UKURASA WA 1288; Ufanisi Siyo Kufanya Kila Kitu, Bali Kufanya Yale Muhimu.

By | July 11, 2018

Katika mambo kumi uliyopanga kufanya leo, mawili mpaka matatu ndiyo muhimu zaidi. Hii ina maana kwamba ukifanya hayo matatu, ukayafanya vizuri, huna hata haja ya kufanya yale 7 yaliyobakia. Kwa sababu umehimu wa mambo hayo matatu ni mkubwa kuliko yale mengine saba. Pamoja na hili, watu wamekuwa wanakazana kufanya mambo (more…)

UKURASA WA 1287; Kulewa Kelele Na Kuogopa Utulivu…

By | July 10, 2018

Niambie katika hali kama hizi umekuwa unachukua hatua gani; Umeamka asubuhi na mapema, na huna ulichopanga kufanya kwa muda huo. Umeenda eneo ulilotakiwa kuwepo, labda kwenye mkutano au darasa, lakini tukio lililopaswa kuanza linachelewa kuanza tofauti na ilivyopanga, hivyo unakuwa na muda ambao huna cha kufanya. Unasafiri kwenda mahali na (more…)

UKURASA WA 1286; Kukwama Kwako Hakumsaidii Yeyote…

By | July 9, 2018

Kuna wakati mtu unakwama kwenye kile ambacho unakuwa umepanga kufanya, unakuwa umefika kwenye hali ambayo unaona huwezi kupiga hatua tena. Na hili linaweza kuwa halisi au inawezekana unalitengeneza. Linakuwa halisi pale unapokuwa umechukua hatua na kukutana na changamoto ambayo inakuzuia kuendelea kama ulivyotaka kuendelea. Na inakuwa siyo halisi, yaani unakuwa (more…)

UKURASA WA 1285; Ni Kwa Sababu Umechagua Kufanya, Na Siyo Kwa Sababu Inakubidi Ufanye…

By | July 8, 2018

Ipo misukumo ya aina mbili kwenye jambo lolote unalofanya kwenye maisha yako. Msukumo wa kwanza ni kwa sababu inabidi ufanye. Hapa ni pale unapofanya kitu kwa sababu huna namna nyingine, inakubidi tu ufanye, hata kama hutaki au hupendi kufanya. Kufanya kwa sababu inakubidi ufanye, mara nyingi hakuleti matokeo bora kabisa, (more…)

UKURASA WA 1284; Kabla Hujaanza Kufikiria Makubwa, Hebu Anzia Hapa…

By | July 7, 2018

Watu huwa tunafikiria makubwa, tuna ndoto kubwa sana kwenye maisha yetu, ndoto za kuibadili dunia na kuifanya kuwa sehemu bora kabisa ya kuishi. Lakini pamoja na ndoto kubwa sana tunazokuwa nazo, kuna mambo madogo mno yanakuwa yanatushinda. Kuna vitu vidogo kama kudhibiti hasira zako mwenyewe. Wengi huwa hatufikirii vitu kama (more…)

UKURASA WA 1283; Kumbuka Siku Ya Kwanza Na Ishi Siku Hiyo Kila Siku…

By | July 6, 2018

Chochote unachofanya kwenye maisha yako, hebu jikumbushe siku ya kwanza kabisa kufanya ilikuwaje? Kazi yako, kumbuka siku ya kwanza kabisa ulipoanza kazi, ulikuwa na hamasa kiasi gani, uliwahi kiasi gani na ulikuwa na utayari kiasi gani wa kufanya kila unachoambiwa kufanya? Kwa hakika hamasa ulikuwa juu, uliwahi sana na ulikuwa (more…)

UKURASA WA 1282; Mambo Haya Hutokea Kwa Kila Mtu…

By | July 5, 2018

Kila mtu kuna wakati fulani kwenye maisha yake anafanya maamuzi ambayo baadaye yanakuja kuwa mabaya kwake. Kila mtu kuna wakati ambapo anaangushwa, anaahidiwa kitu fulani na hakitekelezwi kama kilivyoahidiwa. Kila mtu kuna wakati anakasirishwa na vitu au watu fulani. Kila mtu kuna wakati anashindwa kupata majibu sahihi ya anachohitaji, au (more…)

UKURASA WA 1281; Kipi Kinaweza Kwenda Vibaya Zaidi?

By | July 4, 2018

Hili ni swali muhimu sana kujiuliza kwenye kila jambo unalofanya, swali ambalo litakuwezesha kujiandaa vizuri na pia kukuondolea hofu. Iko hivi rafiki, mambo mengi mabaya yanaweza kutokea kwenye chochote unachofanya. Ni uwezekano wa mambo haya mabaya kutokea ndiyo unawapa wengi hofu ya kujaribu vitu vipya. Kwa sababu wanafikiria kama mabaya (more…)

UKURASA WA 1280; Uwekezaji Mzuri Wa Muda Wako…

By | July 3, 2018

Wengi husema muda ni fedha, lakini hilo siyo sahihi, muda ni zaidi ya fedha. Na sababu pekee kwamba muda ni zaidi ya fedha, ukishapoteza muda huwezi kuupata tena. Poteza fedha na unaweza kutafuta nyingine, lakini ukipoteza muda, ndiyo umepotea moja kwa moja. Hivyo muda ni zaidi ya fedha, kama unahitaji (more…)