UKURASA WA 1229; Jinsi Ya Kutumia Nguvu Binafsi Kama Kipimo Cha Kipaumbele…

By | May 13, 2018

Una simu ambayo ina chaji asilimia 10, umeme umekatika siku nzima, halafu kuna simu ya muhimu sana unaisubiri, je unatumiaje ile asilimia kumi ya chaji iliyobaki? Je utaanza kusikiliza miziki au kuangalie video ulizonazo kwenye simu hiyo? Je utaingia kwenye mitandao ya kijamii na kuanza kuperuzi, uone wengine wanafanya nini? (more…)

#TAFAKARI YA LEO; USISAHAU KUJIPENDA…

By | May 13, 2018

“Don’t forget to love yourself.” -Soren Kierkegaard Hongera mwanamafanikio kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo. Ni nafasi bora na ya kipekee kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana. Kwa msingi wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa TATUA, AMUA NA ONGOZA tunakwenda (more…)

UKURASA WA 1228; Tabia Ya Kujificha…

By | May 12, 2018

Mafanikio yanakuja na hatari moja, kuwa kioo cha wengi, kuonekana na kila mtu na kuhukumiwa na hata wasiokujua vizuri. Kadiri unavyofanikiwa ndivyo watu wengi zaidi wanajua kuhusu wewe, na ndivyo wengi watakavyohiji, kukupinga na hata kuhukumu chochote unachofanya. Hali hii imekuwa inapelekea wengi kupenda kujificha, na sehemu nzuri ya kujificha (more…)

#TAFAKARI YA LEO; USIKUBALI KUVUTWA KILA UPANDE…

By | May 12, 2018

Do external things distract you? Then make time for yourself to learn something worthwhile; stop letting yourself be pulled in all directions. —Marcus Aurelius. Hongera mwanamafanikio kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo. Ni nafasi bora na ya kipekee kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora (more…)

UKURASA WA 1227; Kama Hufanyi, Unafanya Vibaya…

By | May 11, 2018

Kuna vitu ambavyo kila mtu anapaswa kufanya, lakini wengi hawajui kama wanapaswa kufanya, na wanaweza kujiambia kwamba hawafanyi. Wasichojua ni kwamba, chochote ambacho unapaswa kufanya halafu hufanyi, siyo kwamba hufanyi kweli, bali unafanya vibaya. Kwa mfano kila mtu anauza, na kila kitu kwenye maisha kinahusisha kuuza. Wale wanaojitambua kama wauzaji (more…)

UKURASA WA 1226; Kuyaelewa Maisha Na Kuyaishi Maisha…

By | May 10, 2018

Tunaweza kuyaelewa maisha kwa kuangalia nyuma, ni kwa kuangalia yale yaliyotokea ndiyo tunaweza kuelewa kwa nini yalitokea na matokeo yake yalikuwaje. Lakini hatuwezi kuyaishi maisha yetu kwa kuangalia nyuma, bali tunaishi maisha kwa kuangalia mbele. Hivyo tunayaishi maisha yetu kwa kuangalia mbele. Changamoto ya kuangalia mbele ni moja, hatuna uhakika (more…)

UKURASA WA 1225; Kipaumbele Cha Kwanza Kwenye Maisha Yako…

By | May 9, 2018

Kinapaswa kuwa wewe, kinapaswa kujifanya kuwa bora kila siku unayoanza kuliko ulivyokuwa siku iliyopita. Kinapaswa kujifunza vitu vipya. Kinapaswa kuwa mbunifu zaidi kuliko siku zilizopita. Cha kwanza unachofikiria kufanya pale unapoamka, pale unapopata muda wa bure ambao huna cha kufanya, hicho ndiyo umekipa kipaumbele kwenye maisha yako. Sasa hebu chukua (more…)

UKURASA WA 1224; Hukuzaliwa Kufikia Kila Kitu, Kujua Kila Kitu, Kujaribu Kila Kitu…

By | May 8, 2018

Ugonjwa mkubwa wa siku hizi, zama hizi za mitandao ya kijamii ni hofu ya kupitwa. Watu wanataka kuwa kila mahali kwa kila wakati, kujua kila kinachoendelea na kutokupitwa na chochote. Ndiyo maana wengi wamekuwa watumwa wa mitandao hii ya kijamii. Tafiti zimekuwa zinaonesha kwamba watu wanagusa simu zao mara nyingi (more…)