2381; Ubahili ulio sahihi…

By | July 8, 2021

2381; Ubahili ulio sahihi… Siri ya utajiri ni ubahili, hiyo iko wazi na inajulikana na wengi. Lakini ubahili umekuwa unachukuliwa kwa mtazamo hasi, kama kujinyima na kuyafanya maisha kuwa magumu. Ubahili ni kuhakikisha matumizi yako hayazidi kipato chako. Na zipo njia za kuufanya ubahili kwa usahihi, ambapo maisha yako yatakwenda (more…)

#TAFAKARI YA LEO; CHAGUA KUELEWEKA AU KUFANIKIWA…

By | July 8, 2021

Vyote viwili haviwezi kwenda pamoja. Ukitaka ueleweke na kila mtu huwezi kufanikiwa. Na ukitaka upate mafanikio makubwa, huwezi kueleweka na kila mtu. Wanaofikia mafanikio makubwa wanajali zaidi ndoto zao kuliko wengine wanawachukuliaje. Wanaoshindwa wanajali sana wengine wanawachukuliaje kuliko wanavyojali ndoto zao kubwa. Kipenga kimepulizwa, unachagua upande upi? Ukichagua upande wa (more…)

2380; Usiangalie walipo sasa, angalia

By | July 7, 2021

2380; Usiangalie walipo sasa, angalia walipotoka… Nimekuwa nasema na ninaendelea kusema kwamba ushauri mwingi unaotolewa na watu waliofanikiwa siyo ushauri sahihi kwa wale ambao bado hawajafanikiwa. Na sababu kubwa ni mbili. Moja ni vingi walivyofanya, siyo ambavyo jamii inaweza kuelewa, hivyo wakivieleza wataonekana ni watu wa ajabu. Hata kama siyo (more…)

#TAFAKARI YA LEO; HAZINA YA BIASHARA YAKO…

By | July 7, 2021

Ni wateja ambao tayari walishanunua kwenye biashara yako na kuridhika na kile walichokipata. Ukishakuwa na wateja wa aina hii basi biashara yako ina hazina kubwa. Ni wateja ambao ni rahisi kuwashawishi wanunue tena, lakini pia ni wateja ambao wanaweza kuweta wateja wengine. Kila siku pambana kujenga hazina hii kwenye biashara (more…)

2379; Wateja Bora Wa Biashara Yako…

By | July 6, 2021

2379; Wateja Bora Wa Biashara Yako… Wateja bora kabisa wa biashara yako ni wateja ambao walishanunua kwako na wakapata kile walichotegemea kupata. Hawa ni rahisi kuwashawishi wanunue tena kuliko kuwashawishi wateja ambao hawajawahi kununua kabisa. Hivyo unapofanya biashara yoyote ile zingatia vitu hivi vitatu muhimu na ambavyo vitaiwezesha biashara kufanikiwa (more…)

#TAFAKARI YA LEO; WAPE TAARIFA MPYA…

By | July 6, 2021

Kama kuna watu unataka wabadili maamuzi na misimamo yao, usikazane kuwaonyesha kwamba wamekosea, badala yake wape taarifa mpya zinazowapa nafasi ya kufanya maamuzi mapya. Hakuna mtu anayependa kukiri kwamba amekosea, hivyo kuwaonyesha wamekosea kunawafanya wazidi kusimamia maamuzi yao. Lakini unapowapa taarifa mpya ambazo zinawapa mtazamo mpya, wanaamua wenyewe kufanya maamuzi (more…)

2378; Maamuzi Mapya Kulingana Na Taarifa Mpya…

By | July 5, 2021

2378; Maamuzi Mapya Kulingana Na Taarifa Mpya… Watu huwa hawapendi kukubali kama wamekosea. Hivyo watu wakishaonesha msimamo fulani, wataendelea na msimamo huo hata kama utawaonesha ushahidi mkubwa kwamba hawako sahihi. Hii ndiyo maana ubishani huwa hausaidii, kwa sababu kadiri unavyombishia mtu, ndivyo unazidi kumfanya asimamie upande wake. Maana alikubaliana na (more…)

#TAFAKARI YA LEO; UPO TAYARI KUTOA NINI?

By | July 5, 2021

Wengi wanapoyaangalia mafanikio, wanachoangalia ni wanakwenda kupata nini. Huo ni upande mbaya wa kuangalia maana ndiyo ambao kila mtu anauangalia na ndiyo maana wengi hawafanikiwi. Wewe angalia kwanza upande wa unatoa nini. Uko tayari kutoa nini ili uweze kufanikiwa? Mafanikio siyo rahisi na ndiyo maana wengi hawafanikiwi. Kikwazo kikubwa ni (more…)