uwe ambaye huwezi kuzuiwa na chochote. Ambaye umeamua utapata unachotaka au utakufa ukiwa unapambana kukipata, hakuba chaguo jingine. Ukurasa wa kusoma ni mambo (more…)

#TAFAKARI YA LEO; MWENYE MACHAGUO MENGI NDIYE MWENYE NGUVU…

By | April 26, 2021

Kama mtu ana kitu ambacho watu wengi wanakihitaji na hawawezi kukipata pengine, huyo ana nguvu ya kukiuza kwa namna anavyotaka yeye. Kama watu wanaweza kupata wanachotaka popote, wana nguvu ya kuchagua wakapate wanachotaka wapi. Mwenye machaguo mengi ndiye mwenye nguvu ya kuamua apate kiasi gani kwenye majadiliano yoyote yale. Kama (more…)