UKURASA WA 1279; Kama Huoni Vitu Hivi Viwili Basi Haupo Hai…

By | July 2, 2018

Maisha yetu ni mkusanyiko wa matukio mbalimbali yanayotokea kwenye kila siku ya maisha yetu. Japokuwa tunaweza kuwa na lengo moja kubwa tunalofanyia kazi, lakini hatutaamka siku moja na kujikuta lengo limetimia. Badala yake kila siku tunapiga hatua kuelekea kwenye lengo lile kubwa. Sasa watu wengi huwa wanasahau maisha ya kila (more…)

#TAFAKARI YA LEO; USISINGIZIE KILICHOTOKEA, BALI HATUA ULIZOCHUKUA…

By | July 2, 2018

“It’s not what happens to you, but how you react to it that matters.” – Epictetus AMKA mwanamafanikio, Amka kwenye siku hii mpya, siku bora na ya kipekee kabisa kwetu. Ni nafasi nyingine nzuri sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana. Msingi wetu wa maisha (more…)

UKURASA WA 1278; Ili Kesho Iwe Bora, Ifurahie Leo…

By | July 1, 2018

Kama kuna ndoto za alinacha, basi ni ile hali ya watu kuishi hovyo leo wakiamini kesho itakuwa bora sana. Ile hali ya watu kuichukulia poa leo, kutokana na changamoto mbalimbali wanazopitia, wakiamini kesho itakuwa nzuri zaidi. Sikiliza rafiki yangu, jinsi unavyoichukulia leo, ndivyo utakavyoichukulia kesho. Kwa sababu hata kama changamoto (more…)

#TAFAKARI YA LEO; USIFANYE MAMBO KUWA MAGUMU ZAIDI YA YALIVYO.

By | July 1, 2018

AMKA mwanamafanikio, Amka kutoka kwenye ndoto za siku moja mambo yatakuwa mazuri na nenda kaweke juhudi kuyafanya mambo kuwa mazuri kweli. Tayari siku mpya, siku bora na ya kipekee ipo kwenye mikono yetu. Ni maamuzi yetu sisi wenyewe tuitumieje siku hii, kama tuitumie kwa kuzalisha na kusonga mbele zaidi. Au (more…)

UKURASA WA 1276; Fanya Kabla Ya Muda Uliokadiria…

By | June 29, 2018

Kuna makadirio mawili ambayo sisi binadamu hatujawahi kupatia kwa asilimia mia moja kwenye kukadiria. Makadirio hayo ni ya muda na fedha. Muda wowote utakaokadiria kufanya kitu, utahitaji zaidi ya hapo. Na kiasi cha fedha unachokadiria kutumia, utatumia zaidi ya hapo. Leo nataka tuzungumzie makadirio ya muda, hasa pale unapotaka kufika (more…)

#TAFAKARI YA LEO; KUWA MGUMU KWAKO MWENYEWE…

By | June 29, 2018

Siku mpya, Siku nzuri Na siku ya mafanikio. Hongera sana mwanamafanikio kwa siku hii nyingine ya kipekee sana kwetu. Ni nafasi nzuri kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana. Kwa msingi wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa TATUA, AMUA NA ONGOZA tunakwenda kufanya (more…)

UKURASA WA 1275; Aina Tatu Za Watu Katika Mahusiano Na Utoaji…

By | June 28, 2018

Kuna aina kuu tatu za watu katika mahusiano na utoaji. Na katika aina hizi, kuna moja ambayo watu wanafanikiwa sana wakati nyingine mbili watu wanaishia kuwa kawaida na hata kushindwa kabisa. Aina ya kwanza ni wachukuaji, hawa ni watu ambao wanataka kupata vitu kutoka kwa wengine. Wanapenda kunufaika wao zaidi (more…)